Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Tell this Guy kwamba hatutakwenda kupiga kura....akabandike hata majina ya wake sake pia
 
Chama kimeondoa udhamini wake kwa mgombea anawezaje kuendelea kuwa mgombea wa hicho chama? Hivi zenu akili zimeshikiliwa na ccm?
Hawa watu wamechanganyikiwa. Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya Nchi. Sasa wao wameiheuza nchi kuongozwa kwa mawazo na mapendekezo ya mtu mmoja. Sasa madhara yameanza kujitokeza wao wanaogopa kumueleza mburugaji ukweli.
Binafsi namlaumu sana Rais aliyemaliza muda wake kumpitisha mvurugaji huyu kuwa mgombea wa chama kile.
 
MATOKEO YA RUFAA ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA NOVEMBA 10.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO akizungumza Jijini Dodoma amesema katika zoezi la kuchukua fomu kuna makosa mbalimbali yalifanyika katika kujaza fomu nyingi ikiwa ni pamoja na kaukosea majina ya eneo pamoja na udhamini. .
.
Akizungumza jijini Dodoma JAFO amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya katika sehemu mbalimbali amegundua uwepo wa makosa hayo ambapo amesema baadhi ya maeneo wagombea wameigana na kufanya makosa yanayofanana. .
.
Amesema katika zoezi la kuchukua fomu asilimia zaidi ya 98 wagombea wamerudisha fomu na rufaa zaidi ya 13,000 zimewasilishwa ambapo kesho ndio rufaa zitatolewa ili kujua ngapi zimekubaliwa na ngapi zimekataliwa kwa wagombea wote waliowasilisha mapingamizi bila kujali vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi na watakaoteuliwa majina yao watakuwepo siku ya uchaguzi.

Nilikuwa namuoma Waziri pekee anayejuwa anachokifanya lakini huu uchaguzi umemfanya Waziri ametapakaa matope sidhani kama atasafishika tena ndo anashuka watamtumia na kumtupa. Hakuna anayetakiwa kuonekana anafanya vizuri na kusifiwa zaidi ya Baba mwenye nyumba.
 
Bwana Jafo nimekusikiliza, nilichokielewa ni kwamba huko serikalini mnalishana upuuzi kisha mnataka kutuaminisha upuuzi wenu. Iharibuni tu nchi mkidhani ninyi mko salama kwa upuuzi wenu.
Ni hivi bwana Jafo, watendaji ni binadamu. Wamesema wazi kuwa walipewa maelekezo toka juu wasiandike chochote kwenye fomu za wapinzani, bali makarani wa Halmashauri watengeneze jedwali na kuwaandika upinzani kutoteuliwa na CCM wote kiteuliwa. Hivyo acha, uzushi wako unaotia hasira!!!
 
Sasa Hivi Tusubiri Adhabu ya wananchi ya Silent Demonstration “non violent confrontations “
Watanzania watabakia na hasira Ndani ya mioyo ambazo kizogo zilionyeshwa walipokataaa kujiandikisha Pamoja na kufoji idadi ya wapige kura ambayo ingekua rahisi kupika matokeo bado zinafanyika figisu !!!!

Ukitaka kula na kipofu usimshike mkono ; siku hizi hasira zitalipuka kama petrol au watu wakianza kuwatenda hao Viongozi huko mitaani Sijui tutamlaumu nani?
Hali itazidi kuwa mbaya kuliko ya Kibiti.
 
Chadema Imejitoa, Na Atakayegombea Atakuwa Amejifukuzisha Chama!Sasa Tuone Kama Mtakuwa Na Wagombea Wasotokana Na Chama Chochote!Afu Mtatueleza Mmetumia Katiba Ipi?
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
KWANI HUYO MTU ANAGOMBEA KWA TIKETI YA CHAMA GANI? KAMA CHAMA KIKIKATAA KUTOA IDHINI YA KUGOMBEA NANI ATASAINI FOMU YAKO? KAMA WATU WALISHAANZA FIGISU WAENDELEE NA FIGISU ZAO NA WASILAZIMISHE WATU WAKUBALI KUDHULUMIWA
TUSIHALALISHE UHUNI NA WIZI WA KIPUMBAVU HIVYO.
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
Hivi Tanzania mgombea binafsi anaruhusiwa?
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Chama kimesema kinajitoa unalazimisha utaweka jina lá mgombea.
 
Basi waandike barua ya kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wahusika yaani hao wasimamizi wa uchaguzi au msajili wa vya siasa,wakiainisha mambo ambayo hawakuridhishwa nayo katika mchakato mzima wa uchaguzi,hapo huenda msajili akakaa nao meza moja kujua nini kifanyike,kumbuka baada ya kugomea uchaguzi wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria,lakini pia wanaweza kupata mwanga wa chaguzi zijazo zitakavyosimamiwa,wasitangaze tu kwenye vyombo vya habari kisha wakaa kimya.hali itakuwa mbaya sana mwakani,yule dada wanamwita mange kimambi aliwahi kusema kuna uwezekano kusiwe na mbunge hata mmoja wa upinzani bunge la awamu inayofuata.dalili zimeanza kuonekana mapema kwenye huu uchaguzi, tunaelekea kubaya sio siri.
Barua wlishaziandika sana kuripoti rafu walizokuwa wakifanyiwa na chama dola kwa wahusika akiwemo Msajili mwenyewe bila kutoa au hata kuonyesha dalili ya ushiikiano kwao. Fanyeni uchunguzi kabla hamjakurupuka.
 
Na kama uliwaengua
Na kuwakata majina ya nini kuwarudisha?
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
 
Mtapata taabu sana 😂😂😂😂😂😂😂
 
Jafo Yuko sahihi.

Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
Uyo mgombea amegombea bila chama?? sasa kama chama kimeshaamua kujitoa ww mgombea unaenda kugombea kw chama kipi?

Mnajitoa fahamu kila kitu, Watanzania si wajinga wanaelewa kila kitu
 
Barua wlishaziandika sana kuripoti rafu walizokuwa wakifanyiwa na chama dola kwa wahusika akiwemo Msajili mwenyewe bila kutoa au hata kuonyesha dalili ya ushiikiano kwao. Fanyeni uchunguzi kabla hamjakurupuka.
Wewe ndio unakurupuka ,nimeongelea kuhusu huu uchaguzi na tamko hili la juzi kuhusiana na kujitoa kwenye uchaguzi.achana na barua hizo zingine ambazo hata msajili amewaandikia chadema kuhusu uchaguzi wao wa ndani.mimi naona upinzani wasipokuwa makini unakufa,kujitoa tu kwenye uchaguzi sio suluhisho ya changamoto wanazofanyiwa na chama tawala, sasa hata wenye viti wa serikalli za mitaa wakiwa ccm kazi hazitafanyika? Zitafanyika na maisha yataendelea, na hata asipokuwepo mbunge hata mmoja wa upinzani bungeni nchi itaenda tu,kwasababu hawaongezi wala kupunguza chochote kwenye utawala huu,wamekuwa hawana faida,yule mzee anawapuuza tu.hali mbaya sana demokrasia wakati huu kuliko wakati wowote toka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.
 
Anatakiwa atangaze mgombea aliyechukua fomu ndie atangaze kujitoa sio Chama.Chama hakikuomba popote kugombea.Hivyo hakina mandate ya kusema kinajitoa kwani chenyewe ndicho kilijaza fomu kuomba kugombea?
Kwa mfumo wa chaguzi zetu, ambazo hatuna fursa ya mgombea binafsi chama kikishakataa hakuna namna mgombea anaweza kubaki. Kumbuka chama ndicho kinachonipa fursa na dhamana. Sasa kama chama hakishiriki hawa watu wako wanashiriki kwa utaratibu upi?
 
Mtu anasema nimejitoa, sitaki, wewe unasema nitakuweka kwa nguvu! Jafo, hivi unakosa kitu gani/unapata hasara gani/ipi mtu akijitoa?
Huwezi Amina kwa wasiri ambaye Ni msomi kumlazimisha mtu abandikwe jina lake wakati mhusika ametangaza kujitoa Sasa lengo hatujui Ni Nini Kama siyo kutaka vurugu ili nchi yet iingie doa.haiingii akilini
 
Back
Top Bottom