Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Baadhi ya wenye nyumba uwaambia madalali wawatafutie wapangaji and sometimes dalali mwenyewe anatafuta nyumba ambazo zinahitaji mpangaji...

Mwenye nyumba yake awe responsible na kumlipa dalali kwa kumletea mteja.
Madalali wenyewe ndio wanapiga misele kwenye nyumba wakiona mtu anahama tu tayari wamefika wanawaambia wenye nyumba atampelekea mpangaji tena wakati mwingine wanapandiana dau.
 
Hakuna kilichobadilika apo, yaaan ni kama ugeuze mahesabu tu

badala ya kusema 6+1 = 7, useme 7+0 = 0

Wajanja na wanaomiliki nyumba za kupangisha watakua washanielewa
 
Hamna jipya apo,ni kama kubadilisha mahesabu tu

Yaan badala ya kusema 6+1 = 7, useme 7+0 = 7

Wajanja na wanaomiliki nyumba za kupangisha watakua washanielewa
 
Hajasema wasilipwe, ila ni marufuku mpangaji kutoa hiyo kodi ya mwezi mmoja isipokuwa aliyempa kazi ya kutafuta mpangaji ndio amlipe dalali so wenye nyumba ndio wanatakiwa wawalipe madalili wao and obvious kodi itapanda kwa hiyo ni mule mule tu

Mara zote Kwenye hii biashara Mpangaji ndiye anamatafuta Dalali kumuomba amtafutie sehemu
Watuache kabisa sisi ma landlords
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Hiyo ni kazi, serikali inacho paswa kudai ni kodi kutokana na mapato hayo. Pia itapata faini toka mahakamani kwa kuwafungulia mashitaka ya kufanya biashara bila ya leseni. Sioni sababu ya serikali kutoa katazo la kujinyima mapato. Iwaelekeze njia sahihi za kufanya kazi hizo.
 
Lukuvi, huo mfumo ni mgumu kuudhibiti, ni sawa na kutaka kupambana na uchangudoa.

Kuna siku nilijaribu kugoma kumlipa dalali hapo CNZA miaka hiyo, aisee wiki nzima niliishi kama digidigi ikabidi nimlipe tu kodi yake yaishe.
 
Nchi ya kipuuzi sana hii dadadeeki, kwamba hapo Lukuvi kaongea boooonge la hoja..!!
 
Anayekwenda kwa dalali kufata huduma ndo huyo huyo alipe!

Mambo yasiwe mengi!
Hata mimi nashangaa yani mtu kamfuata dalali huko ili apate huduma yake halafu et mimi mwenye nyumba ndio nilipie hiyo huduma kwa kumlipa dalali!!
 
Sawa amlipe yeye huyo dalali! Sio amtwishe gharama mpangaji huo si uungwana.

Na hata wenye nyumba wanaowalipa madalali hawawapi mwezi mmoja Kama wanavyotaka wapangaji tuchajiwe. Unakuta anapozwa elfu 20 anatulia ila mpangaji anataka ampe mwezi mzima si uhuni huo!
Ila mpangaji ndio humtafuta dalali ili apate huduma yake na wakati mwengine mwenye nyumba hata hamjui huyo dalali, sasa kwa mazingira hayo iweje mwenye nyumba ndio amlipe dalali?
 
Mtu asiyeongeza thamani yeyeto kwenye kitu au huduma huyo ni parasite anavuna asipopanda.Madalali ,politishun bure kabisa.
 
Ila mpangaji ndio humtafuta dalali ili apate huduma yake na wakati mwengine mwenye nyumba hata hamjui huyo dalali, sasa kwa mazingira hayo iweje mwenye nyumba ndio amlipe dalali?
Sasa mwenye nyumba hataki mpangaji aje mwenyewe unamuelewaje
 
Hivi kweli hakuna kazi za kufanya?
Si kweli bali hii kazi ya udalali ni sawa na kubet tu, hebu fikiria kwamba et kisa unajua kwamba nyumba fulani kuna chumba kinapangishwa basi kiasi cha kumchukua mtu na kumpeleka tu et unapata kodi ya mwezi mzima kwa kazi kubwa ipi hapo?

Nakubali umuhimu wao madalali ila sio huo mfumo waliyouweka wa kutaka kodi ya mwezi mzima.
 
Huwezi kuzuia madalali kulipwa kwa sababu ni makubaliano rasmi kabla mpangani hajapelekwa kuoneshwa nyumba, kama hutaki basi zoezi linaishia hapo. Hivyo mpangaji atalipa tu atake asitake kama kweli anahitaji nyumba/ chumba.
Kuna wapangaji huwaga wanawadhulumu madalali hawawalipi, unakuta dalali anakuja kulalamika kwa mwenye nyumba.
 
Back
Top Bottom