Waziri Kamwelwe atangaza mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Coronavirus kwenye vyombo vya usafiri

Waziri Kamwelwe atangaza mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Coronavirus kwenye vyombo vya usafiri

Huyo waziri hajawai kuwa serious vikao vya nn tena wakati hapo ni ishu ya kutoa maagizo ya level seat !!

Waziri wa Kazi naye ajaribu kuongea na waajiri watoe likizo ya mwezi kwa baadhi ya wafanyakazi ili kupunguza mrundikano maeneo ya kazi na public transport mfano mzuri Google na Facebook wamepunguza wafanyakazi kwa kuwapa likizo na baadhi ya kazi zinfanywa majumbani sio maofisini.
 
Ni wazo zuri pia.
Pamoja na jitihada zote hizi nadhani ni wakati muafaka kama wachangiaji wengi walivyokwisha shauri mtandaoni kupanua wigo wa tiba na kuweka maeneo mengi ya kupima hali za watu.
Jambo la kushangaza kuona watu wanatembea na maski na glove barabarani. Tumeona hata kiongozi fulani akiwa kwenye vyombo vya habari amevaa maski! Elimu ya matumizi ya hivi vitu wananchi wanatakiwa kuieelewa
yuko msemaji amelisemea hili na kwa kweli unapokaa na maski kwa masaa zaidi ya matano nini kinafuata, si ni ugonjwa mwingine kwako mhusika.
Hivi kweli kama serikali na afya wako wamejipanga LEO hii wakiamua kupima watu 100 nadhani majibu yake yatawashangaa watu kwa namba itakayojitokeza! Tusidahani tu kwa maneno kuwa tumedhibiti ugonjwa na kufunga shule. Hebu pimeni watu 100 majibu yatapatikana.
Linalojitokeza huko America kwa namba kupaa juu kila siku ni maajabu kwani ni kila jimbo lina mgonjwa sasa. Hebu wizara husika mjiongeze na mtoe vipimo kwa watu kwa hiari mikoa walau kumi mtapata jibu halisi na mkakati uanzzie hapo badala ya kukaa kwenye vyombo vya habari kuelezea kuwa tumedhibiti. nawaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena huu utaratibu wa Level seat usiishie hapo baada ya corona uendelee daima ili tusahau kabisa ishu za kusimama kwenye daladala.
 
March 18, 2020

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Eng. Isack Kamwelwe atoa tamko kufuatia Coronavirus Covid-19.

Tamko hilo la Waziri Isack Kamwelwe linahusu sekta ya usafiri wa barabara, reli, anga na majini linataka wenye vyombo vya usafiri na watumiaji kuchukua tahadhari kubwa kufuatia ugonjwa huo kufuatia tangazo la Wizara ya Afya kuthibitisha ugonjwa huo upo Tanzania.



  1. Kampuni za usafiri wafungue vituo zaidi vya kukatia tiketi nje ya vituo vikuu vya usafiri.
  2. Tiketi za kieletroniki ziamzishwe kupunguza msongamano.
  3. Wafanyakazi na abiri watumie sanitizier mara kwa mara kusafisha viganja vyao washikapo nauli, chenji, kushika viti n.k
  4. LATRA, TBS, na wizara ndani ya siku tatu waamue ni idadi gani ya abiria wawemo katika chombo cha usafiri ili kupunguza uwezekano wa maambukizi.
  5. TAZARA na TRC wahakikishe vifaa vya kusafisha mikono viwepo stesheni na katika treni.
  6. Mamlaka za usimamizi wa bandari na zile za viwanja vya ndege kwahakikishe kuwapo na vifaa vya kusafisha mikono n.k katika maeneo yao.
  7. Taasisi zote za usafiri zishirikiane na wizara ya Afya ili kuweza kuchapisha na kubandika matangazo yenye habari sahihi juu ya namna ya kuwa safi na pia kuzuia kusambaa ugonjwa wa Covid19 Coronavirus.

Source: Global TV online
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi a mawasiliano ameitaka mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini ( Latra) kukutana mara moja na kutoa mwongozo juu ya idadi ya abiria wanaoruhusiwa kusimama ndani ya daladala na Mwendo kasi ili kupunguza msongamano.

Waziri Kamwele ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa anaelezea hatua zinazochukuliwa na wizara yake ili kujikinga na virusi vya korona.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

Are these people kidding..!?People should be at least 6 feet apart for effective social distancing.

Under current seating style on public transport, anyone can contract covid-19 from the person sitting next to them.

If public transport must operate, there should be at least one person after every other seat and windows may be left open.
 
Wataalamu wa afya wanasema TB inaambukizwa kwa njia ya hewa, na imekuwepo siku zote hapa Tz, na kila siku kuna zaidi ya watu 500 wanakufa au kuambukizwa TB hapa Tanzania na hakuna hatua zozote za kupambana na msongamano wa kwenye basi au daladala zimekuwepo ili kupunguza maambukizi ya TB.

Sasa waziri anataka kusema nini haswaa?
Corona ndio inatushinikiza hivi?
Hivi waziri anajua Corona si kitu mbele ya TB?
TB inatibika, hata Corona ikipatikana dawa maisha yatakuwa kama kawa tu.
Tatizo Corona haina kinga wa tiba.
 
Kwani miongozo ya abiria wangapi wanatakiwa kwenye chombo cha usafiri husika hakuna Tz?
 
Huu ugonjwa unapaishwa Sana, m'bongo hafi kwamafua. Tusipotezeane muda nakuyafanya maisha kuwa magumu.
 
Watuache tu hatuwezi kufa kwa mafua tu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi a mawasiliano ameitaka mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini ( Latra) kukutana mara moja na kutoa mwongozo juu ya idadi ya abiria wanaoruhusiwa kusimama ndani ya daladala na Mwendo kasi ili kupunguza msongamano.

Waziri Kamwele ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa anaelezea hatua zinazochukuliwa na wizara yake ili kujikinga na virusi vya korona.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom