Waziri Jafo: Hakuna mtendaji kufunga ofisi leo ili watu wote waliochukua fomu waweze kuzirejesha. Hakuna uchaguzi duniani usio na figisu figisu

Waziri Jafo: Hakuna mtendaji kufunga ofisi leo ili watu wote waliochukua fomu waweze kuzirejesha. Hakuna uchaguzi duniani usio na figisu figisu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Tamisemi mh Jafo amesema ni marufuku kwa mtendaji katika eneo lolote ndani ya JMT kufunga ofisi kabla wagombea watarajiwa hawajarejesha fomu zao labda kama mgombea huyo atakuja baada ya saa 10 kamili.

Kesho na keshokutwa ofisi zitapokea mapingamizi na tarehe 7/11 rufani zitasikilizwa

Tarehe 17/11/2019 kampeni zitaanza rasmi.

Mh Jafo amesema yeye ni Waziri kijana sana ndio maana uchaguzi huu umekuwa wa mafanikio makubwa ukilinganisha na chaguzi za siku za nyuma.

Jafo ameahidi kuchunguza malalamiko yote yaliyoripotiwa na hata sasa maafisa wake wametapakaa kila wilaya kukusanya data na malalamiko hayo.

Watendaji wengi wa kata wamewafanyia hujuma sana wapinzani hasa CHADEMA katika zoezi zima la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania Serikali za mtaa.

Jaffo amewataka wapinzani wajue kwamba hizo figisu ni za kawaida sana kwenye siasa kwani hata nchi kubwa mfano Marekani, Uingereza na Israel wanapitia figisu hizo.

Waziri Jafo amesema hayo akihojiwa mubashara na Janeth Mwakalinga wa Star tv.
 
Akiwa kwenye kituo cha Startv leo asubuhi, waziri wa TAMESEMI Selemani Jaffo amekili wazi kuwa watendaji wengi wa kata wamewafanyia hujuma sana wapinzani hasa CHADEMA katika zoezi zima la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania serikali za mtaa.

Jaffo amewataka wapinzani wajue kwamba hizo figisu ni za kawaida sana kwenye siasa kwani hata nchi kubwa mfano Marekani, Uingereza na Israel wanapitia figisu hizo.

Sambamba na hilo, mh Jaffo amewataka wapinzani wasiwe wachanga kisiasa kwani figisu kisiasa ni jambo la kawaida dunia nzima. Na pia amewataka wapinzani wapunguze kulalamika sana na wakomae kisiasa.

Maendeleo hayana chama.

CHanzo: Startv.
 
Bora hata amekuwa muwazi kabisa maana chadema tunalalamika mno bila kuchukua hatua na ndio maana kila siku ccm wanatupiga za usoni.
Hapa ndo utajua tungefanya maandamano ya ukuta na kata funua hawa watu wangekuwa na kaheshima kidgo.
Sasa tatizo sisi ni maneno mengi vitendo 0. Ona sasa wanavyotunyanyasa hawa raia na sisi tunalalamika tu bila kuchukua hatua mbowe baba sema neno tumechoka ala!
 
Siku raia wakikinukisha na mapanga mtaani kwenye uchaguzi, Jaffo arudie hii kauli yake. Maana hatambui kama hili swala linaweza kuleta machafuko.

Rwanda & Burundi walipopita 1994 ndio njia hio hio tunayopita Tanzania sasa hivi.
 
Alafu yakitokea ya kutokea tuombee amani na mshikamano sio. ..
Power is earned not given on a silver platter. .Opposition remember that....
 
Akiwa kwenye kituo cha Startv leo asubuhi, waziri wa TAMESEMI Selemani Jaffo amekili wazi kuwa watendaji wengi wa kata wamewafanyia hujuma sana wapinzani hasa CHADEMA katika zoezi zima la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania serikali za mtaa.

Jaffo amewataka wapinzani wajue kwamba hizo figisu ni za kawaida sana kwenye siasa kwani hata nchi kubwa mfano Marekani, Uingereza na Israel wanapitia figisu hizo.

Sambamba na hilo, mh Jaffo amewataka wapinzani wasiwe wachanga kisiasa kwani figisu kisiasa ni jambo la kawaida dunia nzima. Na pia amewataka wapinzani wapunguze kulalamika sana na wakomae kisiasa.

Maendeleo hayana chama.

CHanzo: Startv.
Imebidi nicheke tu! [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mh Jafo amesema yeye ni waziri kijana sana ndio maana uchaguzi huu umekuwa wa mafanikio makubwa ukilinganisha na chaguzi za siku za nyuma.
Naona amefurahi sana, mbinu aliyowapa watendaji imefanikiwa sana. Kigumu Chama cha Mapinduzi.
 
Anakiri kuwa hao vijakazi wao walikuwa wanafunga ofisi ili kuwanyima wagombea wetu fursa ya kuchukua fomu.
 
Kwa nini hizo figisu figisu hao watendaji wasiwafanyie CCM pia?. Inatokeaje ccm hawafanyiwi?. Na why figisu kutoka kwa watendaji not wanachama kwa wanachama?.
FIGISU hizi zilizobarikiwa katika ofisi hizo haziwezi kuwa ndio hizo hizo zilizoleta hasira watu wakaandamana hata Tukampoteza binti yetu Aquillina?.
Hizi figisu zinaishia kwenye Siasa tu au hata utoaji wa haki nyingine kwa wananchi?.
Kauli na maelezo dhaifu sana. Mimi ningekuwa Jafo , ningetafakari hizi kauli kisja ningejiuzulu.
Umetudharau sana Watz.Kama vile ujumbe ulikuwa unatumia kuku wasitafakari.
Acha ulevi wa madaraka boss.
 
Back
Top Bottom