Waziri Kigwangalla awacharukia wanaomsema hajui Kiingereza

Waziri Kigwangalla awacharukia wanaomsema hajui Kiingereza

Kiranga unatufanya watu tujione hatujui chochote[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Kiingereza Chako kinaumiza kichwa
Hapa hadi nitafute dictionary lol[emoji1787]
Nafikiri huko mtaani au kazini wala hatumii maneno hayo, hicho ni cha kuumiza watu wa JF.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
kiranga!? dah.
kama usomi ndiyo kiingereza hicho nakiri na mimi mburula "blaza"
 
kiranga!? dah.
kama usomi ndiyo kiingereza hicho nakiri na mimi mburula "blaza"
Nimefurahisha genge tu walionibandika kilemba cha ukoka na kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa wafurahi.

Kiingereza ni moja kati ya lugha dhaifu sana, kwa maana imekosa mantiki kisarufi na kimatamshi. Nakubaliana na George Benard Shaw katika hili.

Ukifuatilia istilahi ya maneno yake utaona ni lugha chotara iliyozaliwa katikati ya lugha chotara nyingine za Uhindini-Ulaya.

Ila inaheshimika sana kwa sababu ya historia yake ya kuwahi kuenea dunia nzima.
 
Naunga mkono hoja,kutojua lugha fulani hakuondoi usomi wa mtu,,ila kwa nchi yetu ukijua kiingereza tu basi utatazamwa kwa jicho tofauti

Humu ndani kuna "nyani" bingwa wa kiingereza hatari,ukibahatika kujua kiingereza kama cha yule kwa nchi yetu wewe ni msomi hata kama ni la saba
Kiingereza cha @nyaningabu sio cha dunia hii
 
Mimi naomba kujuzwa, mlima gani ni tallest hapa Africa? Maana lazima utakuwepo
 
Kigwangalla awacharua wanaomsema hajui kingereza asema sio sifa kuijua

Waziri wa Maliasilia na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kuna watu huwa wanajaribu kumkosoa lugha yake ya kingereza.

“Huwa nina washangaa sana maana kwanza siyo sifa kujua lugha hiyo mimi naitumia kama njia ya kuwasiliana tu,” aliandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa “Ningekuwa sijui kiswahili ama kikimbu na mtu akanicheka angekuwa na mantiki.

View attachment 1471687

Waziri anaihifadhi lugha ya Kiingereza kuwasiliana na watalii na katika masuala ya kikazi tu. Hapendi ujinga.
Huyu daktari wa mifugo aache ujinga
 
Lakini pia hapa kuna jambo alijakaa sawa.
Iweje mtu kwa kipindi cha takriban miaka ishirini anajifunza masomo yake kwa kutumia lugha hiyo hiyo na asiweze kuimudu.
Elimu ya Kenya haipishani sana na yetu ilikuwaje mkenya alikuwa anakukimbiza kwa kingereza.
Aidha watanzania wakipelekwa Urusi China Cuba inawachukua miaka miwili kujifunza lugha za huko na baadae wanahitimu shahada zao wakiwa wanaongea hizo lugha kwa ufasaha.
Tunajitetea sijui wachina warusi nk hawaongei kingereza,tunashindwa kutatua tatizo hili la muda mrefu ambalo majirani zetu hawana.

Tatizo sio kusoma kwa kiingereza kutamfanya mtu kuwa mmahiri katika kuizungumza lugha au kuiandika kwa ufasaha. Tatizo wakishatoka huko wanakofundishwa lugha wakirudi huku mtaani au wakitoka tu darasani hakuna lugha watakayoongea zaidi ya hicho kiswahili.

Hao wanaokwenda Uchina, Urusi, Cuba nk wanafanikiwa kuzimudi na kuwa wamahiri wa lugha hizo ni kwasababu ya mazingira kunakuwa hakuna lugha mbadala zaidi ya hiyo hata akitoka nje ya mazingira ya kusomea bado atakutana na lugha hiyo hiyo.

Hapa issue sio kusoma miaka mingi kwa lugha fulani, issue ni ku-practise hiyo lugha kwa muda mrefu hata huko vyuoni walimu wanafundisha kwa lugha zote mbili.

Pia ukiangalia waalimu wetu huko Alevel na Olevel hawaweki mkazo katika kusahihisha kwa kufuata misingi ya uandishi, wanaangalia sana sana key point/word wakati wa kusahihisha mitihani.

Kwa kiasi fulani kama wa Tanzania hasa sisi wa shule zinazomilikiwa na Umma tuna safari ndefu sana katika kujifunza na kuimasta lugha ya kiingereza.

Pia wakufunzi wetu wa somo la kiingereza (waalimu) wanajikita kutufundisha jinsi gani tunaweza tukajibu mitihani na kufaulu na si kutufundisha kuelewa lugha.
 
Aaah uwezi kuelewa na kukubali ukweli lakini..Hivi kujua hiyo Lugha ambayo umefundishwa pia nakufindishiwa ni kosa kama kutoijua?
Sio kwamba sikuijua tatizo ni kusound natural kaka! Kama ulikuwa unajua kiingereza chetu cha kibongo then ghafla bin vuu hapahapa nchini ukapata dili ila mabosi wako wakawa Wamarekani ndo utanielewa vizuri. Boss anaongea 5 words per second halafu hatumii misamiati ya chekechea! Anatumia high level vocabulary za kiofisi ofisi zile.Uzuri written English nilikuwa vizuri,nilifuzu mtihani wao.Tatizo spoken sasa hehe! Ila nashukuru nilivyotoka pale nikarudi home hata wewe ningekwambia Mimi ni American kwa haraka haraka ungekubali,kama usingechunguza sana.
Nimeona pia umegusia suala la kazi kwamba nilikuwa nasukumiwa kisa underground ila nikwambie tu mtu ukipendwa zaidi kazini utafahamu tu.Kuna zile kazi unafanya nje ya working hours so inabidi ulipwe! Hizo nilizikamata nyingi kuliko yule mwenzangu.
 
Kigwangalla awacharua wanaomsema hajui kingereza asema sio sifa kuijua

Waziri wa Maliasilia na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kuna watu huwa wanajaribu kumkosoa lugha yake ya kingereza.

“Huwa nina washangaa sana maana kwanza siyo sifa kujua lugha hiyo mimi naitumia kama njia ya kuwasiliana tu,” aliandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa “Ningekuwa sijui kiswahili ama kikimbu na mtu akanicheka angekuwa na mantiki.

View attachment 1471687

Waziri anaihifadhi lugha ya Kiingereza kuwasiliana na watalii na katika masuala ya kikazi tu. Hapendi ujinga.
Mbumbumbu wa nzega said bagaile
 
Hii nchi bado tuna safari ndefu sana. Waziri anashupaa kutojua kiingereza. Huyu jamaa ni mweupe sana kichwani.
 
Back
Top Bottom