Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Yuko sawa, madalali wajiongeze kwa kujisajili kama kampuni, iwe kampuni moja na hata wakiwa wengi hakuna tatizo, sababu watakuwa wanatambuliwa, wanalipa kodi na kujulikana rasmi, wateja wanaenda kwa madalali waliosajiliwa, wanaonyeshwa nyumba bila kulipa chochote, siku ya mkataba, mwenye nyumba ndio inakuwa jukumu lake kumlipa dalali kutokana na makubaliano yao....Mswano...
 
Sikujua Kumbe bado nchi iko gizani halafu bado wanasema Jiwe alikusanya kodi hivi kodi kiasi gani imepotea kwa hawa watu wanaofanya udalali??

Kuna haja ya kuwa na website za rental houses mtu akitaka anaingia na kulipa akiridhika hij ni rahisi na salama na kila kitu kiko traced!

Happ kodi itaonekana na kukatwa kodi na hizo commision za udalali zitakatwa kodi pia
Kwani hata magazeti hawawezi kuweka 'classified'?
Mbona hili linashangaza kidogo!
 
Safi sana aisee!! Kongole.
Yajayp je ?? Unsweza zurula mwenyewe ukapata nyumba au chumba? Dunia nzima brokers business ipo inalipwa kwa makubaliano sasa yeye hajatoa suluhisho pia uwanja mpana sana.....muda ni mwalim mzuri sana....
 
awaache tu, ni ugumu wa maisha, na wao wana familia za kutunza na hawana kipato kingine. bora hao hata kuturahisishia maisha wakati wa kutafuta nyumba wanapatikana, hatuwezi kukwepa ukweli kwamba wana umuhimu wake, na ukisema wawe registered walipe kodi, aisee watu wenyewe hata anapoenda kukuonyesha nyumba unamwona kabisa ni mtu anayeishi maisha magumu anatafuta ya kula tu.
Sawa ana maisha magumu lakini ndo achukue hela ya mwezi mzima??? Kwa kazi ipi kubwaa sana alofanya?

Imagine umepata nyumba ya laki tano, utampa laki tano dalali??
 
Msishangilie hawa watu ni wagumu kuwadhibiti mana mwenye shida ya chumba,kiwanja,nyumba au shamba anakuwa hamjui mwenye mali. So lazima apitie kwa dalali na hapo ndo mzdalali wanapowavimbia.
Zikiwekwa taratibu nzuri, watadhibitiwa tu
 
South Africa iwe nyumba au ofisi-Kodi ni Kwa Mwezi moja mmoja+kodi ya mwezi kama deposit(dhamana ya Nyumba au ofisi uliyopangishwa) Siku unarudisha chumba/ofisi mwenye Nyumba anakagua kama umearibu kitu mfano umevunja kioo cha dirisha au koki ya maji bafuni aifungi tena etc-atakata garama ya matengenezo toka kwenye Deposit yako. Wakati nikiwa huko my best friend alikuwa ni real estate agent(kule unasomea kwanza ndo
Idea nzuri sana
 
Haya maisha buana... Inawezekana kabisa Lukuvi ndo kajua mwaka huu kuwa Kuna haka ka-utaratibu ka dalali kuchukua kodi ya mwezi mmoja...wakati kina 'sie' tumekuwa tukipambana nako kwa muda mrefu sasa.
 
Sawa ana maisha magumu lakini ndo achukue hela ya mwezi mzima??? Kwa kazi ipi kubwaa sana alofanya?

Imagine umepata nyumba ya laki tano, utampa laki tano dalali??
Hapo kipengele yani! Kuna haja ya kuwekeana %! Yani dalali ale 10-20% kulingana na kiwango cha kodi. Huo ndio uwe muarobaini wa tatizo.
 
South Africa iwe nyumba au ofisi-Kodi ni Kwa Mwezi moja mmoja+kodi ya mwezi kama deposit(dhamana ya Nyumba au ofisi uliyopangishwa) Siku unarudisha chumba/ofisi mwenye Nyumba anakagua kama umearibu kitu mfano umevunja kioo cha dirisha au koki ya maji bafuni aifungi tena etc-
Uhakika yani wacha pakuchwe vizuri
 
Hatimae wameuona huu ujambazi!! Afadhali.
Hili suala ameliibua Mange Kimambi, alimwandikia Lukuvibbarua ya wazi,vhaijachukua hata siku moja limetolewa majibu
 
Nyumba ziwe na mabango kwa nje ,kuwa hapa Kuna vyumba vya kupanga ,huo ndio mwarobaini wa Hawa wahuni wakujiita madalali ,mfano mtu akitaka kuishi tabata kimanga ,anaingia mtaa kwa mtaa kuchek vyumba bila dalali.
Kwa wale wanaishi maisha ya juu kidogo ifunguliwe website itakuwa simple tu Ila uswaz Ni mwendo wa mabango hii itamaliza huu uhuni jumla kabisa
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Utapataje nyumba nzuri bila madalali? shida zako ndiyo zitakupeleka kwa dalali
 
Back
Top Bottom