Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Ni vyema hawa jamaa wakaulizwa aisee yaani NIDA ni shida jamani. Ndiyo maana Boss wa sasa wa TISS ndugu Modestus Kipilimba alienda kupasafisha ila kukawa kama kumepooza hivi. Kama walipata muda hawakujipanga basi ni kweli watapata tabu sana. Nyongeza ingine ya habari hiyo hii hapa.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kuripoti ofisini kwake Agosti 3, 2018 ili kumpa maelezo ya ufisadi wa Sh28.5bilioni.

Amesema Maimu anapaswa kuambatana na Jack Ghothamu ili kueleza kuhusu ufisadi wa kiasi hicho cha fedha uliotokea katika zabuni za ukandarasi wa mfumo wa utambuzi wa watu.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 25, 2018 katika mkutano wake wa waandishi wa habari mjini Dodoma.

Pia, amewataka wamiliki wa kampuni saba zilizopewa zabuni ya ukandarasi wa mfumo wa utambuzi wa watu na kujihusisha na ufisadi nazo kuripoti ofisini kwake siku hiyo.

Amezitaja kampuni hizo na kiasi cha fedha katika mabano kuwa ni Gotham international Ltd (2.8bilioni), Iris Corporation Berhard (22.9bilioni), Gwiholoto impex ltd (Sh 946.4milioni).

Nyingine ni Skyes Travel Agent (5.9milioni), Dk Shija Paulo Rimoy (Sh 27milioni) ,Aste Insurance (sh 1.2bilioni) na BMTL (Sh569.1milioni).

Ameyataka makampuni hayo kufika ofisini kwake na kiasi hicho cha fedha ili zirejeshwe katika mfuko wa Serikali.
 
Mkuu mimi kitambulisho cha uraia mbona nimechukua baada ya miezi 3? Tena nilichelewa mwenyewe tu kwenda ila waliniambia kilikua tayari baada ya wiki 2
 
Kuna vitu naonaga kabisa ni vizuri ila najikuta tu nakua mzito kupongeza... Sababu ccm huwa siwaamini
 
Hivi hayo maji hapo mezani yanakuwa yamenunuliwa na wizaraaaa au hao wanaosemekana wadaiwa?
 
Naona keshachoka kuvaa lile suti lenye mibendera ya CCM uzalendo haupimwi kwa mavazi we mzee.
Utapata tabu sana
 
Anaitisha mtambo upelekwe ofisini kwake Dodoma kivipi? Anaweza kuwa na point ila utekelezaji wake ndo tatizo. Suprisingly Jiwe anafarijika sana anaposikia na kuona hizi drama...

wewe unasikitika na hizi hatua?????
 
Kangi lugola ,ataweza huu mfupa ?

Huyu Jack Gotham , mfadhili na mmoja wa wana mikakati wa Bernard membe , aliyepewa tenda hiyo ili wapige pesa za kampeni 2015, huku huyu Dickson Maimu akiwekwa pale kukamilisha dili, bila kujua mlokole wa kitengo alikuwa pale ,akiwasoma na kuwa study vilivyo ,alivyomaliza kazi yake kwa ustadi , akapewa U DG , hakika kikwete na udhaifu wake kuna mambo alistahili pongezi kwa kiasi maana alikuwa na uzalendo nusu ubandidu nusu


Je kangi ataweza huu mfupa wenye chain ndefu ?

Yetu Macho na masikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…