Waziri Makamba: Kila nyumba itakuwa na mtungi wa gesi

Waziri Makamba: Kila nyumba itakuwa na mtungi wa gesi

Jamaaa anahangaika sana kufanya tumuamini wait and see siku hizo ndo watajua this is Britanicca, Tuna mashoka yetu waiting to grab them when the time allows
 
Naona nawe unafanya biashara kama Makamba, hiyo gesi ya buku itakuwa ya kuchemshia chai ya rangi.
Huyo mtu ni mpumbavu aliyelitiliza, aamahisi wote ni Watoto humu. Gesi ya buku hata nusu saa haifiki
 
Taifa gas marketing manager!

Rostam Aziz amewa-rob Nape na Makamba kiasi hawaoni kuwa wanawakilisha wananchi. Wamebaki kumfanyia kazi za kumtetea na kumtafutia masoko kampuni zake za mawasiliano na gesi
 
Taifa gas ni kampuni ya kitanzani,ni mkakato wa nchi kuhamia kwenye gesi,ndiyo maana wanatandaza mabomba ya gesi,acha roho ya kimasikini
Unaposema taifa gas ni kampuni ya kitanzania unamaanisha nini?! " Ndiyo maana wanatandaza mabomba ya gesi" Unamaanisha ni hao taifa gas wanatandaza mabomba?

Ni maswali mawili tofauti, nijibu tuanze mjadala hapa,..
 
Serikali imesema ina mikakati ya kuhakikisha kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia na kuandaa mifumo mbalimbali kupitia uvumbuzi wa kibiashara ikiwemo kutumia teknolojia ya kupima gesi kidogo kidogo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Oktoba 21, 2022 na Waziri wa Nishati, January Makamba alipokuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Clouds kupitia kipindi cha Clouds 360.

Amesema utamaduni wa Watanzania ni kununua vitu kidogo kidogo hivyo wengi hawaoni unafuu wa gesi kwa kuwa inauzwa katika mitungi mikubwa.

“Kuwa na mtungi wa gesi kila nyumba inawezekana ni suala la kujasiliana maeneo ya vijijini wengi wanasema hawawezi kumudu, wakala yuko mbali siwezi kujaza. Ifike wakati mtu akiishiwa gesi kuna namna anaweza kuipata kwa haraka ukiangalia takwimu Tanzania tupo chini ya kilo 2 kwa matumizi ya mtu mmoja kwa mwaka wenzetu wapo kilo 46 lazima tuangalie tunafanya nini.

“Serikali tumechukua hiyo changamoto na tunaifanyia kazi, tunaona kama Je? Serikali iweke ruzuku, kodi iondolewe au ni vinginevyo,” amesema.

January amesema wengi wana kipato kidogo na matajiri na wenye kipato cha kati wanaomudu ni wachache, hivyo inabidi Serikali iangalia namna ya kulisaidia kundi hilo.

“Mitandao ya simu walifanikiwa baada ya kuweka vocha ndogondogo, ili nishati safi ya kupikia ishindane na mkaa itawezekana tukitumia teknolojia kuwezesha hata gesi iuzwe kwa bando, pale pana mita unaweka mpesa unafungua mita unaingiza gesi ya Sh100 unapika inaisha zipo vumbuzi ikawa moja ya majawabu inawezekana kuweka mitungi kila nyumba, kupitia uvumbuzi wa kibiashara,” amesema.

Mwananchi
Kuandika hotuba bana anawaza tu kupandisha biashara ya aliyembeba na mbeleko kwenye siasa. Yaani anawaza watanzania wawe masikini kwa kununua gesi utadhani ndio maendeleo. Yaani anataka ama anawaza namna Taifa gesi iuzike ili amfurahishe.
Sasa yeye hawazi inakuwaje tuwe na kipato kwa kila mtu japo umasikini upungue.

Sikia jkk aliuza gesi yetu sijui kwa watu Gani. Raisi wa wanyonge alivyotaka umeme nafuu akakuta gesi imeshauzwa kitambo na tunauziwa kwa Bei ghali mno.

Sasa jpm akakimbilia bwawa la nyerere ili tuweze kuzalisha umeme mwingi na nafuu ikashindikana.
Ndio Mana ikabidi akimbilie bwawa la nyerere Sasa marope analipinga hili suala la bwawa kwa nguvu zote hata Samia naye Mana amewekwa hapo na alitolewa huko zenji akawa makamu nadhani Hana nguvu ya kuendeleza bwawa kwanza tunakamuliwa mpaka watu wapate faida kwa hela walizowekeza kwa gesi baadaye ndio watakamilisha bwawa Ila watakuwa wameshatunyonya mno.

.Yani bana anataka wote tununue Taifa gesi amegawa kuhamasisha Ila hakuna kitu
 
Unaposema taifa gas ni kampuni ya kitanzania unamaanisha nini?! " Ndiyo maana wanatandaza mabomba ya gesi" Unamaanisha ni hao taifa gas wanatandaza mabomba?

Ni maswali mawili tofauti, nijibu tuanze mjadala hapa,..
Sentensi 'mkakati wa nchi kuhamia kwenye gesi' hukuiona!?
 
Ni jambo jema sana , ikiwa tutakuwa tunaweza kuprocess gas yetu wenyewe tukaisambaza kwa wananchi.
Lakini kama tunaagiza toka nje ,sioni kama litakuwa future , zaidi naona upigaji wa ten per kwenye makampuni makubwa ya gas
 
Taifa gas ni kampuni ya kitanzani,ni mkakato wa nchi kuhamia kwenye gesi,ndiyo maana wanatandaza mabomba ya gesi,acha roho ya kimasikini
Manjis Gas ni ya Russia? Lake Oil gas ni ya Ukrane? Pia kaa ukijua kuwa hata hayo makampuni ambayo unasema ni ya nje yapo ubia na Government hii hii ya Mama Samia, sielewi unachotaka uzungumze unless huona hoja na hujui unachoongea! Sione wote maboya bro.... mpo kimkakati kupiga deal not otherwise!!
 
Mkaa ni ghali sana kuliko gesi, pia unapoteza muda na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na uvunaji miti.
Mkaa ni ghali kuliko gesi? Kwa dar au nchi nzima? Maana mikoani gunia elfu 10 ambalo mtu mwenye familia anatumia miezi miwili. Ila gesi ya elfu 60 hata wiki mbili hatoboi.

Ukweli kwa hili mm toka siku ya kwanza natamani nikutane na makamba nimueleze
 
Manjis Gas ni ya Russia? Sione wote maboya bro.... mpo kimkakati kupiga deal not otherwise!!
Manjis gas siyo serious Kama taifa,ulitaka kampuni ya nje Kama oryx ndiyo ipewe kipaumbele!?...gas ni future,haiepukiki,so tutumie kampuni gani!?
 
Mkaa ni ghali kuliko gesi? Kwa dar au nchi nzima? Maana mikoani gunia elfu 10 ambalo mtu mwenye familia anatumia miezi miwili. Ila gesi ya elfu 60 hata wiki mbili hatoboi.

Ukweli kwa hili mm toka siku ya kwanza natamani nikutane na makamba nimueleze
Gharama kwa maana ya impact kwenye mazingira. Kiafya na mengineyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom