Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco
Mkuu huyu Mwarabu akiondolewa kweli nitafurahi. Amenyanyasa sana wazawa, ole wako upotee njia upitie karibu na kambi yao, adhabu utakayopata utajuta kuzaliwa Tz. Huyu yuko karibu kabisa na Geti la serengeti ..Cleins gate kutokea Loliondo. Kwa kifupi yuko serengeti national park kwa mpaka wa Loliondo/Wasso.
 
Stan Katabaro my best Tanzanian investigative journalist...!!
Nilikuwa sikosi gazeti la Mfanyakazi kufuatilia Loliondo gate...!!
Siku moja na nafikiri inakaribia ambapo mchango wake wa kufichua mikataba ya kifisadi utakumbukwa na kuenziwa.
CCM wanajikosha tu kwa wananchi,hiyo mikataba waliingia wenyewe na hao wawekezaji..
 
Kwa tamko hili lazima apongezwe sasa tuone kama utekelezaji wake utakamilika haraka iwezekanavyo.

Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.View attachment 618635
 
Acha tu turudi!! Kwanza hawa OBC waliteketeza kijiji kizima kwa madai kuwa eti hilo eneo la kijiji ambacho kimekuwepo hapo kwa makumi ya miaka kipo ndani ya eneo lao! Tena Kigwa angetupa ruhusa tukawaondoe wenyewe,wametuulia ndugu zetu wengi sana hawa hayawani! Mwarabu ni shetani kabisa!!!!
Captain unahasira!hadi unatetemeka! Kunywa maji bana.
 
Kwa tamko hili lazima apongezwe sasa tuone kama utekelezaji wake utakamilika haraka iwezekanavyo.
Mnapenda kupiga makofi na kupongeza bila ya kuangalia "impact" yake.....
 
Mkataba wa kifisadi waliofaidika ni mafisadi. Eneo la ardhi ya Tanzania litageuzwaje na kufanywa ni sehemu ya UAE!?

Mnapenda kupiga makofi na kupongeza bila ya kuangalia "impact" yake.....
 
Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco
Rip stanley Katabaro wananchi wa kweli Bado wanakukumbu moja kati ya maandiko yako ulisema kuna kizazi kitakuja kufukua kaburi lako kuangalia ulikuwa na kichwa cha namna gani na pia watafukua kaburi la rais wa wakati huo ili kujua kichwa chake kilikuwa kinafananaje.
naamini wapo watakao utendea haki uhai wako uliopotea.!
pumzika kwa amani.
 
Kwa hiyo serikali za CCM waliuza kila kitu.
Mwl Nyerere na Ujamaa wake watu wakampa za uso?
Hatuwezi kwenda mbele bila kwanza kuwadhibiti CCM
Kwa haya tumuogope Mungu.
CCM sio mfano mzuri ni madudu kwa kwenda mbele.
Loliondo CCM
IPTL CCM
Buzwagi CCM
Mwadui CCM
Geita Mines CCM
Kilimanjaro Hotel CCM
Air Tanzania CCM
EPA CCM
Kahama Gold Mines CCM
Song Gas CCM
Mtwara Gas Pipe Line CCM
Statiol CCM
Tecs CCM
Bagamoyo Port Complex CCM
Reli ya Kihindi CCM
TIPPER AGIP CCM
Merelani Tanzanite CCM
Escrow CCM
Dowans CCM
Gati no 6 CCM
Twiga KIA CCM
Faru John CCM
Mikopo hewa CCM
Wafanyakazi hewa CCM
Vyeti hewa CCM
Kuuzwa NBC CCM
Kuuzwa TTCL CCM
Kigamboni new city CCM
Flow meter za TPA CCM
 
Nilijua tuu kuwa baada ya mambo kuwa poa ,na mzee prof. kutumbuliwa sasa ni zamu ya maliasili na utalii. Kanaanza kamoto kidogo kama utani lakini baadaye utakuja kulipuka kila mtu atashangaa NAIONA TANZANIA MPYA YA NDOTO YANGU HIYOOO!! BIG UP PRESIDENT lazima rasilimali za taifa zisaidie taifa na sio wanyonyaji wachache
 
Back
Top Bottom