johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Waziri wa Tamisemi mh Jafo amesema ni marufuku kwa mtendaji katika eneo lolote ndani ya JMT kufunga ofisi kabla wagombea watarajiwa hawajarejesha fomu zao labda kama mgombea huyo atakuja baada ya saa 10 kamili.
Kesho na keshokutwa ofisi zitapokea mapingamizi na tarehe 7/11 rufani zitasikilizwa
Tarehe 17/11/2019 kampeni zitaanza rasmi.
Mh Jafo amesema yeye ni Waziri kijana sana ndio maana uchaguzi huu umekuwa wa mafanikio makubwa ukilinganisha na chaguzi za siku za nyuma.
Jafo ameahidi kuchunguza malalamiko yote yaliyoripotiwa na hata sasa maafisa wake wametapakaa kila wilaya kukusanya data na malalamiko hayo.
Watendaji wengi wa kata wamewafanyia hujuma sana wapinzani hasa CHADEMA katika zoezi zima la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kuwania Serikali za mtaa.
Jaffo amewataka wapinzani wajue kwamba hizo figisu ni za kawaida sana kwenye siasa kwani hata nchi kubwa mfano Marekani, Uingereza na Israel wanapitia figisu hizo.
Waziri Jafo amesema hayo akihojiwa mubashara na Janeth Mwakalinga wa Star tv.