Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Kama suala liko mahakamani, Silaa ana haki ipi ya kuliingilia? Huo ndio upumbavu nilikuwa nausema.
Hajaingilia case iliyo mahakamani,

Amefuata umiliki wa sasa Kwa document zilizoko ardhi inaonyesha nyumba ni Mali ya marehemu,

Case iendelee lakini Mushi akiwa nje ya nyumba hiyo aliyoichukua Kwa nguvu ya pesa.
 
Hatari yake ipo huko huko ofisini kwake; na atakapokanyaga waya zinazogusa wateuzi wake, habari yake hutaisikia tena.

Naungana nawe katika kumtakia mafanikio. Wizara hiyo ni ngumu sana; lakini kijana anapambana vizuri sana kwa sasa.
 
Pumba tupu umeandika!!
 
Poyoyoo wwe! Hujui ulisemalo kaa kimya!!
 
Wwe lazima utakua wakili wa mchongo,na unae ishi kwa kesi za.Mchongo, nyinyi ndiyo kina mzee.mmasi mkisha zulumu.mnakimbilia Mahakamani ili kuhalalisha zuluma zenu!
 
Nikaona kuwa kuomba Mmassy ana experience ya kuhonga mawaziri Ili wapotoe HAKI.

Nchi hii tunawahitaji viongozi waliookoka Kweli Kweli wenye HOFU ya Mungu bila kujali vyama vya siasa watokako.
Ee Mwenyezi Mungu endelea kumbariki na kumlinda Mhe. Jerry Slaa, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa kazi kubwa ya kumsaidia kazi Rais wa JMT.

Asante sana kwa utendaji kazi uliotukuka katika kipindi kifupi tu baada ya kuteuliwa kuiongoza Wizara ya Ardhi.

Mfano hai ni Mama mjane wa Mjini Tanga aliyehangaishwa na mpangaji katika nyumba kwa miaka mingi mara baada ya mumewe kufariki dunia akitaka kumdhulumu mali halali waliyokuwa wanaimiliki na marehemu mumewe wakati wa uhai wake.

Ndugu zangu haki ya mtu haipotei, ndipo Serikali ya JMT kupitia Waziri mwenye dhamana ameagiza mama mjane arejeshewe nyumba yake mara moja baada ya Mhe. Waziri kukagua hati za umiliki wa ardhi na kujiridhisha kuwa nyumba ni mali halali ya mama mjane.

Wote twapaswa kuwa na hofu ya MUNGU hivyo tukumbuke na kuzingatia kuwa haki huinua Taifa bali dhuluma ni aibu kwa watu wote !
 
Nenda kasome Hukumu ya Mahakama Kuu ndiyo utajua issue ni jinai au siyo junai!!
Katika hao wote waliokamatwa mpaka sasa hivi ni yupi aliyefikishwa mahakamani?
Au anataka awapeleke jela moja kwa moja. Kwa sababu anaogopa akiwapeleka mahakamani watahonga majaji washinde kesi.
Yaani sijui watanzania ni nani katuloga..nahisi tulipata uhuru mapema sana..namlaumu chief mariale kwa nini aliacha kuendelea kudai uhuru wa kaskazini kwetu...huenda sasa hivi tungekuwa mbali sana.hili lichama la waswahili wa kariakoo linatuangusha sana
 
kweli binadamu hana shukrani,hata ukimbeba mgongoni na kumlisha atakutukana tu..
 
Subiri siku ukifa wwe ndiyo utajua ukweli wote!!
 
Kama suala liko mahakamani, Silaa ana haki ipi ya kuliingilia? Huo ndio upumbavu nilikuwa nausema.
Slahaa, Msajili wa.Hati pamoja na Commissioner wa Aridhi ndiyo wenye mamlaka na Aridhi na siyo Mahakama, Mahakama yake ni migogoro! Commissioner na Msajili wa Hati ndiyo wenye final say kwenye swala zima la Aridhi kuhusu umiliki wa Aridhi iliopimwa!!
 
Migogoro mingi ya ardhi chanzo ni wizara yake,

Na nafasi ya Waziri na maamuzi yake kupitia vikao na taarifa Ofisini kwake Ina umuhimu mkubwa.

Wengi hukosa HAKI wizara ya ardhi ndipo huenda mahakamani.

Kwa case ya Mmassy, tayari imetatuliwa Kwa 50%, mama yule atatumia utatuzi wa Waziri kama mojawapo ya ushahidi na kupata ushindi.

Si lazima kupinga Kila kitu.
 
Hatari yake ipo huko huko ofisini kwake; na atakapokanyaga waya zinazogusa wateuzi wake, habari yake hutaisikia tena.

Naungana nawe katika kumtakia mafanikio. Wizara hiyo ni ngumu sana; lakini kijana anapambana vizuri sana kwa sasa.
Ni kheri unafanya KAZI miezi SITA Kwa ubora ukafukuzwa kuliko kufanya miaka 5, na kisionekane chochote.

Wananchi tunatunza kumbukumbu Kwa matumizi ya baadae.
 
Ana kitu gani kwa kubomoa hovyo nyumba za watu bila kufuata sheria? Ndio kitu gani hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…