Waziri kaambiwa na Rais ajitafakari, yeye na IGP hawauelewi msamiati huu?

Wewe ni Masauni mwenyewe au Siro
 
Matukio ya mauaji yamekuwa ni mwendelezo kwa kipindi chote cha Siro na sioni sababu ya yeye kuendelea kuwa ofisini. Haiwezikani IGP anakuwa kibwetele mbele ya Kingai,Mambo sasa,Jumanne na wengineo. IGP ni statue tu ipo pale ila inanimate tu
 
Wewe ni Masauni mwenyewe au Siro
Siro angejiongezea heshima yake kwa wananchi kama angeamua kuwachia ngazi.

Kwa umri wa huyu mzee wetu angeutumia muda huu kuwaachia wengine yeye akajipumzikie kijijini kwake.
 
Yeye anataka mamlaka imnyofoe hapo ofisini. Haamini ushauri huu.
Nitaamini kama sasa mamlaka zina uthubutu kama watamuondoa huyo mzee hasa kwenye hii kashifa ya mauwaji.
 
Jana Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Mwanza, amemuambia waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni ajitafakari kwa mauaji yanayoendelea nchini.

Hadi Sasa waziri yupo kimya. Je yeye na IGP hawauelewi msamiati huu wa kiswahili?
Kiswahili kigumu
 
IGP afukuzwe kazi bila hivyo nchi itabaki hivi hivi, kila siku mauaji yatakuwa yanaendelea. Masauni inaonekana hawezi kumwambia chochote huyo IGP Sirro.
 
Waziri na IGP need to do something.
 
"Wamekalili" ndio kiswahili gani hichi?
 
Jana Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Mwanza, amemuambia waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni ajitafakari kwa mauaji yanayoendelea nchini.

Hadi Sasa waziri yupo kimya. Je yeye na IGP hawauelewi msamiati huu wa kiswahili?

IGP na huyo waziri wote wanajua matokeo kwenye box la kura yalikuwaje na bado CCM iko madarakani, ni kipi kitawasukuma wao kuachia madaraka? Rais anajua yeye na chama chake wako madarakani kinyume na box kura, na huyo IGP ndio alitumika kwenye uchafu huo, ndio sababu rais hana nguvu ya kumtoa IGP.
 
Hapo zamani za kale 1976 kuna Waziri alijiuzulu kwa kashfa ya vifo ndani ya Wizara yake siku hizi haya hayapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…