Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Kama kweli akitekeleza itakuwa ni faraja kwa wanaharakati wa mazingira, na wananchi wa maeneo hayo. Kimekuwa ni kilio cha miaka mingi.

Binafsi JPM akifanikiwa hili nitaamini kuwa hata kwenye makinikia alikuwa na nia njema, iwe amefanikiwa au hakufanikiwa.
 
Mwinyi aliuza kipande cha ardhi kwa mwarabu enzi zake tena kwa mkataba mreefu. Ortelo ni hatari sana, walijenga uwanja wao wa ndege, ndege kubwa zinatua na kupaa na mzigo bila ukaguzi, kila aina ya mnyama [isipokuwa faru] alihamishwa mzima mzima akiwa bado mchanga. Zoo zao zimejitosheleza kwa wanyama pori aina karibu zote zinazopatikana Serengeti.
 
Mkuu huyu Mwarabu akiondolewa kweli nitafurahi. Amenyanyasa sana wazawa, ole wako upotee njia upitie karibu na kambi yao, adhabu utakayopata utajuta kuzaliwa Tz. Huyu yuko karibu kabisa na Geti la serengeti ..Cleins gate kutokea Loliondo. Kwa kifupi yuko serengeti national park kwa mpaka wa Loliondo/Wasso.
Wewe ulishapata adhabu gani? The lead tafadhali.
 
Mwinyi aliuza kipande cha ardhi kwa mwarabu enzi zake tena kwa mkataba mreefu. Ortelo ni hatari sana, walijenga uwanja wao wa ndege, ndege kubwa zinatua na kupaa na mzigo bila ukaguzi, kila aina ya mnyama [isipokuwa faru] alihamishwa mzima mzima akiwa bado mchanga. Zoo zao zimejitosheleza kwa wanyama pori aina karibu zote zinazopatikana Serengeti.
Mkuu hii ni nchi huru na mamlaka kamili. Hicho unachosema sio sahihi. Huwezi ukaruka na ndege bila ukaguzi kwenda nje ya nchi. Lazima upitie katika viwanja vya kimataifa km kia. Kwasababu ndege huwa lazima zipate clearance hata ya kupita tu katika anga ya nchi husika sembuse kutua na kuruka.
 
Ruler of Dubai huyo ni Sheikh Al Makhtoom
Kabla yake alisiani Brigadier General wa Emirates kumiliki ekari 1500 za mraba.
Hapo sijui kama waliongezewa miaka mingapi maana 1993 mkataba ulikuwa miaka 10
Kazi ipo, maana hela isikie tu,
Ukiambiwa nyumba tatu Dubai na mall moja, watoto wakasome nje hapo,
kweli useme Mimi mzalendo
 
Tunatamani sana hili litokee. Wasiwasi wetu ni kuwa labda Waziri ametoa tu kauli bila kupata ridhaa ya wakuu wake. Tusishangae kauli hiyo kubaki kuwa kauli tu.
 
Tatizo letu watanzania huwa tukishakuwa excited hata kufikiri hatutaki. Nnavyoelewa hii issue siyo rahisi hivyo. Kwasababu hiyo kampuni haifanyi biashara. Ipo hapo kwa ajili ya kurahisisha safari za mapumziko ya ukoo wa kifalme wa Emirates. Na kama ni kweli muda wa kuwaondoa umefika approach ya waziri ni mbaya mno kwa mahusiano ya kidiplomasia. Kumbukeni Tanzania sio kisiwa. Kama tunategemea kuheshimiwa kwa viongozi wetu wa kitaifa basi tunapaswa na sisi tuwaheshimu viongozi wa mataifa mengine.
 
Haya mambo ni mazur kama nyuma ya pazia yana nia njema, ila kama ni kick hakuna jipya
 
Mtu ambaye tangu anasoma hadi anaanza kazi hana accomplishment yeyote matamko kama haya naona kama yale aliyokuwa anampa Dr mwaka tu
 
Duh! pumzika Stan katabaro nazikumbuka makala zako ulianza na loliondo gate kisha ukaja na TBL gazeti la mfanyakazi lilikuwa juu wakati ule.
 
Ndiyo hao hao nimepongeza kauli Mkuu ambayo hakuna ambaye aliyewahi kuitoa tangu hao waarabu wanunue/wapewe eneo hilo. Sasa tusubiri utekelezaji wake. Je, atawaondoa kweli au atapigwa stop na maagizo toka mamlaka za juu?

Kweli mkuu lakini mafisadi si ndio wale wale au CCM imebadilika..
 
Sijaelewa kuhus ugawaji wa vitalu, wanataka vigawiwe kwa wazawa tu au ?

au ndio anawabeep ili wamletee bahasha yake ?
Yule msingida bahasha zilikuwa nyingi mpaka zingine mahausi boy wanakimbia nazo. Nasikia alikuwa na mtu wa m pesa anamsaidia tu kutuma m pesa kwa mamiss !
 
Back
Top Bottom