Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, Generali Lương Cường ameeleza kuwa, madhimisho hayo yanaandaliwa ikiwa ni ishara ya kutambua na kuheshimu mchango wa kipekee wa mashujaa wa Taifa hilo uliojenga misingi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taifa hilo kwa kipindi cha nusu karne katika kujenga umoja wa kitaifa, maendeleo ya kiuchumi na mahusiano ya kimataifa.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wa Nchi na Serikali, na Wanadiplomasia kutoka mbalimbali duniani, ambapo kutoka Afrika ni mataifa matatu pekee yaliyoalikwa kwenye maadhimisho hayo ambayo ni Tanzania, Angola na Msumbiji.
Mbali na kushiriki katika sherehe za uapisho huo, Waziri Kombo alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Viet Nam Mhe. Pham Minh Chinh jijini Ho Chi Minh, muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya miaka 50 ya Uhuru na Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam.
Mazungumzo hayo yalijikita kujadili kuhusu masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza zaidi ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo; biashara na uwekezaji, utalii, uchumi wa bluu, viwanda, kilimo, elimu na mafunzo kwa lengo la kukuza ustawi kwa pande zote mbili za Mataifa hayo rafiki.
Waziri Kombo alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Viet Nam, ambapo amehitimisha leo Aprili 30, 2025.