Pre GE2025 Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Pre GE2025 Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siwadanganyi nimefika gairo tu hapo, ndugu zangu, ukiona maaendeleo kwenye mji wako shukuru Mungu, ukiweza piga puli hadharani.

Example Temboni to matosa road, aisee ile njia ni hovyo, wakazi wa hapo wanaelewa, pata picha siku raisi anazindua ile barabara iwe na rami, tujiulize tu, wangapi watafurahi. A very simple example hata raisi awe mbowe.

Hospital au shule inafunguliwa eneo lako, kitu cha matamanio, kama raia this is a big thing, kama Kiongozi it's an achievement. Kongole serikali iliyo madarakani.

WAZIRI UNGEWEZA UNGEVUA HIZO GOLD UMPE RAISI, MKANDARASI AU HATA WANANCHI WALIPA KODI.

HONGERENI.
 
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.

My jicho ......

Tuseme kwamba huu ni uchawa au ni udhaifu kwa kiongozi kuonyesha kitu kama hichi kwani alishindwa kushukuru kawaida hadi kufanya alichokifanya binafsi natafsiri ni ushamba wa maarifa. Ifike mahali hawa viongozi wafanye mambo yao kwa uwelidi na sio kuongozwa na mihemuko fulani.

Soma Pia: Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara

Hii nchi tunaenda pabaya bila kitiba🤦🏾‍♂️
 
Kuna laaana Hapa.Mu

Mungu ndiye wa kuabudiwa Siyo MTU.
 
Tena! Maana kughalaghala huku kama sikosei kulishafanyika ama miezi ya mwanzoni mwaka huu au mwaka jana.
 
vijana wasio na utambulisho wa kitamaduni kuna tabu, mshangao na sintofahamu nyingi sana aise dah

hili nalo ni la kushangaza au kusikitisha kweli?....
Utamaduni wa Kingoni naufahamu na nafahamu hata Staili aliyofanya Inaitwa Kugalauka...

Ila Inashangaza Pale ambapo Utagalauka Bila Kufata Mavazi ya Kugalaukia...

Mfano ukimkuta Msichana Katembea Kifua wazi Halafu kavaa Suruali na High heels Na akakuambia kwamba Anatoka Ngomani Utamuamini ??

UTamaduni Wowote Ili uweze kutenganishwa na Ujinga,Utumwa Lazma kuwepo na Mavazi maalumu..

Imagine Unatoka Nyumbani kwako Unaona Watu zaidi ya Tisa wamevaa Suruali na Jinsi au Mavazi ya kawaida wana Marungu na Simu wameshika Mkononi Akili itakujia kwamba hawa Ni vbaka Vipi inafaa Kuwa uliza Kabila au Kujitetea Kwnza Roho yako??

Ila wakivaa mashuka ya Kimasai Huku wameshika Sime na Virungu amani inakuwepo tena unaweza hata Ukawasalimia huku ukitabasamu.

Mfano mwingine Ukiona Watu Zaidi ya Sita Wamekufata Njiani Wameshika Silaha za Moto Lazima utashtuka na Utajua lazma ni majambazi ila kuepusha hayo yote.

Kukawepo na Nguo maalumu za Kutambulisha kwamba Huu Ni utamaduni na Huu Ni Uhalisia..

Comrade Tusipofushwe na hata Vidogo Kwa umri wangu Nimeona Tamaduni Nyingi zikiwa Bado mbichi kabisa acha sasa Hivi Zimefifia na zingine zimekufa.

Na kwanini Zamani Hatukuwahi Kuwa Hivi? Kwani hatujawahi kuwa na Mawaziri Au Wabunge wangoni Enzi za Nyerere?, Mkapa?, Mwinyi? Kikwete? Unaweza kunionyesha Picha wakigalauka?

Kugalauka hakuna jinsia Umewahi kumuona Nape Akigalauka?
 
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake...
Mtu kama huyu ukiingia ofisini kwake bila kumsujudu utakoma.
 
Utamaduni wa Kingoni naufahamu na nafahamu hata Staili aliyofanya Inaitwa Kugalauka...

Ila Inashangaza Pale ambapo Utagalauka Bila Kufata Mavazi ya Kugalaukia...
wamama walilala Nape akatembea juu yao huko mtama. Lakini pia walitandika kanga ili asikanyage vumbi ni utamaduni wa huko kwao Lindi.

Lakini pia waziri Jenista Muhagama mara nyingi hugalagala kishujaa sana na hata kipindi cha Hayati JPM pamoja na wamama wengine wa huko songea.

Hata hivyo, mavazi husika hutumika tu kwenye sherehe husika za kitamaduni, vinginevyo kuonyesha vionjo vya kishujaa vya utamaduni wenu haihitaji ulazima wa mavazi ya kitamaduni.

Lakini pia, mimi mwenyewe, nikirudi Jimboni kwangu, mapokezi yangu kwa wananchi hua ni ya kishujaa na ya kipekee sana.

huwa navishwa baadhi vitu vyenye utambulisho wa kitamaduni, lakini pia napakwa majivu na unga wa kimjadi ambao ni mashujaa tu hupakwa.

Kiufupi, mtu asie na utambulisho wa yeye ni wa utamaduni gani akinitazama anaweza kudhani mimi ni mganga wa kienyeji, lakini ndio utamaduni wetu..

So, mie nadhani hakuna sababu hata moja, wala hakuna cha kushangaza kwa alichokifanya waziri Jenista Muhagama mbele ya Rais Jimboni kwake.

Kwangu mimi nampongeza sana waziri Jenista, kwa kuenzi kishujaa na kwa umahiri mkubwa sana utamaduni wa Kingoni, katika kushukuru viongozi wanaofanya vizuri 🐒
 
Ndio utamaduni wao. Nimeshuhudia mara kibao Jenista akija Jimboni wanawake wakigalagala kumshukuru kwa kazi nzuri. Ni haki naye kumshukuru kiongozi wake, sio uchawa…. ni utamaduni.
 
Ndio utamaduni wao. Nimeshuhudia mara kibao Jenista akija Jimboni wanawake wakigalagala kumshukuru kwa kazi nzuri. Ni haki naye kumshukuru kiongozi wake, sio uchawa…. ni utamaduni.
Hujawahi kusikia kuhusu utamaduni wa kipumbavu?

Kwa mfano kuna baadhi ya nchi ushoga upo kwenye utamaduni, ni sawa?
 
Back
Top Bottom