Kwa Mara Ya Kwanza Ninawaona Wale Wanaoonekana Kuwa Na Maarifa Mengi Wakifichuo Hisia Zao Bila Ya Wenyewe Kujua!
Hivi Ni Kweli Nyinyi Hamujui Tofauti Ya TREASON (UHAINI) na TERRORISM (UGAIDI) ?
Kwasababu Yule Jamaa FETULLAH Anajuilikana Kimataifa Kuwa Ni Mtu Anaepigania Mageuzi Nchini Turkey, Na Ndiyo Maana Mataifa Ya Magharibi Yote Yanamuunga Mkono ikiwemo Marekani Ambayo Imempa Hifadhi Kwenye Nyumba Maalum Akilindwa Na Maafisa Wa Uslama wa CIA.
Na Mapinduzi Yaliyofanyika Uturuki Yaliungwa Mkono Na Marekani pamoja Na Mataifa Ya Ulaya Wakisema Kuwa Yangelifanikiwa Mapinduzi Hayo, Basi Wangelikuwa Wanaumaliza Ugaidi!! Kumbe Kwa Mtazamo Wa Wamagharibi Erdogan Ndiye Gaidi.
Serikali Ya Uturuki imeamua Kuwa Wale Wahaini Waliojaribu Kumpindua Rais Kuwaita MAGAIDI, Hivi Kumbe Maana Ya Gaidi Kwa Mtazamo Wako Na Mtazamo wa Waturuki Ni Yule Anaetaka Kumpindua Raisi??
Kwahiyo Wale Waliotaka Kumpindua NKURUNZIZA nao Ni Magaidi???
CCM waliopindua Zanzibar (1964) Nao Ni Magaidi??
Mkuu Si Kila Linapotumika Neno Ugaidi Unatakiwa Kuliunga Mkono eti tu Waliolengwa Ni Wafuasi Wa Dini Fulani.
Hayo Ni Maswala Ya Kisiasa si Ya Kidini.
Serikali Ya CCM zanzibar imeamua Kuvunja Maduka Ya Wapemba Pale Darajani Mjini Unguja wakiamini Kuwa Kuuwa Upinzani ni Lazima Uondoshe Zile Sehemu Zao Za Chanzo Cha Mapato.
Na Mfano Huo Ndiyo Anaotumia Erdogan Kutaka Kuuwa Upinzani Kwa Kuvunja Vyanzo Vyao Vya Mapato Kwa Ktumia Jina la Kuwabambikizia Ugaidi.
Tanzania Haiizidi Marekani Kwa Intelijensia, Mbona Marekani imekataa Kumlabel Fetullah Kuwa ni Gaidi?? Kwasababu inajua Kuwa Fetullah ni Mwanaharakati Anaepigania Demokrasia Na Wala si Ugaidi.
Ulipashwa kuelewa contents za habari kabla huja react. Sijui ni wapi ulipoona mtu anasema ugaidi ndio uhain.
Serikali ya uturuki, kupitia balozi yake, imesema huyo Fetullah kwa kushirikiana na wamiliki wa Feza shule, wamehusika katika jaribio la kuipindua serikali ya uturuki.
Mwandish amebainisha kwamba Fetullah, umiliki wa Feza shule, na baadhi ya wafanyabiashara pia wanajihusisha na ugaidi. Na kwamba **** michakato hata katika Feza shule yenye vinasaba vya ugaidi.
Hakuna sehemu mtu amesema uhaini ndio ugaidi.
Pili tunajadili mada iliyoko mezani kutoka Uturuki.
Hatataki kufanya maamuzi ya kisiasa wala mihemuko. Tunataka uchunguzi wa kina ufanyike ili kubainisha ukweli.
Kwamba hao siyo magaidi bali ni wahaini ambao serikali ya uturuki imeamua kuwaita magaidi, hili ni jipya. Let chanzo chako bayana cha habari kwa sababu, haya mambo yote yanamwelekeo mmoja. Yanaweza kufanywa kwa mara moja ama kwa nyakati tofauti lakini lengo ni moja. Tofauti approach. Kwa hiyo mtu kuwa gaidi, halafu akawa haini ni sawa na uji wa sukari na ukwaju.
Kwa hiyo naomba ujadili hoja kama ilivyo usipindishe ama kwa kusudi ama kwa bahati mbaya.
Kama hivi unaonyesha kuwa na ufahamu mpya kwamba serikali ya Uturuki inafanya makusudi ama haijui hivyo inchanganya ugaidi na uhaini, unaweza kutuwekea chanzo chako hapa tujajili.
Tunahitaji amani na usalama wa dunia.
Ahsante.