Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Kukataa rushwa kwa mwanachama wa ccm ni jambo jipya , ni maajabu na jambo lisiloaminika , Hata Dr Magufuli aliyejaribu kuwadanganya wanaccm wenzie kwamba hachukui rushwa , jambo hili lilimshinda .

Baada ya mdogo wa Rostam Aziz kukamatwa na shehena ya Meno ya Tembo na mamia ya bunduki za kivita zilizotumika kudungulia Tembo hao , Rostam Aziz aliingilia kati na kumhonga Magufuli na chama chake TV ya Channel 10 , hatimaye mdogo wake akaachiwa huru , ikimbukwe kwamba huyu Magufuli ndiye alisifiwa kwamba hachukui rushwa , Nani amesahau jambo hili ?

Sasa Kabla ya kutaka sifa tunaomba Jerry Silaa aweke ushahidi mezani ili tuthibitishe kwamba kakataa rushwa ndogo ya tsh mil 300 .

Labda kwa Wageni au labda na wale wasahaulifu ni kwamba , huyu Jerry silaa anayejinadi leo kukataa rushwa , ndio muasisi wa uporaji wa Masufuria yenye chakula ya Mama lishe alipokuwa Meya wa Ilala , natumai hakuna aliyesahau dhuluma ile , Hivi hata kwa akili ya kuvukia barabara , aliyepora masufulia ya ubwabwa ndondo wa masikini , anawezaje kukataa rushwa ya matajiri ya mil 300 ?
👍👏🤣
 
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi.

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu.

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.

I wish you a Merry Christmas 😀

======

Dar es Salaam

“Nimekataa Rushwa ya Tsh. Milioni 300”- Waziri wa Ardhi Mhe . Jerry Silaa

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa, ametangaza kusitisha matumizi ya kituo cha mafuta cha Barrel kilichopo Mikocheni, mkoani Dar es Salaam, kutokana na kituo hicho kujengwa bila kufuata utaratibu wa Wizara hiyo.

Mhe. Silaa amesema hayo alipotembelea eneo hilo, kilipojengwa kituo hicho, ambapo amebainisha kuwa, kuna watu walimfuata wakitaka kumpa rushwa ya Tsh. Mil. 300/= ambazo amedai amezikataa huku akibainisha kuwa ukichukua rushwa kila kitu utaona kipo sahihi.

Waziri huyo pia amewaagiza Wakuu wa Idara wa Ardhi na Mipango Miji nchi nzima kufanya uhakiki wa vituo vya mafuta vilivyo kwenye maeneo yao, kwa kuangalia matumizi yake pamoja na mchakato uliotumika kupatikana kwa viwanja hivyo
View attachment 2851260
Ilikuwa kauli ya kijinga sana toka kwa Jerry, yaani kukataa kwake rushwa kumefifishwa na hii kauli ya kijinga. Hata Bill gate bado anatafuta hela. Wala kuwa mtoto wa masikini au mkulima siyo sifa na haijawahi ila kila mmoja huelezea ukweli wa maisha yake. Yaani hata Dkt Samia ni mtoto wa maskini.
 
Pamoja na kwamba rushwa ni changamoto kubwa katika siasa zetu, Jerry anastahili pongezi nyingi kwa kupambana kwa maneno na vitendo. Amesema hadharani kwamba alipelekewa rushwa akakataa na amewaachisha watumishi kazi.
Baada ya kukataa rushwa alihakikisha anatoa taarifa TAKUKURU ili wahusika wafikishwe mahakamani?

Kama hajatoa taarifa ni muongo tu hakukataa rushwa bali anatafuta attention tu.
 
Sawa, je akiwa kama waziri amewachukulia hatua gani za kisheria hao waliotaka kumpa rushwa? Aliwaripoti Takukuru?.
 
Baba yake alikuwa Rubani kweli, njaa hatakuwa nayo, tunashukuru kukataa rushwa kubwa sana hiyo, familia za marubani wengi nazijua, wanaishi maisha mazuri sana na wengine wame invest sana.

Swali langu: TAKUKURU si mpo? Au hamsikii Waziri wa Ardhi alitaka kupewa rushwa ya mil 300, mbona mmekaa kimya as if hakuna kinachoendelea, PCCB si mko jamani, kamateni haraka hao watu wa BARREL OIL, au mpaka Mh Rais Mama Samia aseme muende kukamata?

TAKUKURU haraka sana mmerahisishiwa kazi, kamateni huyo mtoa rushwa na investigators waanze kuhoji haraka, narudia TAKUKURU mpo? Mh. Mama Samia anawaangalia tu, ooohh kalamu nyekundu sasa hivi itakula mtu.
 
Huyo muongo mkubwa!
Hiyo issue ya kituo cha mafuta Mikocheni imemkalia vibaya sababu kuna wastaafu wakubwa kwenye hilo sakata.

Kiongozi wao ni Mama Anna Tibaijuka.
Hivyo Slaa angekula hiyo pesa na uwaziri ndio ungekuwa bye-bye!
Hivi ninyi watu ni wajinga kiasi gani? Nani alikwambia kupokea rushwa ni ufahari? Kwanini hautaki kuamini kuwa kuna watu wana ethics zao?
 
Baada ya kukataa rushwa alihakikisha anatoa taarifa TAKUKURU ili wahusika wafikishwe mahakamani?

Kama hajatoa taarifa ni muongo tu hakukataa rushwa bali anatafuta attention tu.
Hiyo rushwa ya mawaziri na viongozi wakubwa (mamia ya mamilioni) haipelekwi mikononi kama ile 100,000 ya hakimu wa mahakama ya mwanzo.
Kukamata na kupata ushahidi wa kuthibitisha bila shaka yoyote (standard of proof in criminal case) siyo rahisi, bora jamii ielewe tu kwa ushahidi wa kimazingira.
Mitego ya moja kwa moja kwa TAKUKURU inafanikiwa kwa rushwa ndogo ndogo tu. Rushwa kubwa wanazuia zaidi kuliko kukamata.
 
Ilikuwa kauli ya kijinga sana toka kwa Jerry, yaani kukataa kwake rushwa kumefifishwa na hii kauli ya kijinga. Hata Bill gate bado anatafuta hela. Wala kuwa mtoto wa masikini au mkulima siyo sifa na haijawahi ila kila mmoja huelezea ukweli wa maisha yake. Yaani hata Dkt Samia ni mtoto wa maskini.
Rubani siyo tajiri, ni mtu mwajiriwa wa mshahara kama wengine, vinginevyo awe anamiliki na kuendesha ndege zake kibiashara.
 
Kibaya zaidi bora angekaa kimya,anajitangaza hadharani na kukitukana chama kuwa eti wanakula rushwa huku wakijiita watoto was maskini na yeye ni tajiri mkataa rushwa!!

Aiseh kacheza Boko,hiyo wanafiki ndani ya chama watasema anatukana chama huyu jamaa!!

Mengine tumwachie mungu!
Kale kaugonjwa ka kupumua ni shida !!
Nasikia huwa kanabeep na kupotea !!
 
Back
Top Bottom