Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

[emoji38][emoji38][emoji38]..
No chadema NO CCM.
huo ndo u kweli
 
Sasa Hivi Tusubiri Adhabu ya wananchi ya Silent Demonstration “non violent confrontations “
Watanzania watabakia na hasira Ndani ya mioyo ambazo kizogo zilionyeshwa walipokataaa kujiandikisha Pamoja na kufoji idadi ya wapige kura ambayo ingekua rahisi kupika matokeo bado zinafanyika figisu !!!!

Ukitaka kula na kipofu usimshike mkono ; siku hizi hasira zitalipuka kama petrol au watu wakianza kuwatenda hao Viongozi huko mitaani Sijui tutamlaumu nani?
 
bado mnatulazimisha.
Mna Mnapenda kushinda kwa KISHINDO Leo imekuwaje?

MMEANZA KUUONA UMUHIMU WA CHADEMA SASA.

niliwahi kusema Bila vyama vingi magufuli asingekuwa RAIS.
maana hadi uwe rais nchi hii unatakiwa upigiwe kura tena ushindane na wapinzani anatakiwa awaheshimu Akina MBOWE.
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
 
Basi waandike barua ya kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wahusika yaani hao wasimamizi wa uchaguzi au msajili wa vya siasa,wakiainisha mambo ambayo hawakuridhishwa nayo katika mchakato mzima wa uchaguzi,hapo huenda msajili akakaa nao meza moja kujua nini kifanyike,kumbuka baada ya kugomea uchaguzi wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria,lakini pia wanaweza kupata mwanga wa chaguzi zijazo zitakavyosimamiwa,wasitangaze tu kwenye vyombo vya habari kisha wakaa kimya.hali itakuwa mbaya sana mwakani,yule dada wanamwita mange kimambi aliwahi kusema kuna uwezekano kusiwe na mbunge hata mmoja wa upinzani bunge la awamu inayofuata.dalili zimeanza kuonekana mapema kwenye huu uchaguzi, tunaelekea kubaya sio siri.
 
Mtu anapewa ridhaa na chama,sasa kma chama kimejitoa huyo mtu anapata wapi uhalali? unless kma sheria ina ruhusu mgombea binafsi mtuambie
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
 
Hiyo sio fiesta kuna taratibu zake kujitoa
Kila siku mnafanya makosa Yale Yale,hakuna uchaguzi rahisi Africa
Sasa mnalazimisha nini? Jafo si atangaze tu mmeshinda bila kupingwa? Kwanini mnateseka hivyo ccm?
 
Haijatumika demokrasia kuwakataza watu wasigombee

Mbowe ametumia ubabe
Siyo ubabe,iila sehemu au taasisi Ina msemaji wake.
Ikulu Ina msemaji wake.
Takukuru,jeshi,CDM,CCM na Kila idara.
Na ngazi ya juu ikishatoa maamzi kupitia vikao na tamko likatolewa huo ndo utakuwa msimamo was hiyo taasisi, either liwe jema au baya.
Hivo usiwalaumu CDM,kupanga Ni kuchagua
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea

Usichokijua ni kwamba katiba inasema mgombea yeyote lazima awe na udhamini wa chama cha siasa, kwa lugha nyingine ni kwamba katiba hairuhusu mgombea binafsi. Sasa CHADEMA kama chama kimetangaza kufuta huo udhamini kwa wagombea wake wote nchi nzima. Kwahio automatically wagombea wake wote wanapoyeza sifa ya kuwa wagombea kwa mujibu wa katiba. Kwahio hawawezi kugombea hata kama wangelitaka kuendelea na uchaguzi.
hapo upo?
 
Chama kimeondoa udhamini wake kwa mgombea anawezaje kuendelea kuwa mgombea wa hicho chama? Hivi zenu akili zimeshikiliwa na ccm?
Asante mkuu,umepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza.Akili lazima ziwarudi Jafo anataka kulazimisha kuweka majina ya wagombea wenye vyama vilivyojitoa,maajabu haya kwani hiyo inasaidia nini?
 
Kiukweli Chadema ni kichaka cha wakora,yaani kakikundi ka kina Mbowe na washirika wao wachache wanawatesa wanachadema nchi nzima ,aibu kubwa sana kwa wanachama wote
Hujajibu hoja iliyoko mezani umeishia kulalamika tu tukusaidieje?
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
Kuna mgombea anaegombea bila kupitishwa na chama? Hivi kwanini CCM tunaumia wakati apo ndo tumepata mteremko?
 
MATOKEO YA RUFAA ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA NOVEMBA 10.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO akizungumza Jijini Dodoma amesema katika zoezi la kuchukua fomu kuna makosa mbalimbali yalifanyika katika kujaza fomu nyingi ikiwa ni pamoja na kaukosea majina ya eneo pamoja na udhamini. .
.
Akizungumza jijini Dodoma JAFO amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya katika sehemu mbalimbali amegundua uwepo wa makosa hayo ambapo amesema baadhi ya maeneo wagombea wameigana na kufanya makosa yanayofanana. .
.
Amesema katika zoezi la kuchukua fomu asilimia zaidi ya 98 wagombea wamerudisha fomu na rufaa zaidi ya 13,000 zimewasilishwa ambapo kesho ndio rufaa zitatolewa ili kujua ngapi zimekubaliwa na ngapi zimekataliwa kwa wagombea wote waliowasilisha mapingamizi bila kujali vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi na watakaoteuliwa majina yao watakuwepo siku ya uchaguzi.
Mmekwama ndugu hayo madaraka mnayopata bila elimu au elimu za kufoji na huyo anayewapa hayo madaraka IQ ni below zero negative, yaani watu wajitoe ndio upitishe rufaa hiyo akili matope? Wananchi wanajua msimamo wa vyama kujitoa, jumuia za kimataifa zinajua msimamo wa vyama kutoshiriki uchaguzi huu haramu, sasa Jafo mnamdanganya nani?
 
Basi CDM waandike barua za kujitoa unless otherwise itakuwa Ni udaku Kama ubuyu mwingine wowote, huwezi amini kujitoa kwa mgombea wa CDM huku masebe lugoje kwa kauli ya Bwana furani dar es salaaaama runingani
Bado Tanzania hakuna wagombea huru, wote wanatokana na udhamini wa vyama. Hivyo kauli ya chama ikisema hiki ni haramu basi ni tamko la pamoja
 
Back
Top Bottom