Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

"Uturuki imetuambia"
Fanyeni uchunguzi wenu
Vita vya kisiasa vya Erdogan na Gullen visituhusu
Matter ofa fact Erdogan alihaidi mengi sana kuhusu kuborosha uchumi wa Turkey
Kama tu Magufuli alivyotuhaidi watz
Lkn siku zikawa zinakwenda hali ikawa ndiyo mbaya zaidi
UCHUMI ulitaka umpindue Ardogan asisingizie shaba
 
Watu wengine kila sehemu mnatamani kujamba tu, hivi wewe mwislamu mvaa kandambili una jeuri ya kumsomesha mtoto wako FEZA School? Au unadhani ile ni Al almain?

Feza malipo ni kwa dola hakuna hata sheikh ubwabwa mmoja mwenye jeuri ya kupeleka mtoto wake pale.
Bahati mbaya Pengo haruhusiwi kujamiiana hivyo hana watoto !
 
Ye si rais malaika akae pale milele, inamana hata watanzania magaid kama wanadai hao hivyo, mana wanakaa nchini kivyovyote tunajua kichojir wasituchafue wauane wenyewe yetu yanatushinda itakuwa kufadhili magaid, dikteta mkubwa
 
Wagaratia wanaozungumziwa kwenye biblia ndio Waturuki haswa.. Nadhani waislam wote waeleweni hii jamii ndio tabia yao wakigombana wao kwa wao na wewe una urafiki nao wote wanakuambia uchague upande mmoja. Zama hizo waliitwa watu wapumbavu.

Erdogan anatumia mwanya Wa mapinduzi kuteketeza adui zake wote... Hadi walimu wauza pipi n.k yaani mpango wake sio kuwazuia au kuwafunga Bali kuwanyonga wote... Watatoa msimamo wao soon na hizo shule watazichukua serikali ya Ankara
Ukiristo ulianzishwa na Paulo katika mji wa Antiokya uliopo Uturuki, kasome Biblia Duduwasha. Wanafunzi wa kwanza waliitwa Wakiristo hapo Antiokya
 
Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
Walikuwa wapi mda wote huo wasiseme waache siasa za maji taka
 
Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
Hizo ni akili za kuambiwa,mkuu by the way taarifa inaendelea kufanyiwa kazi
 
The bottom line of the entire story ni udini. Shule za FEZA ndio zilionekana kutoa upinzani mkalikwa shule za makanisa na hili lilikuwa halifurahiwi. Kama zilikuwa zinatumia mbinu za kigaidi kufundishia wanafunzi(sijui ndio maana wanafanya vizuri mitihani yao) Serikali ilikuwa wapi wakati wote huo " isiwashughulikie"? Wacheni unafiki wa kidini tena kweupe

kwan wanaosoma hapo wote wasilamu?? Tena hata wanaofauli sana wengi sio wasilam
 
Watanzania ni waongeaji sana. Huenda hili likawa moja ya sababu zinazochelewesha maendeleo yetu
 
Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
kwani waturuki si ni wafuasi wa ile dini pendwa, dini ya Haki. Balozi wa Uturuki ndio anaomba shule ifungwe , sio Pope anayeomba hivyo, wala sio Pastor Emmanuel Munguatosha
 
mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi.

shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM.

miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni.

nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha.

ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia.

Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu.

kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani.

Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule.

rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe.

huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan.

shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.

Umeanza vizuri ila umemalizia kijinga sana hao wataalamu wapo wapi??
 
Hata Mandela, Samora, Mugabe na wakombozi wengine waliwahi kuitwa magaidi. Imekuwa ni fashen kwa kila anayepinga status quo anaitwa gaidi! ili kulinda maslahi kikundi.
NADHANI Feza inaingizwa mkumboni kutokana na rekodi yake njema katika kutoa elimu bora nchini, jambo haliwapendezi baadhi ya wafafidhina waliokwishazoea kuona shule za madhehebu Fulani tu zikiongoza katika utoaji wa elimu bora! Ni tafakuri binafsi tu ambayo haitakuwa na nguvu km serikali itayapuuza madai hayo pandikizi!

Inferiority inawasumbua sana
 
You Nailed it Bro, nimesoma University na wanafunzi waliosoma Feza, napenda niseme kweli jamaa wapo serious na kitabu na nidhamu ya hali ya juu. tusije tukaentertain mambo ya nje yavuruge mazuri yetu ya ndani.

hao walikua wametoka feza na ni watoto wa masikini, ila wa matajiri hawana usiriaz na shule kabisaaaa walifaulu kwa kua kazi yako ni kumeza tu
 
*****, hivi kwa hali hii unafelije.?

Ilipaswa hili shule liwe chuo kikuu cha dodoma ( Natania tu).

Ni nouma afrika mashariki na kati.

Dah mimi mkali sana asee na wengine tunafaulu katika mazingira magumu sana SANA hakika ukipata two hapo wewe kilaza SANA kwa shule hii
 
Mwenyekiti wa bodi amejibu tuhuma kirahisi sana hao wamiliki anaweza kuwataja akipelekwa mahakaman?? Ili hali inajulikana ni waturuki
 
hao walikua wametoka feza na ni watoto wa masikini, ila wa matajiri hawana usiriaz na shule kabisaaaa walifaulu kwa kua kazi yako ni kumeza tu
Watoto wa maskini wanafikaje feza boys/girls mkuu maana ada yao kwa mwaka ni kubwa kuliko ada ya mwanachuo anayesomea engineering kwa miaka yote mitatu.
 
Back
Top Bottom