Hivi winchi ni kitu cha kusema haipo, tena waziri mzima, kabla hata ya mradi kuanza, inajulikana kila aina ya nyenzo zinazohitajika kwa kazi fulani, na hiyo ndio kazi ya mkandarasi, alafu huyo mkandarasi ana uwezo mkubwa tu. Alafu waziri anasema easily hakuna winchi, hii ni njia ya makusudi kuchelewesha mradi au kuuhujumu, imagine JPM angekuwa hai ndio Rais, hivi Makamba au waziri yeyote angethubutu kusema haya? Kwanza hii ni dharau kwa SSH.
Mama Samia Rais wangu, angalia sana huyu January, juzi kati tena tumesikia Tanesco wameingia mkataba wa USD 30 mil.. Takriban 69 bil tshs. Jamani, Mh. Rais mchunge huyu mtu, hatujakaa sawa mara gharama za kuchimba gesi tril 70.. Eeeeh eeeh, Mama yangu jamani, ebu mwangalie kwa umakini sana huyu January. Tril 70 ni gharama zote hizo kweli kwa ajili ya gesi kweli? Matrilioni hayoo jamaniiiii, OMG. Sasa kama ni tril 70, hiyo gesi hao wawekezaji si watatumia miaka 100 hadi warudishe gharama zao.. Mwanzoni tuliambiwa gharama ni tril 40 tu, ghafla imekuwa tril 70 za Tshs.