Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

Proffessa hapa unachomekea DELA better keep quite "disapered and died" maana yake nini Kwa hiyo yuko hai Azory?
Labda mimi ni mshauri tu professor Kabudi asiwe na pupa na papara anapongea na wanahabari kiukweli kauli yake haikua ina maanisha kupotea na kufa. But since he is on the side of the government any slip of a tongue in such issues is taken terribly serious! He should calibrate himself and adopt such communication skills that leaves no loopholes for misinterpretation of his verbal contents.
 
mbona hatuulizi vifo vya wale wengine ambao ni viongozi wa serikali na wanaCCM, na polisi kule rufiji? au kwa kuwa ni wanaCCM vifo vyao haviumizi? aisee! kazi kweli kweli... leo swali linaulizwa juu ya alipo azory Gwanda huku anayeuliza anajua kabisa Gwanda tukio lake lilitokea kibiti ambapo kuna wengine wengi walipotea huko n wengine kufa lakini cha kusikitisha vifo vya wengine vimesahaulika, ni kwa sabbau gani?

Prof. Kawajibu vyema kwamba tukio lile kama linahusika na kibiti kuna wengine wengi walipotea na wengine kufa na si Gwanda tu lakini bado serikali inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo
Wewe akili yako ni mbovu sana. Hao wengine waliouwawa maiti zao zilipatikana. Azory yeye alifwatwa na kutekwa na wasiojulikana amboa kila mtu anajua ni kina nani?

Wakati mwingine uwe unatumia akili sio kuropoka kama jibwa. Fools
 
Labda mimi ni mshauri tu professor Kabudi asiwe na pupa na papara anapongea na wanahabari kiukweli kauli yake haikua ina maanisha kupotea na kufa. But since he is on the side of the government any slip of a tongue in such issues is taken terribly serious! He should calibrate himself and adopt such communication skills that leaves no loopholes for misinterpretation of his verbal contents.
waandishi wa habari ndio wanatakiwa wa- develop skills za kuwahoji maprofesa, inaonekana duniani kuna waandiahi wa habari wa chache sana wenye weledi , ujuzi na uwezo wa kuhoji maprofesa vizuri na mjadala ukawa mzuri kwa pande zote. Tumeshuhudia jana Zuhura Yunusi akiwa kabanwa na maelezo ya Prof mpaka kushindwa kuwa na attention nzuri. Yule mwenzake wa BBC FOCUS ON AFRİCA alikuwa anajitahidi kuachana na mjadala ambao mwisho wake ni kuaibika
 
Alipaswa kusema ‘waliopotea au kuuwawa’.

Siyo ‘waliopotea na kuuwawa’ maana hiyo inaacha mwanya wa tafsiri zingine.

Yeye kama mwanasheria nguli nilitegemea awe makini sana na uchaguzi wa maneno atumiayo.
Toka lini Kabudi akaweza kuchagua maneno? Once provoked yeye ndipo huwa ana react na kutoka kwenye mstari kirahisi sana... Na toka lini ukaona Police au mwanasheria akawa mudiplomasia?
 
Nimesikiliza mara kadhaa yale mahojiano yaliyofanyika kwa lugha ya Kiingereza. Nikasikiliza pia alipohojiwa kwa lugha ya Kiswahili. Hakuna mahali prof Kabudi amesema Azory kafa. Sasa nimeamini kwamba ni kweli kuna watu wanatumia kila njia kuichafua serikali na viongozi wa nchi. Ni bahati mbaya sana.
 
Ni kweli. Hajasema declaratively kuwa Azori kafa.

Ila, kwa maneno aliyoyasema, ameacha mwanya wa kutafsirika kuwa kasema hivyo.

Ni suala dogo sana la kubadilisha tu kiunganishi kilichotumika.
 
Ujumbe tulioupata hapa ni kurudi darasani kujifunza lugha upya. Maana ni wengi tumemuelewa tofauti na alichokusudia kutueleza.
Darasani rudi mwenyewe, wengine tumemuelewa pasi na shaka
 
Yeye ndiye anapaswa kurudi darasani kujifunza tofauti ya "disappeared and died" na "disappeared or died".

Kama hawa ndio watu wanaosimamia mikataba yetu, si ajabu tunapigwa changa la macho kila siku.
Na anajiita prof nguli wa sheria!!!
 
Mwafrica akizungumza kitu chukua neno la kwanza tu , sisi tunachochukua ni ile kauli yake ya kwanza tu , hizi porojo zingine za akina Abbas hatuzitambui
Kama anakanusha kua hajafa maana yake anatuambia bado yupo hai.
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas amemnukuu Profesa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia amesema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi amesema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."
Mwambieni sisi siyo wanafunzi wake aliokuwa anawakosesha kwa makusudi
 
Nimesikiliza mara kadhaa yale mahojiano yaliyofanyika kwa lugha ya Kiingereza. Nikasikiliza pia alipohojiwa kwa lugha ya Kiswahili. Hakuna mahali prof Kabudi amesema Azory kafa. Sasa nimeamini kwamba ni kweli kuna watu wanatumia kila njia kuichafua serikali na viongozi wa nchi. Ni bahati mbaya sana.
Utakuwa hauko sawa, au tuliyosikiliza sio uliyoisikiliza
 
Usiwe mpambe mpaka ujitoe ufahamu na mnao wapamba wanawashangaa, mwenyewe amekiri kuwa alikosea na kusema mahojiano aliyoongea kiswahili ndio yachukuliwe yale ya kiingereza aliongea kitu asichokuwa na uhakika nacho..sasa wewe unatetea nini?
Mtz ukimpa fursa ya kuongea Kwa Kiswahili atakudanganya Sana, mpe SASA aongee Kwa kiingereza ataongea ukweli mtupu,

Sisi ile version ya kiingereza ndio ukweli mtupu, Hiyo ya Kiswahili ni upupu mtupuuu
 
Back
Top Bottom