Waziri Kabudi: Tutazungumza na NSSF kuhusu hatma ya mafao ya uzeeni ya Waandishi wa Habari

Waziri Kabudi: Tutazungumza na NSSF kuhusu hatma ya mafao ya uzeeni ya Waandishi wa Habari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palagamba Kabudi amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia suala la mafao ya Uzeeni ya Wanahabari kutokana na baadhi yao kupitia changamoto ya kiuchumi wanapozeeka.

Amesema hayo katika Mkutano wake na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji, leo Desemba 18, 2024 ambapo amesema Serikali inatakiwa kuzungumza na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuona namba ya kuwasaidia Waandishi kuhusu mafao yao.

Mara kadhaa na kwa nyakati tofauti, Wadau wa JamiiForums.com wametoa maoni na malalamiko wakidai Wamiliki na Viongozi wa Taasisi nyingi wamekuwa wakiwakata Waandishi makato ya NSSF katika mishahara yao lakini hawayafikishi sehemu husika.

Pia soma
~
Waandishi wa Habari Azam wanataabika Mikoani, wanahitaji msaada kulipwa stahiki zao
~ CCM lipeni haki za waandishi wenu (NSSF na madai mengine)
~ Tumeachishwa kazi kihuni na Global Publishers, wanataka kutudhulumu haki zetu, tufanye nini?
 
Serikali iweke takwa Kila Chombo cha habari kiwe kinatoa Mkataba wa ajira sambamba na kuwakata michango na kuiwasilisha NSSF

Kwa maana hakuna atakaye endelea kuwa Kijana mpaka kufa kwake

Haiwezekani mtu unakuta anafanya kazi maybe Ayo TV, ama IPP lakini hadi anazeeka hana cha maana alichofanya. Na Siku akiugua, inakuwa ni mateso Kwa familia

Haipendezi Waandishi wa habari kuishi Kwa Posho tu za kupewa wanapoarikwa kwenye baadhi ya matukio
 
Aachen maneno ya kitapeli. Wakati sheria ya kikotoo inapita alikuwa bungeni. Hilo jambo lipo kisheria siyo habari ya kukaa kuongea na NSSF.
 
Back
Top Bottom