Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Kalemani is very right.

Hakuna chanzo cha umeme cha bei rahisi kama cha maji Duniani. Hakuna.

Mhongo ni mganga njaa tu.
Tafiti za taasisi zinazohusika na nishati zimeonyesha nishati ya solar na upepo ndiyo ya gharama nafuu kuliko zote. Endelea kushangilia uongo wa mataga.
 

Chernobyl haikuwa kinu cha kuzalisha umeme
Zilikuwa nuclear za matumizi ya kutengeneza silaha..
Fossil fuels za umeme wa nuclear technology ya usalama ime develop sana
 
Wachache sana watakuelewa mkuu. Manake naona wengi ni wale wakusikia tu na kukubali bila kufanya analysis.

Ukweli ni kama ulivyosema hapo; umeme wa maji siyo wa uhakika kwenye "digital economy". Na hiyo ndo point kubwa ya Prof Muhongo. Mabadiliko ya Tabia nchi na matatizo mengine ya kimazingira pamoja na sensitivity ya "social ecological systems", kutegemea maji kama chanzo kikuu cha umeme ni ujinga.
 
Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Gharama za ujezi wa vinu vyake na risk ya uvujaji wa mionzi yake ambayo ina madhara makubwa kwa mazingira na viumbe.

Umeme wa maji... pamoja na urahisi wake, pia ni rafiki endelevu wa mazingira.
 
Prof Muhongo yupo Bungeni maana siku kadhaa nyuma nilimsikia kwamba umeme wa gesi ndio wa gharama nafuu na wa uhakika ukilinganisha na huu wa kizamani wa maji.
Tulipofikia, unaweza kuwapa mtihani mmoja wahitimu wa darasa la saba na maprofesa na madokta na wahitimu wa la darasa la saba wakafaulu mtihani huo kuliko hao wengine.
 
Hiyo analysis iko wapi mbona haiweki tuone ili tulinganishe? Muhongo atawadanganya nyinyi wavivu na msiojua kuwa usomi ni kuprove empirically sio suala la kusadikisha watu.

Eti unasema waziri hajaangalia investment cost , hiyo investment ya bomba la gesi tu unajua ni trilioni ngapi ?
 
Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Nyuklia unaipataje.?
 
Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Mkuu umeme wa maji athari zake bado ni ndogo ukilinganisha na vyanzo vingine na hata hizo athari zake tunaweza kupambana nazo tukaziovercome hata kwa nusu yake kwa hata kampeni za kupanda miti.

Na tukizingati athari za Mazingira Nuclear ni hatari zaidi ya vyanzo vyote.
Maana Uranium hata baada ya kutumika huendelea kutoa mionzi kwa kipindi hata cha miaka 100 na zaidi ambayo huathiri mazingira na viumbe hai.

Pia hadi leo hii wataalam wa Nuclear bado hawajagundua njia madhubuti ya kudisposal nuclear wastes mara baada ya matumizi, kwani njia inayotumiwa hadi leo hii ya ni ile ya kufungia nuclear wastes kwenye mitungi mikubwa ya chuma na kudisposal baharini au kuyachimbia chini sana ardhini.
 
Dr Muhongo hajaongopa amesema ukweli kuwa itachukua mda mrefu, kama miaka 10 mpaka 15 ili kurudisha return kama umeme utauzwa kwa TSH 36.00 per unity toka mwanzo, kama alivyosema waziri.

Kama umeme utakaozalishwa na bwawa la Nyerere utauzwa kwa Standard Prize ya $ 0.05 ambazo sawa na TSH 116.00 per Unity, itachukua miaka mitatu mpaka minne kuweza kurudisha hela za investment. Baada ya hapo ndiyo bei inaweza ikapunguzwa kuwa TSH 36.00 per Unity.

Nimetoa hapa hesabu ndogo za arthmetic ambazo kila mmoja aliye enda shule kidogo anaweza akazipata. Katika mahesabu inaonyesha kwamba TSH Trilion 7 tutazopata baada ya miaka kumi na TSH Trilion 11 tunazopata baada ya miaka mitano. Ghrama zote za mradi ni TSH Trilioni sita mpaka saba.

 

Professor Muhongo ni Muongo na Tapeli mkubwa.

Anatunganya Watanzania ili awatapeli wawekezaji. Imekula kwake!
 
Sawa basi
Tuweke mchanganuo wako wa gharama
Tutofautishe na ya waziri

Ova
hujanielewa sizungumzii kuhusu huo mchanganuo nazungumzia kwa ujumla jinsi wataalamu wanaweza kujenga hoja za msingi na zikaleta ushawishi kwa wanasiasa na tija kwa taifa.

kikawaida wanasiasa wanatakiwa wawategemee wataalamu katika kujenga hoja kwa wananchi na jamii na sio wataalamu kuwasikiliza kwanza wanasiasa.

wataalamu wanatakiwa waelewe kuwa wao ndio wana vision itakuwaje na tutapata nini na wanasiasa wabaki na mission yaani tunafanyaje kufikia tunachotaka kitokee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…