Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

Waziri Lugola: Aliyekuwa Mkurugenzi NIDA, Dickson Maimu na Jack Gotham wasipoitikia wito ‘watapata tabu sana’

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema, kuna kampuni zimelipwa fedha kifisadi kwenye mradi wa vitambulisho vya taifa.

Amezitaja kampuni hizo ni Gotham International Limited inayodaiwa Sh bilioni 2.8, Iris Corporation Berhard Sh bilioni 22.9, Gwiholoto Impex Limited Sh milioni 946.4, Sykes Travel Agent Sh milioni 5.9, Dk Shija Paul Rimoy Sh milioni 27, Aste Insurance inayodaiwa Sh bilioni 1.2 na BMTL Sh milioni 569.1.

Amesema kampuni hizo zinadaiwa Sh bilioni 28.5.

Ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na Jacky Gotham waende Dodoma Agosti 3 kujieleza.

“Wafike ili watoe maelezo yanayojitosheleza hasa kwenye ule mtambo wa shilingi bilioni 32 inaonekana fedha imetolewa lakini mtambo haujaletwa,” amesema na kuagiza watu hao waandikiwe barua na hata kupigiwa simu na wasifanye jaribio lolote la kutofika siku hiyo.

Amesema Kampuni ya Iris ilikuwa mkandarasi na walihusika katika kuleta mtambo, kampuni ya Gotham ilikuwa mshauri mwelekezi na ililipwa fedha za dharura kwenye viwango ambavyo si sahihi.
ATUELEZE KA NINI ALIOMBA RUSHWA YA MILIONI 30!


TUHUMA ZA RUSHWA BUNGENI: Wabunge Kangi Lugola, Victor Mwambalaswa na Sadiq Murad waburuzwa mahakamani
 
Kusema Lugola amebaini ilihali huu Ufisadi kwenye National IDs unafahamika tangu Kabla ya Magufuli? Magufuli Mwanzoni kabisa mwa utawala wake akalisemea hili! Hii nchi kituko, iko siku tutasikia Waziri amebaini Ufisadi Passport za ki electronics ilihali kina Heche wameshalisema na kufikia kutishiwa kuuawa!
 
Yaonekana kila mkataba wa manunuzi ya serikali ya Tanzania ilikuwa fursa ya kufuja mali ya umma.
Lipo tatizo kubwa sana nchini linataka kuwekwa wazi,kuwabaini wale wote waliotuibia tokea uhuru hadi leo bila kujali hao walikuwa na nyadhifa zipi.
Siungi mkono hoja eti ya kuwalinda wakubwa walioishastaafu.Tunahitaji kufanya mjadala wa kitaifa haraka sana.
 
Good move,hata Zii akitulia anatengeneza asali!....wakati mwingine hawa wapiga"Diri" ni bora kuwapelekea moto usioeleweka!
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kuripoti ofisini kwake Agosti 3, 2018 ili kumpa maelezo ya ufisadi wa Sh28.5bilioni.
Hivi hii tabia ya kuita watu kupitia vyombo vya habari ina malengo gani hasa ............!!?

Ina maana wakitoa maelezo ya hizo Billion 28 atakuja kutupa marejesho ama vipi ...........!!?
 
Kuna Uzi humu wa 2015 uliandikwa na kusema hivi "jack Gotham ni nani kwenye siasa za tanzani?

Ova
 
Lugola naye kazidi kwa matamko yake sasa. Kila siku anakuja na mpya. Ya awali ameshayatekeleza?

Hana tofauti na Aggrey Mwanri RC wa Tabora ambaye akifika site hufoka mno lakini utekelezaji zero.

Lugola mpaka sasa amerukia rukia mambo mengi lakini sioni anachofanikiwa zaidi ya kutoa masaa kadhaa lakini baada ya hapo hurukia mengine.
Mkuu Huwezi kumlinganisha Mwanri na Lugola kiutendaji.
Huyu kashika wadhifa juzi, maagizo mengi aliyoyatoa kwa utekelezaji, tarehe zake hazija expire.
Embu tumpatie muda ndiyo tumtathimini.
Lakini uchambuzi wako kwa RC wa Tabora, ninakupa bigup,ni mzigo usiobebeka.
 
Hivi hii tabia ya kuita watu kupitia vyombo vya habari ina malengo gani hasa ............!!?

Ina maana wakitoa maelezo ya hizo Billion 28 atakuja kutupa marejesho ama vipi ...........!!?
Hivi hii tabia ya kuita watu kupitia vyombo vya habari ina malengo gani hasa ............!!?

Ina maana wakitoa maelezo ya hizo Billion 28 atakuja kutupa marejesho ama vipi ...........!!?
Mkuu hawaitwi kwa media, wanaitwa kwa barua za kiofisi.
Serikali haifanyi kazi kwa kutumia vyombo vya habari.
Ukiona hivyo, elewa tayari walikwisha kukabidhiwa barua za wito na kusaini.
 
Mkuu hawaitwi kwa media, wanaitwa kwa barua za kiofisi.
Serikali haifanyi kazi kwa kutumia vyombo vya habari.
Ukiona hivyo, elewa tayari walikwisha kukabidhiwa barua za wito na kusaini.
Swali hapa ..... ni kwa nini atutangazie kwenye vyombo vya habari kuwa fulani na fulani ni lazima wafike ofisini kwake siku fulani. La sivyo watapata tabu sana.

Wewe huoni kuwa anawadhalilisha hao watu ....!!
 
Back
Top Bottom