Waziri Kombo aongoza Mkutano wa dharura wa Kamati ya Mawaziri wa SADC

Waziri Kombo aongoza Mkutano wa dharura wa Kamati ya Mawaziri wa SADC

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) *ulio*fanyika kwa njia ya mtandao kujadili hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkutano huo umejadili na kupokea ajenda zitakazojadiliwa na kuamuliwa katika Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Extra-Ordinary Organ Troika Summit - EO-OTS), Nchi Zinazochangia Askari katika Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini DRC (SAMIRC) pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Machi 6, 2025 kwa njia ya mtandao.

IMG-20250305-WA0316.jpg
 
Back
Top Bottom