Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

hivi we jamaa una akili timamu kweli ?
 
Proffessa hapa unachomekea DELA better keep quite "disapered and died" maana yake nini Kwa hiyo yuko hai Azory?
 
Kwa nini unaamini ni suala la sentence structure na tafsiri ya lugha tu na si kile ambaçho kiko katika kichwa chake?
Kwa nini unataka kuuzika huu mjadala kirahisi namna hiyo?
Alipaswa kusema ‘waliopotea au kuuwawa’.

Siyo ‘waliopotea na kuuwawa’ maana hiyo inaacha mwanya wa tafsiri zingine.

Yeye kama mwanasheria nguli nilitegemea awe makini sana na uchaguzi wa maneno atumiayo.
 
Wakati Dr. Mahiga alipokuwa balozi wa Tanzania UN, aliletewa scandal alitulize na Kikwete.

Membe alilikoroga, ilionekana watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania, wengine wenye hadhi ya kibalozi, wanahusishwa na biashara za silaha na waasi wa Congo.

Membe alihojiwa na BBC, akakataa kijinga, katukatu, kama vile anajua nyendo za watumishi wote wa serikali ya Tanzania.

Kumbe BBC wakati wanamuuliza tayari wana ushahidi mpaka wa text messages za wafanyakazi wa serikali ya Tanzania.

Kesi akapelekewa Mzee Mahiga aitulize.

Nikawa namsikia anahojiwa na BBC. Kawanzia mbali, anawaeleza historia ya Tanzania kama msuluhishi wa migogoro, akaeleza tuna wakimbizi wengi, akawaeleza kwamba hatuna cha kufaidi ikiwa jirani zetu watapata maafa ya vita, tuna wanajeshi wengi wanalinda amani. Akaulizwa swali la mtegoi, anajua kwamba serikali ya Tanzania inahusika kuuza silaha?

Akajibu kwamba, serikali ya Tanzania haihusiki, ila hawezi kutoa jibu la uhakika kama watu ambao ni wafanyakazi wa serikali wanahusika wao binafsi kama wao si kwa niaba ya serikali, akasema wanaanzisha uchunguzi wa kimataifa kuchunguza na matokeo yatatangazwa.

Sikuisikia hiyo habari tena.

Nilisikia tu Balozi wa Tanzania Burundi karudishwa nyumbani.

Dr. Mahiga kukubali kwamba hawezi kujua kila kitu kuhusu wafanyakazi wa serikali wote sehemu zote muda wote, an unrealistic expectation, kuli defuse issue, ikatoka kwenye habari za serikali ya Tanzania inahusika, kwend kwenye inawezekana wafanyakazi wa serikali ya Tanzania wanahusika kama watu binafsi, uchunguzi unaendelea.

Mtu kama Kabudi anayejifanya anajua kila kitu, ni vigumu sana kukubali kakosea, au hajui kila kitu.

Na hiyo ni weakness, si strength.

Nasikitika sana wamemtoa Dr. Mahiga hapo foreign relations.
 
Usiwe mpambe mpaka ujitoe ufahamu na mnao wapamba wanawashangaa, mwenyewe amekiri kuwa alikosea na kusema mahojiano aliyoongea kiswahili ndio yachukuliwe yale ya kiingereza aliongea kitu asichokuwa na uhakika nacho..sasa wewe unatetea nini?
 

Just a simple plausible deniability! To a career diplomat, that’s easy work!
 
Waziri amechemka on camera. Maelezo yake yaliacha mwanya kwa watu kuwa na tafsiri sahihi kuwa Aazory Gwanda amefariki.

Kakosea kwanza kwa kusema hivyo, halafu anaendelea kukosea kwa kushindwa kuomba radhi na kukubali kosa, analaumu tafsiri.
Makonda alifanya hivi hivi kwa Mo Dewji na Mengi (RIP). Asubuhi anasema hivi jioni anasema vingine mchana.

Tatizo anaamini kuwa Watanzania hatujui Kingereza. Hiyo ameamua kutuchanganya ili tuchanganyikiwe.

Anachosahau ni kwamba wanaohoji siyo Watanzania peke yao na si kweli kuwa Watanzania wote hawajui Kingereza.
 
we nae ni mpuuzi kuna alichokiongea hakijaeleweka??, na kama yupo hai kwanini hajapatikana??.Hivi Azory alikuwa na uhasama gani na watu mpka wamteke?acha kutoa matapishi katika uhai wa Binadamu mwenzako tena Baba wa familia na mtegemewa wa familia yake. Idiot
 
OMG Palamagamba has just admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory has “disappeared and died”. How did Palamagamba know that Azory is dead? @CPJAfrica Amnesty https://t.co/EjCrH98MuI
 
hatumshangai hata Mwakyembe alishasema hatukumuelewa alisema kwenye bunge la katiba alipokuwa anapinga andiko/thethis yake ya Phd juu ya muungano uzuri ni kwamba mambo yakiandikwa hayafutiki.
Huyu nae anasema hatukumuelewa ? labda yeye ndiyo hajielewi ANZORY GWANDA KAUWAWA basi.
1. aKIONGEA kWA JAZIBA huku akipigiwa makofi bwana Magufuli ALIHOJI kwanini wanauwawa wa CCM tu? hapa alimanisha wauaji wale walikuwa wapinzani.
Akiandika humu JINGA LAO alishawahi kuhoji kwann gazeti la mwananchi linakuwa la kwanza kuripoti mauaji ya Rufiji kweli mwandishi AKAUWAWA
AKIONGEA BUNGENI wazir wa mambo ya ndani bwana Lugola alishawahi kusema Gwanda kaenda kutafuta maisha
 
Usiwe mpambe mpaka ujitoe ufahamu na mnao wapamba wanawashangaa, mwenyewe amekiri kuwa alikosea na kusema mahojiano aliyoongea kiswahili ndio yachukuliwe yale ya kiingereza aliongea kitu asichokuwa na uhakika nacho..sasa wewe unatetea nini?
Usiwe mpambe mpaka ujitoe ufahamu na mnao wapamba wanawashangaa, mwenyewe amekiri kuwa alikosea na kusema mahojiano aliyoongea kiswahili ndio yachukuliwe yale ya kiingereza aliongea kitu asichokuwa na uhakika nacho..sasa wewe unatetea nini?
unadhani kila mtu anaweza kupotoshwa kwa ulimwengu huu wa utandawazi? Prof. kasema kwamba mlishindwa kumuelewa na kuanza kumtafsiri vibaya lakini wewe unapotosha eti kakiri kukosea. Prof shikilia hapohapo kuna watu wanataka kupima fikra za kiprofesa kwa uzushi na upotoshaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…