Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Hii ni ishara kuwa tuna watawala kwenye nchi hii badala ya viongozi......

Maneno kama hayo hutolewa na watawala na sio Kwani mtawala yupo kwa ajili kuimarisha utawala wake na kiongozi yupo kwa ajili ya wananchi........

Kwa kauli hiyo maana yake ni kwamba wizara ya mambo ya ndani haipo kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao bali usalama wa watawala na mali zao.......

Kwa hiyo suala la usalama ni la mwananchi mwenyewe na sio waziri husika
 
Hivi kabla ya kuwateua hawa watu ni vigezo gani vinatumika?? Kwa inavyoonesha jeshi la polisi linataarifa ya kupotea kwa Gwanda lakini si jukumu lao kumtafuta. Hii Ni Hatari Sasa.

Kwa hali mtu anaweza kumpongeza Peter Zacharia kwa alivyo wapiga risasi watu wa usalama wa Taifa
 
"Waziri kaingia kazini"

Kwa hiyo inawezekana Azory yuko pahala anatafuta maisha??
 
Huyu amenukuliwa vibaya, hayo majibu kweli kiboko.
Nchi hii imekosa viongozi kabisa, kila anayekuja ni jipu
Majibu ya kipumbavu, which shows kwamba Wizara na serikali wanahusika...na waandishi nao wanakenua tu meno wakaendelea kumsikiliza huyu mpuuzi badala ya kumziria kikao chake!
Ebu tupe majibu yako juu ya hili, endapo wewe ungepewa nafasi hiyo ya kuteuliwa kuwa uwaziri wa mambo ya ndani.
 
Polisi wanasema hawajachunguza kwa kina....wewe umeingia huna hata wiki...lkn una majibu ya kuhitimisha....nn maana yake?
Tangu ukiwa waziri unaelewa hii issue


Amekuja moto kweli ngoja tuone mwisho wake.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema wizara hiyo haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited (Ltd), Azory Gwanda.

Kangi ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Julai 6, 2018 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari aliyetaka kujua mkakati wa Lugola kuhusu kupotea kwa Gwanda tangu Novemba mwaka jana.

Swali: Mheshimiwa waziri hivi karibuni kumekuwa matukio ambayo sisi waandishi wa habari yanatusumbua mojawapo ni kupotea kwa mwanahabari mwenzetu, Gwanda ambaye bado hajaonekana tangu atoweke Novemba mwaka jana.

Polisi wanasema bado hawajachunguza kwa kina. Nini kinachoendelea, hili unalizungumziaje ili waandishi wa habari tufanye kazi katika mazingira salama bila kubughudhiwa.

Lugola: Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu ametoweka. Sisi mambo ya ndani hatuingilii uhuru wa mtu kutoweka nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria.

Waziri Lugola alisema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.

“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema.

Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

"Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka," alisema Lugola

Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.

Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wiuzara ya Mambo ya Ndani.

jamaa wizara inamshinda hata kabla hajaanza.
jana katoa mguu Mbeya, ajali ikaweka guu lake.
leo hata hajasoma faili la Gwanda, yeye anakimbilia kutoa majibu aliyolishwa!

Bashite part 2!
 
Back
Top Bottom