mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi.
shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM.
miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni.
nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha.
ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia.
Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu.
kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani.
Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule.
rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe.
huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan.
shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.