Waziri Kikwete kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Songwe

Waziri Kikwete kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Songwe

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
✅ Atakagua na Kuzindua Miradi ya Maendeleo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu -Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Februari 23, 2025 amewasili mkoani Songwe kwa lengo la ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya wananchi .

Mhe. Waziri Kikwete anatarajiwa kukagua na kuweka Mawe ya msingi katika miradi hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 700 katika Halmashauri zote za mkoa huo.

Mara baada ya kuwasili katika mkoa huo, Waziri Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Daniel Chongolo ambaye alimpa hali ya maendeleo ya Mkoa huo na maandalizi ambayo yameshafikiwa kwa ajili ya ziara hiyo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri Kikwete ameambatana na watendaji mbalimbali ambapo amemhakikishia Mkuu wa mkoa huo kuwa timu yake iko tayari kwa ajili ya kazi iliyowaleta.

Vile vile Mhe. Kikwete anatarajiwa pia kukagua Maendeleo ya Kituo cha Vijana cha Sasanda wilayani Songwe ambapo atakagua mradi wa Shamba la vijana lililopo kituo hicho.

FB_IMG_1740339785780.jpg
FB_IMG_1740339811312.jpg
FB_IMG_1740339772072.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1740371168360.jpg
    FB_IMG_1740371168360.jpg
    76 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740339788679.jpg
    FB_IMG_1740339788679.jpg
    39.8 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1740339794578.jpg
    FB_IMG_1740339794578.jpg
    77.2 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1740339803857.jpg
    FB_IMG_1740339803857.jpg
    59.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom