Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Yuko sawa, madalali wajiongeze kwa kujisajili kama kampuni, iwe kampuni moja na hata wakiwa wengi hakuna tatizo, sababu watakuwa wanatambuliwa, wanalipa kodi na kujulikana rasmi, wateja wanaenda kwa madalali waliosajiliwa, wanaonyeshwa nyumba bila kulipa chochote, siku ya mkataba, mwenye nyumba ndio inakuwa jukumu lake kumlipa dalali kutokana na makubaliano yao....Mswano...
 
Kwani hata magazeti hawawezi kuweka 'classified'?
Mbona hili linashangaza kidogo!
 
Safi sana aisee!! Kongole.
Yajayp je ?? Unsweza zurula mwenyewe ukapata nyumba au chumba? Dunia nzima brokers business ipo inalipwa kwa makubaliano sasa yeye hajatoa suluhisho pia uwanja mpana sana.....muda ni mwalim mzuri sana....
 
Sawa ana maisha magumu lakini ndo achukue hela ya mwezi mzima??? Kwa kazi ipi kubwaa sana alofanya?

Imagine umepata nyumba ya laki tano, utampa laki tano dalali??
 
Msishangilie hawa watu ni wagumu kuwadhibiti mana mwenye shida ya chumba,kiwanja,nyumba au shamba anakuwa hamjui mwenye mali. So lazima apitie kwa dalali na hapo ndo mzdalali wanapowavimbia.
Zikiwekwa taratibu nzuri, watadhibitiwa tu
 
Idea nzuri sana
 
Haya maisha buana... Inawezekana kabisa Lukuvi ndo kajua mwaka huu kuwa Kuna haka ka-utaratibu ka dalali kuchukua kodi ya mwezi mmoja...wakati kina 'sie' tumekuwa tukipambana nako kwa muda mrefu sasa.
 
Sawa ana maisha magumu lakini ndo achukue hela ya mwezi mzima??? Kwa kazi ipi kubwaa sana alofanya?

Imagine umepata nyumba ya laki tano, utampa laki tano dalali??
Hapo kipengele yani! Kuna haja ya kuwekeana %! Yani dalali ale 10-20% kulingana na kiwango cha kodi. Huo ndio uwe muarobaini wa tatizo.
 
Uhakika yani wacha pakuchwe vizuri
 
Hatimae wameuona huu ujambazi!! Afadhali.
Hili suala ameliibua Mange Kimambi, alimwandikia Lukuvibbarua ya wazi,vhaijachukua hata siku moja limetolewa majibu
 
Nyumba ziwe na mabango kwa nje ,kuwa hapa Kuna vyumba vya kupanga ,huo ndio mwarobaini wa Hawa wahuni wakujiita madalali ,mfano mtu akitaka kuishi tabata kimanga ,anaingia mtaa kwa mtaa kuchek vyumba bila dalali.
Kwa wale wanaishi maisha ya juu kidogo ifunguliwe website itakuwa simple tu Ila uswaz Ni mwendo wa mabango hii itamaliza huu uhuni jumla kabisa
 
Utapataje nyumba nzuri bila madalali? shida zako ndiyo zitakupeleka kwa dalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…