Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,969
- 3,392
Ufisadi hautakaa kutuacha salama. Ukiona hivyo wanataka kuanzisha ile project ambayo Mama Samia aliipiga chini, ya kujenga storage facility ya TPA. TIPER kuna tanks zimekaa bila mafuta sababu hakuna anayefanya storage, na serikali ina hisa zake. PUMA pia serikali ina hisa zake na haijawahi kujaa.Nimeona luninga Waziri Makamba akitamba kuwa Tanzania itafanywa kuwa kituo kikubwa cha usambazaji mafuta.
Mimi nikifikiri serikali itafufua kiwanda cha refinery cha TIPER, kumbe sivyo.
TIPER, Tanzania Italian Petroleum Refinery, ilianzishwa na Mwalimu Nyerere kama strategic plant around 1965.
Serikali ya Awamu ya pili chini ya Rais Mwinyi ilifanya KOSA KUBWA kuua kiwanda cha TIPER.
Katika kiwanda hiki nchi ililuwa ikiagiza tu crude oil, a one off operation.
Katika crude oil baada ya ku refine na kudistill hiyo crude oil, utapata mafuta aina zote hadi lami na mafuta ya vaseline.
Kilichotokea wakati wa Mwinyi kwa hakika ni cha kulaumiwa maana haieleweki kwanini tuagize finished product badala ya kuagiza malighafi ambayo itatoa mafuta aina zote na bidhaa nyingi za ziada.
Lami iliyokuwa inapatikana kama by product sasa hivi wanafaidishwa wafanyabiashara wakubwa kwa gharama za usafiri.
J Makamba, be strategic.
Hii project ya TPA ni ya nini sasa? Tujifunze kufahamu wakati ukuta. Haya tunayofanya tutakutana nayo mbele ya safari