Waziri Makamba: Kila nyumba itakuwa na mtungi wa gesi

Waziri Makamba: Kila nyumba itakuwa na mtungi wa gesi

Mkaa ni ghali kuliko gesi? Kwa dar au nchi nzima? Maana mikoani gunia elfu 10 ambalo mtu mwenye familia anatumia miezi miwili. Ila gesi ya elfu 60 hata wiki mbili hatoboi.

Ukweli kwa hili mm toka siku ya kwanza natamani nikutane na makamba nimueleze
Mkoa gani mkaa gunia elfu kumi babu!?..mkaa gunia hutoboi mwezi ilhali mtungi wa 54 unatoboa mwezi unusu na familia ya watu watano
 
Serikali imesema ina mikakati ya kuhakikisha kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia
Deal man na harakati za Taifa Gas......tutashtuka baadae sana kuwa si lolote isipokuwa ni kuinadi taifa gas!
 
Mitungi yote au
Mtungi ni huu.
Screenshot_20221004_095735.jpg
 
Serikali imesema ina mikakati ya kuhakikisha kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia na kuandaa mifumo mbalimbali kupitia uvumbuzi wa kibiashara ikiwemo kutumia teknolojia ya kupima gesi kidogo kidogo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Oktoba 21, 2022 na Waziri wa Nishati, January Makamba alipokuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Clouds kupitia kipindi cha Clouds 360.

Amesema utamaduni wa Watanzania ni kununua vitu kidogo kidogo hivyo wengi hawaoni unafuu wa gesi kwa kuwa inauzwa katika mitungi mikubwa.

“Kuwa na mtungi wa gesi kila nyumba inawezekana ni suala la kujasiliana maeneo ya vijijini wengi wanasema hawawezi kumudu, wakala yuko mbali siwezi kujaza. Ifike wakati mtu akiishiwa gesi kuna namna anaweza kuipata kwa haraka ukiangalia takwimu Tanzania tupo chini ya kilo 2 kwa matumizi ya mtu mmoja kwa mwaka wenzetu wapo kilo 46 lazima tuangalie tunafanya nini.

“Serikali tumechukua hiyo changamoto na tunaifanyia kazi, tunaona kama Je? Serikali iweke ruzuku, kodi iondolewe au ni vinginevyo,” amesema.

January amesema wengi wana kipato kidogo na matajiri na wenye kipato cha kati wanaomudu ni wachache, hivyo inabidi Serikali iangalia namna ya kulisaidia kundi hilo.

“Mitandao ya simu walifanikiwa baada ya kuweka vocha ndogondogo, ili nishati safi ya kupikia ishindane na mkaa itawezekana tukitumia teknolojia kuwezesha hata gesi iuzwe kwa bando, pale pana mita unaweka mpesa unafungua mita unaingiza gesi ya Sh100 unapika inaisha zipo vumbuzi ikawa moja ya majawabu inawezekana kuweka mitungi kila nyumba, kupitia uvumbuzi wa kibiashara,” amesema.

Mwananchi
Hii nafikiri ndiyo tunaita ndoto ya mchana kweupe. Yaani mtungi kila kaya. Nafikiri itafika mahali tuwe na malengo yanayoweza kutekelezeka ama sivyo tutakuwa tunapiga siasa zxa uongo na majisifu yasiyokuwa na ukweli ndani yake.

Ni juzi juzi tu Makamba aligawa mitungi michache kwa maana ya "pilot study". Ile mitungi ilipokauka ukawa ndiyo mwisho. Huenda yale maganda (mitungi mitupu) iliishauzwa kama chuma chakavu. Sasa unatuletea hadithi ya gesi ya mita.

Tulianza na umeme wa REA. Tukiwaaminisha wanavijiji kuwa umeme unakuja kwao na kila mtu anayetaka umeme atapata. Kilichotokea kwenye vijiji vingi ni umeme kupelekwa kijijini na kufungwa kwenye shule au zahanati. Wananchi wengine wote hawakupata transformer za kuwawezesha kupata umeme. Ukiwauliza wanasema kipaumbele ni taasisi za kiserkali. Mtu akiomba umeme anaam,biwa zinahitajika nguzo kadhaa na bei yake ni hii. Sasa kuna faida gani ya umeme kufika kijijini huku wananchi hawaupati? Sasa tena tunrukia gesi, kwa nini tusimalize ya umeme kwanza? Yeye gesi ya meter kufika vijijini labda miaka 50 au zaidi!
 
hili swala unalolibishia kuwa haliwezekani ndio M-Gas tunalifanya tunapeleka mitungi ya gesi kwenye kaya bure kabisa. Ukitaka kujua zaidi piga 0747744895
 
Wakafanye study Japan waone wamewezaje kuingiza system za gesi kwenye nyumba.

Serikali iwekeze kwenye real estate ,wajenge nyumba kama za nhc kwa ajili ya kupangisha watu wa kipacho cha chini then in the future ni big generating income.....wakishajenga waoutsorce wao wawe wanapewa targeted amount yao tu kila mwezi.
 
Back
Top Bottom