Waziri kaambiwa na Rais ajitafakari, yeye na IGP hawauelewi msamiati huu?

Waziri kaambiwa na Rais ajitafakari, yeye na IGP hawauelewi msamiati huu?

Yaan kwa kiswahili fasaha kujitafakari ni kujipima kama una uwezo wa kuendelea na kazi uliyonayo.Unaweza kuachia ngazi au kubadilisha mwenendo wako ukaongeza bidii.Lakin naona wabongo wengi wamekalili kuachia tu ngazi.Nafikiri tusiwe na wivu na roho mbaya kwa wenzetu waliopo kwenye nafasi za kazi.Yaan ukifanya utafiti humu wengi hawawezi kumuombea mtu aendelee na nafasi yake na ajirekebishe.Watataka aachie ngazi wafurahi.Ndio tulivyo wabongo wengi.
Wewe ni Masauni mwenyewe au Siro
 
Matukio ya mauaji yamekuwa ni mwendelezo kwa kipindi chote cha Siro na sioni sababu ya yeye kuendelea kuwa ofisini. Haiwezikani IGP anakuwa kibwetele mbele ya Kingai,Mambo sasa,Jumanne na wengineo. IGP ni statue tu ipo pale ila inanimate tu
 
Wewe ni Masauni mwenyewe au Siro
Siro angejiongezea heshima yake kwa wananchi kama angeamua kuwachia ngazi.

Kwa umri wa huyu mzee wetu angeutumia muda huu kuwaachia wengine yeye akajipumzikie kijijini kwake.
 
Jana Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Mwanza, amemuambia waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni ajitafakari kwa mauaji yanayoendelea nchini.

Hadi Sasa waziri yupo kimya. Je yeye na IGP hawauelewi msamiati huu wa kiswahili?
Kiswahili kigumu
 
IGP afukuzwe kazi bila hivyo nchi itabaki hivi hivi, kila siku mauaji yatakuwa yanaendelea. Masauni inaonekana hawezi kumwambia chochote huyo IGP Sirro.
 
Hata kama wakielewa msamiati sidhani wako tayari kuwajibika. Utamaduni na kawaida za nchi hii ni vigumu mtu kuamua kuwajibika kwa makosa ya walio chini yake. Katika historia ya Tanganyika/Tanzania huru kuna exceptions chache za uwajibikaji wa ku step down. Tunatakiwa kubadilika. Mauaji ni moja ya makosa makubwa kufanywa. Kosa la mauaji linatosha kabisa mtu kujipima na kuamua kuondoka. Inakuwa heshima kubwa kwa aliyeamua kuondoka na pia heshima kwa taasisi au idara yake
Waziri na IGP need to do something.
 
Yaan kwa kiswahili fasaha kujitafakari ni kujipima kama una uwezo wa kuendelea na kazi uliyonayo.Unaweza kuachia ngazi au kubadilisha mwenendo wako ukaongeza bidii.Lakin naona wabongo wengi wamekalili kuachia tu ngazi.Nafikiri tusiwe na wivu na roho mbaya kwa wenzetu waliopo kwenye nafasi za kazi.Yaan ukifanya utafiti humu wengi hawawezi kumuombea mtu aendelee na nafasi yake na ajirekebishe.Watataka aachie ngazi wafurahi.Ndio tulivyo wabongo wengi.
"Wamekalili" ndio kiswahili gani hichi?
 
Jana Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Mwanza, amemuambia waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni ajitafakari kwa mauaji yanayoendelea nchini.

Hadi Sasa waziri yupo kimya. Je yeye na IGP hawauelewi msamiati huu wa kiswahili?

IGP na huyo waziri wote wanajua matokeo kwenye box la kura yalikuwaje na bado CCM iko madarakani, ni kipi kitawasukuma wao kuachia madaraka? Rais anajua yeye na chama chake wako madarakani kinyume na box kura, na huyo IGP ndio alitumika kwenye uchafu huo, ndio sababu rais hana nguvu ya kumtoa IGP.
 
Hapo zamani za kale 1976 kuna Waziri alijiuzulu kwa kashfa ya vifo ndani ya Wizara yake siku hizi haya hayapo
 
Back
Top Bottom