Waziri Makamba, nakushauri kuwa 'strategic thinker' suala la mafuta. Fufueni TIPER

Mkuu Jidu La Mabambasi kwanza naunga mkono Tanzania kuwa na a big oil refinery, eneo ilipokuwepo Tipper but not necessarily Tipper ndio ifufuliwe, zile mashine za Tipper kwa sasa ni obsolete, zifunguliwe zipelekwe kwenye chuma chakavu.

January Makamba ni very strategic, msikilize hapa akizungumzia hilo

Kwa vile baadhi ya nchi majirani zetu, zinaagiza mafuta nje ya nchi kupitia Dar Port, J. Makamba is very strategic and very right, tukijenga huge oil storage tanks, sisi ndio tukafanya bulk procurement, hizo nchi badala ya kuagiza mafuta kutoka huko, wataagiza kutoka kwetu, hivyo Tanzania kuwa an oil hub.

Kama ni kujenga refinery, tuijenge Chongoleani, Tanga, tununue mafuta ya Uganda, tuachane na kuagiza mafuta ya Waarabu.

Kumhusu January Makamba, karibu pande hizi

P
...kuna eneo kigamboni walitengwa wa Zambia kwa ajili ya kuweka storage yao ya mafuta, JPM baada ya kuskia Zambia wanataka kujenga Storage tanks zako na ss tunanang'aa macho akalimega lile eneo ili na sisi tuwe na storage yetu pale...

Zambia walishapata mkandarasi wa kujenga though mchakato umesimamishwa...on our side tuliua kwenye mchakato wa awali bt hapa katikati ukafa a natural death hasa baada ya bi mkubwa kuuponda huo mradi kwenye ufunguzi wa Gati za Bandari...
Am not sure Makamba ana come from which angle...

JPM hakua Mwanasiasa mzuri bt he had visions...From Reli, Bandari ya Tanga down to Mtwara to those Fuel storage facilities u can see this guy kuna kitu alikua anataka ku achieve...

With January is doubt....he is not a doer, ni mwanasiasa, maneno maneno mengiiii, bt utendaji na ku deliver ni almost hakuna kitu
 
Hela za kujenga Nyerere Hydro Power Plant na SGR tumepata wapi?
Lazima kuthink forward.
Mbona una majibu ya kitoto? Benki ikikukopesha kufanya mradi A haimaniishi itakukopesha kufanya mradi B au kufanya mradi C.

Kuna factors nyingi zinaenda kabla hawajatoa mkopo.

Kama una hakika ya kupata hizo hela za kujenga refinery ndiyo useme zitatoka wapi.
 
...kuna eneo kigamboni walitengwa wa Zambia kwa ajili ya kuweka storage yao ya mafuta, JPM baada ya kuskia Zambia wanataka kujenga Storage tanks zako na ss tunanang'aa macho akalimega lile eneo ili na sisi tuwe na storage yetu pale...
Kigamboni mbona maeneo ni plenty?, kwanini amege eneo la yeyote?, kwa Zambia, tuna TAZAMA Pipeline, na wana matenki ya kutosha kwa uwezo wa ile line, unless kama ni increased demand hivyo they need increased supply na increased storage.
Zambia walishapata mkandarasi wa kujenga though mchakato umesimamishwa...on our side tuliua kwenye mchakato wa awali bt hapa katikati ukafa a natural death hasa baada ya bi mkubwa kuuponda huo mradi kwenye ufunguzi wa Gati za Bandari...
Sidhani kama aliuponda, bali mpango mkakati wa upanuzi wa Bandari ya Sar Port, tunatenga storage za kufa mtu pale Kurasini, hivyo Kigamboni watasubiri.
Am not sure Makamba ana come from which angle...
Msikiliza kwa makini Januari hapo, utaijua angle yake

JPM hakua Mwanasiasa mzuri bt he had visions...From Reli, Bandari ya Tanga down to Mtwara to those Fuel storage facilities u can see this guy kuna kitu alikua anataka ku achieve...
Its true JPM hakuwa mwanasiasa wa politicking, he was a doer, maneno mafupi, vitendo virefu, he had a vision ya Tanzania anayoitaka, and mission to accomplish, but tatizo ni yale mambo yake mengine... kwenye hayo, naomba tumwache marehemu apumzike kwa amani.
With January is doubt....he is not a doer, ni mwanasiasa, maneno maneno mengiiii, bt utendaji na ku deliver ni almost hakuna kitu
I'd like to differ, you just sit and watch!.
Kuna wengi wanadhani wanamfahamu January, lakini sii kweli, wengi wanamfahamu January kijuu juu tu, kwa kuwasaidia kumfahamu vizuri January, karibu mitaa hii
P
 
Nimeona luninga Waziri Makamba akitamba kuwa Tanzania itafanywa kuwa kituo kikubwa cha usambazaji mafuta.

Mimi nikifikiri serikali itafufua kiwanda cha refinery cha TIPER, kumbe sivyo.

TIPER, Tanzania Italian Petroleum Refinery, ilianzishwa na Mwalimu Nyerere kama strategic plant around 1965.

Serikali ya Awamu ya pili chini ya Rais Mwinyi ilifanya KOSA KUBWA kuua kiwanda cha TIPER.

Katika kiwanda hiki nchi ililuwa ikiagiza tu crude oil, a one off operation.

Katika crude oil baada ya ku refine na kudistill hiyo crude oil, utapata mafuta aina zote hadi lami na mafuta ya vaseline.

Kilichotokea wakati wa Mwinyi kwa hakika ni cha kulaumiwa maana haieleweki kwanini tuagize finished product badala ya kuagiza malighafi ambayo itatoa mafuta aina zote na bidhaa nyingi za ziada.

Lami iliyokuwa inapatikana kama by product sasa hivi wanafaidishwa wafanyabiashara wakubwa kwa gharama za usafiri.

J Makamba, be strategic.
Kipindi hicho unachokitaka cha Nyerere,mafuta yalikuwa kwa foleni, mafuta ya mgao,,hayapatikani,kutokana na ukosefu wa mafuta,oil ilikuwa kupata tabu,lami hakuna.Alipokuja Mwinyi,ndio akawa anaagiza mafuta kutoka Iran.

Wewe utakuwa ni kijana mdogo,huufahamu hilo.
 
Aina za crude oil zinatofautiana. Refinery huwa zinajengwa kwa kulenga aina ya crude oil, huwezi kwa mfano ukajenga refinery ya kusafisha crude oil ya Urusi ukaitumia kusafisha crude oil ya Saudi Arabia.

Na kuigeza refinery kusafisha crude nyingine ni mabilioni ya dola. Siyo kitu kidogo.
Huyu ni kijana mdogo,hajui,kipindi cha Nyerere mafuta yalipatikana kwa tabu sana.Kwa foleni,yalikuwa ya mgao,ni vituo maalumu tu,vikipata mafuta,unaweza kukuta mji mzima,ni kituo kimoja kina mafuta.Ilipelekea mpaka jumapili,gari kutembea mwisho saa 8 mchana,zaidi ya hapo mwenye gari,awe na kibali maalumu.

Ilikuwa hakuna petrol,diesel,oil,mafuta ya taa(mafuta yataa yalikuwa yakiuzwa na watu wa baiskeli,wakichukuwa nchi za jirani,wakati huo vijijini,wananchi walitumia taa za mafuta ya taa).
 
Huenda wazo lako ni sawa ila lazima tujue kwanini mwinyi aliamua kukiuwa kiwanda je unafikri huyu makamba na mama samia wanaweza kukifufua kikawa na ufanisi?

Ccm ni ile ile haijawahi kuwaga na maajabu wanaweza kukifufua then kikafa maana ccm ni ile ile haijawahi kubadilika kisera na kimtazamo.

Leo makamba atakifufua kesho Mwigulu akakiuwa
Mafuta kipindi cha awamu ya kwanza,yalikuwa shida sana,ni kwa mgao,kuanzia petrol,diesel,oil,mafuta ya taa,lami hakuna.

Mafuta yalikuwa ya mgao,ilipelekea jumapili,magari kutembea mwisho saa nane mchana,zaidi ya hapo,uwe na kibali maalumu.
 
Unachosema ni kweli.

Hadi kesho hatujui kwa nini Mwinyi alikiua kiwanda cha TIPER.
Kipindi cha awamu ya kwanza,mafuta ya petrol,diesel,oil,mafuta ya taa,yalikuwa ya mgao,yanapatikana kwa tabu.Ilipelekea mpaka jumapili,gari mwisho saa nane mchana,kutembea barabarani,zaidi ya hapo uwe na kibali.

Mwinyi,alipoingia madarakani,ndio akaagiza mafuta kwa wingi,kutoka Iran na mgao,ukaisha.Kama kufa kwa kiwanda,huwenda kilikufa kabla ya awamu ya pili.
 
Alikuwa na upeo mdogo mno
Alikuwa na upeo mkubwa Mwinyi Yeye ndio baba wa uchumi.

Hii Hali ya kuwa vitu madukani,magari kuingia nchini,biashara kushamiri,majengo makubwa na ya kisasa kujengwa,mafuta ya magari na mitambo kupatikana kwa wingi,mashule binafsi,hospital binafsi,nk ni yeye aliruhusu,ndio akaitwa Mzee wa Ruksa.
 
Hizo ndege na hizo SGR zinazoletwa sasa zitabaki kuwa mali halali ya nchi hii.

Ni afadhali tumeweza kuimiliki hiyo miradi mapema maana imagine siku zijazo na hali ya uchumi wa Dunia unavyoenda halafu utafakari bei na gharama zake kama zitashikika kwa nchi kama hii?

Huko mbeleni italazimika kuwa na mbia wa kizungu toka ubeberuni ndio tuweze kuimudu.

Wazo lako zuri ila tatizo ni usomi wa kibongo wa weledi wa kuchambua bila kutekeleza.
Au kuja na njia mbadala
Ya ufumbuzi.

Bomba la Uganda bado ni kitegauchumi kwa nchi yetu kama mnufaika wa malipo ya kila ujazo wa Crude oil itakayphudumiwa nalo.

Tatizo bado litabaki kwetu na ubadhirifu wetu wa kula urefu wa kamba.

Kosa la mwinyi ni kukubali ushauri mbovu toka kwa waliokuwa na nia mbaya,bila ya yeye kujua.

Kama ilivyo sasa kwa mama na Msoga team ya makamba .

JPM aliamua the other way round!
Bila Mwinyi,maendeleo haya unayaona,usingeyaona.Mwinyi ndio aliruhusu biashara,ujenzi wa majumba makubwa kisasa,mafuta ya petrol,diesel,oil,mafuta ya taa,kuingia nchini.

Magari na spare kuingia nchini,nk.Awamu ya kwanza,mafuta yalikuwa ya mgao,mji mzima unaweza ukakuta ,ni kituo kimoja tu,ndio kinamafuta,tena unauziwa kwa mgao,kama imepangwa mwisho kuuziwa mtu,ni lita 5,huwezi kuzidisha hapo.
 
Kipindi cha awamu ya kwanza,mafuta ya petrol,diesel,oil,mafuta ya taa,yalikuwa ya mgao,yanapatikana kwa tabu.Ilipelekea mpaka jumapili,gari mwisho saa nane mchana,kutembea barabarani,zaidi ya hapo uwe na kibali.
Mwinyi,alipoingia madarakani,ndio akaagiza mafuta kwa wingi,kutoka Iran na mgao,ukaisha.Kama kufa kwa kiwanda,huwenda kilikufa kabla ya awamu ya pili.
Ni kweli lakini kulikuwa na mismanagement ya hali ya juu hasa baada ya vita ya Kagera.

Kabla ya vita, miaka ya 60 mambo yalikuwa mazuri tu.
 
Kipindi hicho unachokitaka cha Nyerere,mafuta yalikuwa kwa foleni, mafuta ya mgao,,hayapatikani,kutokana na ukosefu wa mafuta,oil ilikuwa kupata tabu,lami hakuna.Alipokuja Mwinyi,ndio akawa anaagiza mafuta kutoka Iran.
Wewe utakuwa ni kijana mdogo,huufahamu hilo.
Wewe umezaliwa miaka ya Azimio la Arusha, sisi long time miaka ya Edward Twining na Richard Turnbull, na nina hakika humju yeyote kati ya hao.
Tunajua maisha ya nchi hii bana!
 
Kigamboni mbona maeneo ni plenty?, kwanini amege eneo la yeyote?, kwa Zambia, tuna TAZAMA Pipeline, na wana matenki ya kutosha kwa uwezo wa ile line, unless kama ni increased demand hivyo they need increased supply na increased storage.

Sidhani kama aliuponda, bali mpango mkakati wa upanuzi wa Bandari ya Sar Port, tunatenga storage za kufa mtu pale Kurasini, hivyo Kigamboni watasubiri.

Msikiliza kwa makini Januari hapo, utaijua angle yake

Its true JPM hakuwa mwanasiasa wa politicking, he was a doer, maneno mafupi, vitendo virefu, he had a vision ya Tanzania anayoitaka, and mission to accomplish, but tatizo ni yale mambo yake mengine... kwenye hayo, naomba tumwache marehemu apumzike kwa amani.

I'd like to differ, you just sit and watch!.
Kuna wengi wanadhani wanamfahamu January, lakini sii kweli, wengi wanamfahamu January kijuu juu tu, kwa kuwasaidia kumfahamu vizuri January, karibu mitaa hii
P
Heb nitajie jambo moja ambalo January alisha accomplish ambalo unaweza kusema hili lina mdifine, hili ni symbol yake, hili ni Legacy yake ukiacha bao lao la mkono...

The guy is a pure politician, maneno meeengi vitendo sifuri, I bet ndicho watanzania mnapenda kuskia( nice empty words)...nenda jimboni kwake, sometime mtu unawaza hua anapitaje huyu?
He is good at talking, and probably ana kismati km cha JK bt he is just full of promises bt result hazionekani...

Show me his works and i will show you tens of his empty words.

NB: unapo attach video za maneno yake, please attach na video za accomplishment zake, empty words simply doesnt cut with me.

Issue ya bi mkubwa kuponda huo mradi nadhani its better ukaachana na hisia ukaskiliza hotuba yake.

Issue ya kwann alimega hilo swali anajua yy ya watu wa Tazama(You can verify this info na watu wa tazama) maana aligawa eneo lao akawapa Tiper ili nao wajenge tanks zao baada ya kuona project proporsal ya wazambia ..

I have Just confirmed kua Zambia wameshaanza ujenzi wa addional tanks though baada ya raisi mpya kuingia ulisimama kwa muda coz ya rushwa.
Link: Red flag against Dalbit’s highly inflated Tazama tank farm project.
 
...kuna eneo kigamboni walitengwa wa Zambia kwa ajili ya kuweka storage yao ya mafuta, JPM baada ya kuskia Zambia wanataka kujenga Storage tanks zako na ss tunanang'aa macho akalimega lile eneo ili na sisi tuwe na storage yetu pale...

Zambia walishapata mkandarasi wa kujenga though mchakato umesimamishwa...on our side tuliua kwenye mchakato wa awali bt hapa katikati ukafa a natural death hasa baada ya bi mkubwa kuuponda huo mradi kwenye ufunguzi wa Gati za Bandari...
Am not sure Makamba ana come from which angle...

JPM hakua Mwanasiasa mzuri bt he had visions...From Reli, Bandari ya Tanga down to Mtwara to those Fuel storage facilities u can see this guy kuna kitu alikua anataka ku achieve...

With January is doubt....he is not a doer, ni mwanasiasa, maneno maneno mengiiii, bt utendaji na ku deliver ni almost hakuna kitu
JPM hakuwa na vision yoyote bali kufaidisha miradi ya kwao tu.

TAZARA ( 1800km to Dar port) ipo pale hajatia hata neno.

Majuzi Angola wamaiendelza Benguela Railway(1400km to port) kwenda Lobito Port.

Zambia tutawasikia kwenye bomba kwa sababu ya mkabila na mtu asiyeona mbali mmoja.
 
Heb nitajie jambo moja ambalo January alisha accomplish ambalo unaweza kusema hili lina mdifine, hili ni symbol yake, hili ni Legacy yake ukiacha bao lao la mkono...

The guy is a pure politician, maneno meeengi vitendo sifuri, I bet ndicho watanzania mnapenda kuskia( nice empty words)...nenda jimboni kwake, sometime mtu unawaza hua anapitaje huyu?
He is good at talking, and probably ana kismati km cha JK bt he is just full of promises bt result hazionekani...

Show me his works and i will show you tens of his empty words.
NB: unapo attach video za maneno yake, please attach na video za accomplishment zake, empty words simply doesnt cut with me.
"Nice empty words" umeuwa ndugu
 
Heb nitajie jambo moja ambalo January alisha accomplish ambalo unaweza kusema hili lina mdifine, hili ni symbol yake, hili ni Legacy yake ukiacha bao lao la mkono...

The guy is a pure politician, maneno meeengi vitendo sifuri, I bet ndicho watanzania mnapenda kuskia( nice empty words)...nenda jimboni kwake, sometime mtu unawaza hua anapitaje huyu?
He is good at talking, and probably ana kismati km cha JK bt he is just full of promises bt result hazionekani...

Show me his works and i will show you tens of his empty words.

NB: unapo attach video za maneno yake, please attach na video za accomplishment zake, empty words simply doesnt cut with me.

Issue ya bi mkubwa kuponda huo mradi nadhani its better ukaachana na hisia ukaskiliza hotuba yake.

Issue ya kwann alimega hilo swali anajua yy ya watu wa Tazama(You can verify this info na watu wa tazama) maana aligawa eneo lao akawapa Tiper ili nao wajenge tanks zao baada ya kuona project proporsal ya wazambia ..

I have Just confirmed kua Zambia wameshaanza ujenzi wa addional tanks though baada ya raisi mpya kuingia ulisimama kwa muda coz ya rushwa.
Link: Red flag against Dalbit’s highly inflated Tazama tank farm project.
Kwa vile mimi ni just an AV Digital producer na sio archivest, ngoja nianze compilation ya his achievements, kisha nikurudie
 
JPM hakuwa na vision yoyote bali kufaidisha miradi ya kwao tu.
TAZARA ( 1800km to Dar port) ipo pale hajatia hata neno.
Majuzi Angola wamaiendelza Benguela Railway(1400km to port) kwenda Lobito Port.
Zambia tutawasikia kwenye bomba kwa sababu ya mkabila na mtu asiyeona mbali mmoja.
I bet hujui ht maana ya vision...

Ulitaka afanye nn na Tazara while hio reli ni co-owned...au ht hilo ulikua hujui...any decision regarding Tazara lazima inchi zote mbili zikubaliane sio maamuzi binafsi ya Raisi, wasipokubaliana wanabaki kwenye endless loop...kifupi Tazara ni km Nyumba ya urithi kariakoo, mmoja anaweza kutaka kupaka rangi mwingine akagoma..[emoji1787][emoji1787]

Untill hio reli itakapokuja kua na management mbili zinazojitegemea na kila inchi ku manage kipande chake nothing will ever change period.
 
Kwa vile mimi ni just an AV Digital producer na sio archivest, ngoja nianze compilation ya his achievements, kisha nikurudie
Sawa bro na kusubiri kwa hamu sana,

Na kwakua mi ni mtaalam wa mifumo I will crawl the entire internet for all the NICE EMPTY PROMISES he has ever given anywhere and everywhere, then ntawashirikisha na watu wa jimboni kwake kupata na mengineyo to sum up.

Ukiwa teyari please let me know...

This challenge gona be funny.
 
Tipper sio ifufuliwe tu,ila inabidi ifungwe mitambo mipya na mikubwa ya kukidhi mahitaji yetu na labda majirani.

Ile Tipper ya zamani ilikuwa na Refinery ndogo mno na mitambo ilikuwa imechakaa mno,kwa sasa ni scrap and outdated.

Pili jambo la msingi ni kujenga storage tanks zenye ujazo mkubwa wa kuhifadhi mafuta ghafi na mafuta yaliosafishwa, kulingana na matumizi ya nchi yetu angalau miezi 6.

Mwenye storage tank capacities kubwa ndio mfalme wa leo kwenye medani ya mafuta.

Hivi vikampuni vya mafuta vilivyoshahimiri nchi nzima hawana storage tanks kubwa,inabidi zijengwe pia Depots za mafuta kanda ya kaskazini,Kanda ya Kusini,Kanda ya magharibi na Kanda ya Ziwa.

Biashara ya mafuta ni yenye ushindani na yenye umakini katika kuweka maamuzi yaliyo salama kwa mazingira,salama kwa mitambo na mazao yake lakini zaidi salama kwa watu.

Tusije kuwekeza pesa zote hizo tukawapa wajinga na walafi watuendeshe Tipper mpya.
Hayo chini ya utawala wa awamu ya 4B hayawezekani😂😂😂 huu utawala ni wa kuiba kwa nafasi uliopo
 
Hayo chini ya utawala wa awamu ya 4B hayawezekani[emoji23][emoji23][emoji23] huu utawala ni wa kuiba kwa nafasi uliopo
Tumerudi kua wanasiasa..maneno meeengi vitendo sifuri...

Inaonekana maneno matam tam ndo watanzania wanapenda, they make us feel better, and sleep better at night ht km tunajua kukikucha nothing positive will come out of it.
 
Wewe umezaliwa miaka ya Azimio la Arusha, sisi long time miaka ya Edward Twining na Richard Turnbull, na nina hakika humju yeyote kati ya hao.
Tunajua maisha ya nchi hii bana!
Hujui chochote,kijana wajuzi.

Nyerere hakuwa mbaguzi wa Rangi,kabila,dini.

Na alisaidia sana ukombozi wa nchi za Afrika na zisizo za Afrika,kama wapalestina.
 
Back
Top Bottom