Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
WAZIRI KOMBO ASHIRIKI KONGAMANO LA KISWAHILI NA MAADHIMISHO YA PILI YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI PARIS
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameshiriki Kongamano la Kiswahili pamoja na Maadhimisho ya Pili ya Kimataifa ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), jijini Paris, Ufaransa.
Kongamano hilo lililowakutanisha viongozi wa serikali, wanadiplomasia, wasomi, wataalamu wa lugha na wadau wa Kiswahili kutoka mataifa mbalimbali duniani, lililenga kutathmini nafasi ya Kiswahili katika kuimarisha mawasiliano ya kimataifa, kukuza utamaduni, elimu na ushirikiano miongoni mwa jamii duniani.
Katika kongamano hilo, Tanzania imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika ufundishaji, utafiti, uchapishaji wa machapisho ya Kiswahili pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuhakikisha lugha hiyo inaendelea kukua na kupata nafasi kubwa zaidi duniani.
Kiswahili miongoni mwa lugha zinazotambulika kimataifa na kutumika katika majukwaa mbalimbali ya kikanda na kimataifa, kimeendelea kuwa alama ya utambulisho wa Afrika, urithi wa kiutamaduni na chombo cha kukuza amani, mshikamano na uelewano kati ya watu.
Maadhimisho ya Pili ya Kimataifa ya Siku ya Kiswahili Duniani jijini Paris yameongeza msukumo katika juhudi za kimataifa za kukuza matumizi ya Kiswahili, huku Tanzania ikiendelea kushirikiana na UNESCO pamoja na wadau wengine duniani kuhakikisha lugha hiyo inazidi kuenea na kutumika katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Attachments
-
IMG-20260710-WA0001.jpg161.8 KB · Views: 16 -
IMG-20260707-WA0013.jpg44.5 KB · Views: 15 -
IMG-20260708-WA0064(1).jpg245.2 KB · Views: 15 -
IMG-20260708-WA0057(1).jpg473.1 KB · Views: 16 -
IMG-20260707-WA0012.jpg56.4 KB · Views: 16 -
IMG-20260710-WA0003.jpg185.4 KB · Views: 16 -
IMG-20260710-WA0000.jpg227.9 KB · Views: 18 -
IMG-20260709-WA0017.jpg116.1 KB · Views: 17 -
IMG-20260709-WA0016.jpg118.8 KB · Views: 16 -
IMG-20260709-WA0015.jpg179.7 KB · Views: 14 -
IMG-20260709-WA0019.jpg137.5 KB · Views: 16 -
IMG-20260709-WA0018.jpg164.1 KB · Views: 19 -
IMG-20260709-WA0014.jpg158.9 KB · Views: 16