Waziri Kombo amwakilisha Rais Samia ufunguzi rasmi wa Mkutano wa CHOGM

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri Kombo amwakilisha Rais Samia ufunguzi rasmi wa Mkutano wa CHOGM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliofanyika jijini Apia, Samoa leo Oktoba 25, 2024.

Tanzania kwenye Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar, Mhe. Shaaban Ali Othman pamoja na vijana wa Kitanzania walioshiriki Jukwaa la Vijana la CHOGM, imebeba agenda ya nishati safi ya kupikia kwa kuzihamasisha nchi wanachama wa CHOGM kuwa mstari wa mbele katika kuandaa mikakati madhubuti ya kuzalisha nishati hiyo kwa maendeleo endelevu ya Nchi hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Tanzania inalenga kushirikiana na wadau mbalimbali wa Jumuiya za kikanda na kimataifa ikiwemo CHOGM, sekta binafsi na taasisi za kifedha ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.

Akifungua rasmi Mkutano huo, Mfalme wa Uingereza, Charles III amezitaka Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo kuongeza jitihada za pamoja kuleta maendeleo stahimilivu ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni changamoto ya dharura inayotishia kuleta majanga ya kimazingira duniani na yenye kuhitaji jitihada za haraka katika kuitatua kwani kila nchi mwanachama ana sauti katika kutatua changamoto zinazojitokeza za kijumuiya.

Mfalme Charles ameongeza kuwa katika mipango yote ya Jumuiya ya Madola (JYM) vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele wakiwezeshwa kitaaluma na kiujuzi hususan waishio katika visiwa vidogo vidogo, akisema yeye mwenyewe anaendelea kuwa mstari wa mbele katika hilo.

Agenda kuu ya mkutano wa 27 wa CHOGM, imejikita kwenye ustahimilivu katika kufikia malengo ya pamoja ambapo nchi wanachama zimeshauriwa kuendelea kuwa wastahimilivu katika uchumi, mazingira, demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu na ustawi wa watu katika jamii.

Aidha, tarehe 26 Oktoba 2024, Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Madola atachaguliwa na hadi sasa nchi zinazogombea nafasi hiyo ni Lesotho, Gambia na Ghana.
 

Attachments

  • 464502890_18087863683502573_8480210474737253374_n.jpg
    139.9 KB · Views: 3
  • 464501509_18087863692502573_1902369556154307326_n.jpg
    100.4 KB · Views: 3
  • 464385200_18087863701502573_1809093655059847818_n.jpg
    172.3 KB · Views: 3
  • 464534801_18087863710502573_3395834835029216883_n.jpg
    188.4 KB · Views: 4
  • 464551442_18087863719502573_4276356753869078736_n.jpg
    136 KB · Views: 6
  • 464372794_18087863728502573_6951214333254224675_n.jpg
    117.7 KB · Views: 4
  • 464486102_18087863740502573_703512343760475223_n.jpg
    86.5 KB · Views: 4
  • 464676330_18087863749502573_959487448236434187_n.jpg
    110.9 KB · Views: 5
  • 464395452_18087863758502573_2229497553833916753_n.jpg
    142.8 KB · Views: 4
  • 464677812_18087863767502573_1369634081026786134_n.jpg
    170.2 KB · Views: 5
Kombo doesn't ring!
Mbona hatumfahamu, what is his accomplishments in Foreign Affairs?
 
Urithi alioachiwa na marehemu baba yake kama alivyoachiwa Nape na watoto wengine waliorithishwa vyeo CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…