Waziri Kombo amwakilisha Rais Samia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola Apia, Samoa

Waziri Kombo amwakilisha Rais Samia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola Apia, Samoa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 49 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea Apia, Samoa kuanzia Oktoba 21 hadi 26, 2024.

Kati ya mambo muhimu katika mkutano huo ni pamoja na kumchagua Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Masuala mengine nyeti yatakayojadiliwa ni pamoja na uwekezaji, kutafuta suluhu ya pamoja kwa ajili ya maendeleo endelevu, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa kijinsia, uchumi, demokrasia, na amani.

Mkutano huu utaibua changamoto na matarajio ya wanachama, huku Tanzania kama moja ya wanachama 56 wa Jumuiya ya Madola ikiwa miongoni mwa wale watakaonufaika katika sekta za uwekezaji, mabadiliko ya tabianchi, uchumi stahimilivu, na kubadilishana ujuzi kati ya mafanikio mengine mengi.

Mhe. Kombo amewasili Samoa na kupokelewa na Waziri wa Fedha wa Samoa Mhe. Lautimuia Vaʻai. Akiwa safarini Mhe. Kombo amefanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda, Mhe. Gaston Browne pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Seychelles, Mhe. Sylvestre Radegonde.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni Ustahimilivu katika kufikia malengo ya pamoja ya kimaendeleo ‘One Resilient Common Future: Transforming Our Common Wealth
IMG-20241022-WA0038.jpg
IMG-20241022-WA0045.jpg
IMG-20241022-WA0041.jpg
 
Attachments

  • IMG-20241022-WA0042.jpg
    IMG-20241022-WA0042.jpg
    112.7 KB · Views: 7
  • IMG-20241022-WA0046.jpg
    IMG-20241022-WA0046.jpg
    155.8 KB · Views: 6
  • IMG-20241022-WA0044.jpg
    IMG-20241022-WA0044.jpg
    136.8 KB · Views: 6
  • IMG-20241022-WA0040.jpg
    IMG-20241022-WA0040.jpg
    108.9 KB · Views: 4
  • IMG-20241022-WA0048.jpg
    IMG-20241022-WA0048.jpg
    145.6 KB · Views: 4
  • IMG-20241022-WA0047.jpg
    IMG-20241022-WA0047.jpg
    140.9 KB · Views: 5
  • IMG-20241022-WA0043.jpg
    IMG-20241022-WA0043.jpg
    137.5 KB · Views: 6
  • IMG-20241022-WA0039.jpg
    IMG-20241022-WA0039.jpg
    87.6 KB · Views: 5
Tanzania kususa kikao cha CHOGM 2024 kilicho na nchi wanachama 56 kutoka Africa, the Caribbean na Americas, Europa, Asia na the Pacific
1729873687736.jpeg

Je nchi yetu ile sera ya kufunguka kwa njia ya kidiplomasia kushawishi wadau wa maendeleo wa sekta na mabara tofauti kuifahamu Tanzania sasa imefuka ukomo?

Nini sababu za Tanzania kujifungia kama Zimbabwe katika jukwaa hili muhimu la kimataifa kwa mwanadiplomasia namba moja aliye rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kutuma waziri wa mambo ya nje?

Kuna madokezo ya karipio kidiplomasia kichinichini kushindikiza Tanzania kutoka jumuiya za kimataifa ikiwemo hii ya Jumuiya ya Madola kuhusu hali ya kisiasa, kidemokrasia, haki za binadamu, haki ya kuishi na kutembea kokote, kutekwa, kupotezwa na pia watu wasiojukikana kuchukua hatamu za usalama na mfumo mzima wa haki jinai, uchaguzi na maisha kwa ujumla ya watanzania

Kwa maana nyingine tujiulize utawala wa kidikteta na kiimla unaopigiwa na wapenda haki, watetezi wa haki za binadamu pia demokrasia bila kusahau uhuru wa habari mayowe yao yamesikika nje ya mipaka hata nje ya bara hili la Afrika, kiasi utawala wa chama dola kongwe CCM kuanza kuongopa mikutano ya aina hii ?

Hizi ni dalili kama moshi au mawingu kutuonesha kuwa kuna kitu hakipo sawasawa siyo ndani ya nchi bali hata katika mahusiano nje ya nchi kupitia vyombo hivi vya kimataifa na baina ya mahusiano ya nchi na nchi na Tanzania.

Yetu macho ni muda utatufunulia jibu sahihi nini kinaendelea serikali ya Tanzania kuingia hofu kuu.
 
Huyo ataweza kuchangia hoja kweli au ndo kwenda Kumumunya TENDE na HALUA alizotoka nazo Kibanda Maiti na KIZIMKAZI?
 
Mama chapa kazi, wapika majungu waachie waendelee na majungu, hiyo ndio fani yao, madebe matupu hupiga kelele tu.
Wewe simamia yenye kipaumbele kwa nchi mengineyo waachiye wasaidizi wako. Huo ndio uongozi.
Malizia miaka yako ya mpito uanze miaka yako 10 mpaka 2035
 
Tanzania kususa kikao cha CHOGM 2024 kilicho na nchi wanachama 56 kutoka Africa, the Caribbean na Americas, Europa, Asia na the Pacific
View attachment 3135092

Je nchi yetu ile sera ya kufunguka kwa njia ya kidiplomasia kushawishi wadau wa maendeleo wa sekta na mabara tofauti kuifahamu Tanzania sasa imefuka ukomo?

Nini sababu za Tanzania kujifungia kama Zimbabwe katika jukwaa hili muhimu la kimataifa kwa mwanadiplomasia namba moja aliye rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kutuma waziri wa mambo ya nje?

Kuna madokezo ya karipio kidiplomasia kichinichini kushindikiza Tanzania kutoka jumuiya za kimataifa ikiwemo hii ya Jumuiya ya Madola kuhusu hali ya kisiasa, kidemokrasia, haki za binadamu, haki ya kuishi na kutembea kokote, kutekwa, kupotezwa na pia watu wasiojukikana kuchukua hatamu za usalama na mfumo mzima wa haki jinai, uchaguzi na maisha kwa ujumla ya watanzania

Kwa maana nyingine tujiulize utawala wa kidikteta na kiimla unaopigiwa na wapenda haki, watetezi wa haki za binadamu pia demokrasia bila kusahau uhuru wa habari mayowe yao yamesikika nje ya mipaka hata nje ya bara hili la Afrika, kiasi utawala wa chama dola kongwe CCM kuanza kuongopa mikutano ya aina hii ?

Hizi ni dalili kama moshi au mawingu kutuonesha kuwa kuna kitu hakipo sawasawa siyo ndani ya nchi bali hata katika mahusiano nje ya nchi kupitia vyombo hivi vya kimataifa na baina ya mahusiano ya nchi na nchi na Tanzania.

Yetu macho ni muda utatufunulia jibu sahihi nini kinaendelea serikali ya Tanzania kuingia hofu kuu.
Hawa wazenj wanakula nchi siku ikirejea kwa wenyewe wabara wasianze kulalamika maana sasa tunaona wakitumbua kiroho mbaya chance wamepata kwenye serikali ya muungano.
 
Napongeza hili.Kiongozi wa nchi Kwenda Kumpigia magoti mfalme wa uingereza ni ujinga na ushamba katika dunia ya sasa.Hao ndiio haohao wanaosapoti maovu mengine huko duniani huku wakijifanya wema.Si watu hao.Asante sana Mama.Tena ungemtuma hata Spika wetu akuwakilishe kwenye hicho kikao,maana yeye ndiye hapendi ujinga kabisaaaaaa.
 
"Roho naona yachinjwa, sumu ya Mwanza inakorokota".......alisikika mama mmoja alisema hivo
 
Tanzania yaigeukia mshirika mkuu wa Russia, nchi ya Belarus
1729941143436.jpeg

kuu Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya kwa mazungumzo ya pande mbili kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika kikao cha Alhamisi kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam, Majaliwa aeleza dhamira ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili na Belarus kwa manufaa ya pande zote.

"Tanzania itaendelea kushirikiana na Belarus katika sekta ya madini, afya, utalii, kilimo na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili," ilisoma taarifa kutoka ukurasa rasmi wa Instagram wa Waziri Mkuu.

Mkutano huo unakuja siku mbili baada ya Balozi Vziatkin kufanya kikao cha maelewano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Cosato Chumi, katika mji mkuu wa Dodoma.

Wawili hao walipendekeza kusaini Mkataba wa Maelewano (MoUs) na kubadilishana ziara ili kuimarisha kwa kiasi kikubwa uhusiano baina ya nchi hizo huku wakizingatia mienendo ya kimataifa.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus ulianza mwaka 1996 na kufikia kilele mwaka 2016 ambapo Oktoba 31, nchi hizo mbili zilifanya Kongamano la Biashara la Belarusi na Tanzania mjini Minsk, ambapo Mkataba wa Ushirikiano ulitiwa saini kati ya Kituo cha Taifa cha Masoko cha Belarus. Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).

Mnamo mwaka wa 2017, Belarus iliwasilisha rasimu mbalimbali za Makubaliano kwa serikali ya Tanzania ili kuzingatiwa katika maeneo yanayohusiana na uhusiano wa nje, elimu na biashara. Walakini, hakuna habari inayoonyesha kuwa serikali hizo mbili zilikamilisha Makubaliano haya kuanzia leo.

Mnamo Januari mwaka huu, ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Belarusi na wawakilishi kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Belarusi waliitembelea Tanzania. Walikutana na wenzao kutoka Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA). Ujumbe huo ulionyesha nia ya kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania.

Kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili bado ni cha kawaida. Ilifikia kilele mwaka 2017 wakati Tanzania ilipouza nje bidhaa zenye thamani ya dola milioni 46.6 na kuagiza takriban dola za Marekani milioni 1.3 kutoka Belarus. Hata hivyo, uhusiano wa kibiashara unaonekana kupungua, ambapo Tanzania iliuza nje dola za Marekani milioni 4.8 na kuagiza dola milioni 4 mwaka 2021
 
TOKA MAKTABA:

Je nchi kufunguka sasa mahusiano ya Tanzania yageukia zaidi Mashariki ya dunia yetu hususan nchi za ulaya ya Mashariki, Uturuki na Mashariki ya Kati, India na China

Kwa kiswahili:

BUNGE LA DUMA

Vyacheslav Volodin alihudhuria mkutano wa Vladimir Putin na Rais wa Muungano wa Mabunge Tulia Ackson​

Mkutano ulifanyika kando ya Kongamano la 10 la Wabunge wa BRICS huko St
Julai 11, 2024, 17:54
Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin, Spika wa Baraza la Shirikisho Valentina Matvienko, Mwenyekiti wa Jimbo Duma Vyacheslav Volodin na Rais wa Muungano wa Mabunge, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson (picha kwa hisani ya vyombo vya habari huduma ya Rais wa Shirikisho la Urusi)

Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin, Spika wa Baraza la Shirikisho Valentina Matvienko, Mwenyekiti wa Bunge la Duma Vyacheslav Volodin na Rais wa Muungano wa Mabunge, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson (picha kwa hisani ya vyombo vya habari huduma ya Rais wa Shirikisho la Urusi)

Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin amekutana na Rais wa Muungano wa Mabunge, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson. Mwenyekiti wa Bunge la Duma Vyacheslav Volodin na Spika wa Baraza la Shirikisho Valentina Matvienko walihudhuria mkutano huo.
"Kiwango cha bunge cha ushirikiano wa BRICS kinafurahia maslahi makubwa na kukua kwa imani kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Hili linaeleweka, kwa sababu kanuni za kazi za BRICS – usawa wa kweli na kuzingatia maslahi ya kila mmoja wao – haziwezi ila kuvutia washiriki katika shughuli za kimataifa,” alisisitiza mkuu huyo wa taifa.
Vladimir Putin alikumbuka kwamba IPU "ni shirika linaloheshimika ambalo lilianzishwa nyuma mwishoni mwa karne ya 19. Nchi nyingi ni wanachama wake.

Tunakaribisha ukweli kwamba sasa inaongozwa na mwakilishi wa uchumi unaoendelea barani Afrika.

“Kwa upande wetu, tunatumai kwamba mtaunga mkono kazi ya mwelekeo wa wabunge wa BRICS, ambayo ni muhimu. Sio tu kwamba inaweka msingi wa kazi ya pamoja ili kuimarisha mfumo wa udhibiti kati ya mataifa yanayoshiriki, lakini pia inajenga mazingira mazuri ya kibinadamu kwa ajili ya kufikia malengo ya pamoja ya maendeleo. Kwa mara nyingine tena, ningependa kuwashukuru kwa ushiriki wenu katika mkutano wa wabunge wa nchi za BRICS,” alisema Vladimir Putin.

Mkutano wa Vladimir Putin na Tulia Ackson ulifanyika kando ya Mkutano wa 10 wa Wabunge wa BRICS unaoendelea mjini St.
1kutoka 4
Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin na Mwenyekiti wa Jimbo la Duma Vyacheslav Volodin (mikopo ya picha: huduma ya vyombo vya habari ya Rais wa Shirikisho la Urusi)

Rais wa Muungano wa Mabunge, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson (picha ya hisani: huduma ya vyombo vya habari ya Rais wa Shirikisho la Urusi)

Back
Top Bottom