Napoleone
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 10,087
- 16,036
Wakalipwe 1.2m????...PASCAL MAYALA na HAJI MANARA kitenisi hicho mmerushiwa ,mkishindwa kukishambulia msimlaumu mtu
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakalipwe 1.2m????...PASCAL MAYALA na HAJI MANARA kitenisi hicho mmerushiwa ,mkishindwa kukishambulia msimlaumu mtu
Kwa erratic nature ya flow ya umemem kwa sasa nchini, hakuna kitengo chochote cha habari ambacho kingeweza kuhabarisha umma adequately. Umeme unakatika saa nne kamili , unarudi saa nne na dakika saba, unakatika tena baada ya dakika 12 na unarudi ndani ya dakika 3. Sijui wewe kama mtu wa kitengo cha habari unasemaje kuhusu mtiririko huu wa umeme?Waziri wa Nishati Mh Makamba amevunja kitengo cha habari na mawasiliano Tanesco akikituhumu kimeshindwa kulisemea shirika na kulitetea shirika kwenye nyakati ambazo kitengo na watu wake kimetakiwa kufanya hivyo!
Ikumbukwe kitengo cha habari na mawasiliano kinaongozwa na mwana dada Badra Masoud kwa misingi hiyo amekali kuti kavu ...
Maswali ya kujiuliza...
Ni kweli kitengo hichi ndicho tatizo kwenye shirika?
Ni kweli wameshindwa kuitetea tanesco?
View attachment 2095460
Nchi inasimamiwa na kuendeshwa na Rais mstaafu, what do you expect?TATIZO LA TANESCO NI MAKAMBA MWENYEWE NA ANATAKIWA AJIFUNGE KAMBA MWENYEWE.
ASITAFUTE WA KUMUANGUSHIA JUMBA BOVU.
KITENGO CHA HABARI WANGESEMA NINI KILA SIKU WAKATI HAKUNA SABABU ZA KUSEMA?
MWISHO WA UONGO UMEKARIBIA.
Makamba anavyodai kitengo kimeshindwa kuitetea Tanesco ana maana gani? anataka kitengo kiwe kinazalisha propaganda au kifanyeje?
Navyojua hao watu wa idara ya habari wanatakiwa kupewa taarifa za majibu ya kero za wateja kutoka kwa wahusika (waziri, naibu wake, katibu mkuu nk) then wao ndio watangaze taarifa hizo kwa umma.
Sasa mfano wananchi wakiulizia ujio wa ile winchi ya tani 26 toka huko ilipoagizwa mbona mpaka leo kimya? Makamba anataka hao jamaa wa kitengo cha habari wajibu kitu gani kama hajawapa majibu?
Hasemi Arusha alifata nn anakimbilia kwenye wasemajiMwandishi wetu,Arusha
Waziri wa nishati ,January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja afisa habari wa shirika la umeme nchini(Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.
Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.
Waziri Makamba ametoa maagizo hayo Leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.
Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.
"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya " alisema Makamba
Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.
"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba
Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.
"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba
Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.
"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara " alisisitiza Makamba
Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.
"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba
Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.
Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.
Mwisho.
View attachment 2095358View attachment 2095359View attachment 2095360View attachment 2095361View attachment 2095362
ahahahahahaaaa,,,,,, Makosa ya benchi la ufundi😀😀😀[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tena atatufaa sana anaweza akasema mtatusamehe mpira umepiga transformer umeme umezima ila utarudi haraka baada ya wiki
labda kule twita kuna wadau wao wa nguvu, sisi wengine wakina kabwela kajamba nani, taarifa wanaona hazina umuhimu kwetu.Taarifa ni muhimu
Kuna kipindi tulikuwa tunapata sms kuwa tarehe fulani saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni hakutakuwa na umeme, kuna matengenezo
Siku hizi taarifa wanatoa Twitter
ahahahahahaaaa,,,,,, Makosa ya benchi la ufundi😀😀😀
Badra masoud wa wapi wewe, si kila kitu u akurupuka tu. Google hapo afisa habari wa tanescoKwa hiyo Badra Masoud anahamishiwa kwenye kubeba mistimu ya umeme sio
Wapatie watu vifaa mkuu sio unapanga kwa maneno tu., sasa umeme unakatika mara kwa mara unategemea ni maneno mdomoni tu, mwaga nguzi za umeme kila kata kila kijiji mamashine tuone kama kweli mnataka mitano tenaMwandishi wetu, Arusha
Waziri wa Nishati, January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja Afisa Habari wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.
Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.
Waziri Makamba ametoa maagizo hayo leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.
Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.
"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya" alisema Makamba
Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.
"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba
Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.
"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba
Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.
"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara" alisisitiza Makamba
Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.
"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba
Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.
Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.
Mwisho.
View attachment 2095358View attachment 2095359
Si umtaje tu maana nimesoma mwananchi wamemtaja huyo dada, Kama unamjua unasema tu sio iwe ishu sanaBadra masoud wa wapi wewe, si kila kitu u akurupuka tu. Google hapo afisa habari wa tanesco