Waziri Jafo, siku nyingine uache kiherehere cha kufananisha Siasa na uweledi wa tiba za Kisayansi

Waziri Jafo, siku nyingine uache kiherehere cha kufananisha Siasa na uweledi wa tiba za Kisayansi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Wewe badala ya Kumuambia wazi wazi Boss wako kuwa Tanzania sasa hali ni mbaya dhidi ya Corona ukaona utafute Sifa mbele yake kwa kuja na Upuuzi wako wa Nyungu Season Two.

Haya sasa hii Nyungu Season Two yako ndiyo inatufyeka kweli kweli na Safari hii ikipiga huko huko juu mliko na muda si mrefu itamgusa Namba 1, 2 au 3 ndipo mtatia Akili.

Na kama kweli nawe unaamini Nyungu yako mbona unaingia Ofisini Kwako kwa Machale huku muda mwingi ukiwa na wasiwasi wa Kupata Corona?

Na usijisahaulishe tafadhali kuna Watu ulikuwa nao Juzi na nyepe nyepe (za chini ) zinasema Mmoja wao sasa Kaburi analiona kwa mbali huku Mochwari ikimkaribisha.

Yaani Ugonjwa umshinde Mzungu halafu Mzaramo wa Kisarawe auweze? Kuna Watu mna Upuuzi kweli kweli Vichwani mwenu. Haya njoo sasa na Nyungu Season Three yako ili uondoke nayo vizuri.
 
Ha ha ha mkuu umemnanga kweli, kwani nyungu saa hizi haisaidii kbs!?

Ila pamoja na hayo huu ugonjwa wa sasa hivi siyo masihara aisee na watu wengi wanauchukulia easy tu unapanda daladala hawana mask hawajali kbs mpk unajiuliza hawa watu wana shida gani yaani wao mpk waambiwe mvae mask ndiyo utawaona wanavaa ila mimi sijali sanitizer mfukoni mask usoni nyungu malimao tangawizi na maombi sisubirii tamko la yeyote afya yangu ni jukumu langu na si la yeyote.
 
Wale wote wanao mislead watanzania wanatakiwa wafungwe kwa kusababisha vifo!
.
654321097.jpg
 
wala sio mislead wale wanaowaona binadamu wengine ni wapumbavu ila wao ndio wana akili sana na hatari zaidi hawa ni wauwaji katika macho yangu.
Ingelikuwa wewe ndiyo Jafo ungeshauri Watamzania wafanye nini?
 
Back
Top Bottom