Waziri Jumaa Aweso awataka Wananchi kulinda mazingira ya vyanzo vya maji kwa kuacha kukata miti ovyo

Waziri Jumaa Aweso awataka Wananchi kulinda mazingira ya vyanzo vya maji kwa kuacha kukata miti ovyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wananchi kulinda mazingira ya vyanzo vya maji kwa kuacha kukata miti ovyo na kufanya shughuli za kibinadamu ili kuepuka ukame.

Ametoa wito huo mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 2, 2025 yanayoendelea kwenye Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mhe. Aweso amesema kuwa uwepo kwa rasilimali za maji toshelevu ni usalama wa taifa kwakuwa uwepo wa maji ni uhakika wa chakula, nishati ya umeme pamoja na mipango ya kimaendeleo ambapo yote hayo yanategemea na mazingira endelevu.

Pia, Waziri Aweso alisema ni wakati sasa Watanzania watambue kuwa athari za mazingira ziwe funzo, akitolea mfano Mto Ruvu mkoani Pwani ulivyokauka kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yalisababishwa na binadamu wenyewe.

“Athari za mazingira ziko wazi kwa mfano ukienda Pangani athari zikio wazi, leo tunaona bahari imekula mji na hivyo kina cha maji kinaongezeka kina kwahiyo changamoto hizi za kimazingira tunazoziona sasa ziwe funzo kwetu,” alisema.

Pamoja na changamoto hizo, alishukuru na kuipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa mikakati thabiti na hatua madhubuti inazochukua katika kuyasimamia na kuyatunza mazingira.

WhatsApp Image 2025-06-02 at 14.38.09_4bacbc78.jpg

WhatsApp Image 2025-06-02 at 14.38.09_cbd71099.jpg
Amesema hayo yote yanafanyika kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa kusimamia agenda ya mazingira.

“Nashukuru kwa kupata nafasi ya kutembelea mabanda haya, hakika Ofisi ya Makamu wa Rais mmejipanga na sisi kama Wizara ya Maji tutaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuyalinda na kuyatunza mazingira ili kuhakikisha Tanzania inakuwa bora na salama, kama mtakumbuka tumefanya mabadiliko ya Sera ili yaendane na mazingira,” alisema Aweso.

Maonesho hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 5, 2025 ambayo itakuwa kilele chake.
WhatsApp Image 2025-06-02 at 14.38.08_f54333a4.jpg
 
Mbona wao hawalindi mali za nchi?? Mwambie aache usenge
 
Back
Top Bottom