Waziri Makamba, nakushauri kuwa 'strategic thinker' suala la mafuta. Fufueni TIPER

Waziri Makamba, nakushauri kuwa 'strategic thinker' suala la mafuta. Fufueni TIPER

Ili andiko lako liwe zuri zaidi naomba kama unaweza ukatafuta na haya:-
Cost ya kufanya refinery (na hapa usiweke hata capital cost tunaweza kujibana na kufanya investment) weka operation cost n.k.
Difference ya kununua already refined na kurefine hapa ni kiasi gani...

Hizo addictives tutakazopata je zitaoffset gharama ya refinery ?

Je kwa nchi yenye gas pia tunaonaje kupunguza matumizi ya petroleum (ambayo inabidi tuagize) na kutumia Compressed Natural Gas wherever Possible kwenye magari na viwandani kwenda full gas / electricity ?

Tunaonaje kuhusu kumalizia lile Bwawa la Nyerere as soon as possible ili umeme viwandani na majumbani katika kupikia na shughuli zingine usitegemee gesi ?

All in all Kupanga ni Kuchagua and its all about Opportunity Cost
 
Mku wewe una akili za kukariri lakini thinking capacity ni very low.
Elewa kwanza maudhui ya mada na urudi na mawazo endelevu.
Ni ufinyu wa mawazo kutegemea TOTAL, mfanya biashara ya mafuta akujengee refinery, atakula wapi?
Wewe ndiyo hujamwelewa mwenzako.

Badala ya kumuona ana akili finyu za kukariri, I thought ungemtaka athibitishe iwapo kweli TIPPER ilishanunuliwa na TOTAL

Au wewe mwambie kuwa si kweli kuwa TIPPER ilishauzwa na serikali kubaki na share kidogo sana kiasi cha kukosa uhalali wa umiliki wa shirika hilo

Halafu from there, muendelee kujadiliana kwa hoja pasipo kukwazana kwa kuitana majina

Kwa sababu kama serikali si mmliki wa TIPPER, basi ina maana hata hoja yako inakosa nguvu na automatic inakufa kifo cha kawaida na hoja ya Bondpost inakuwa na nguvu

By the way, tunarudi palepale kuwa SERA na MIPANGO ya serikali ambayo chanzo chake ni mifumo mibovu ya utawala wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yetu!!
 
Hajasema, ila ni kuunga mkono hoja yako, kwenye baadhi ya mipango yetu ya maendeleo, we are not strategic, tunakimbilia kununua midege mikubwa kwa cash, bila business, midege imefika sasa ndio tunatengeneza business plan!.
Tunakimbilia kujenga SGR, huku hatuna port ya kuifeed SGR ika operate kwa faida !. Sasa tuna bomba la mafuta la Uganda, ni ajabu sana kama mafuta ya Uganda, yatapita kwetu, halafu sisi tukaendelea kufuata mafuta Arabuni!.
Hili nimelizungumza.
na asante kuchangia.
P
Hizo ndege na hizo SGR zinazoletwa sasa zitabaki kuwa mali halali ya nchi hii.

Ni afadhali tumeweza kuimiliki hiyo miradi mapema maana imagine siku zijazo na hali ya uchumi wa Dunia unavyoenda halafu utafakari bei na gharama zake kama zitashikika kwa nchi kama hii?

Huko mbeleni italazimika kuwa na mbia wa kizungu toka ubeberuni ndio tuweze kuimudu.

Wazo lako zuri ila tatizo ni usomi wa kibongo wa weledi wa kuchambua bila kutekeleza.
Au kuja na njia mbadala
Ya ufumbuzi.

Bomba la Uganda bado ni kitegauchumi kwa nchi yetu kama mnufaika wa malipo ya kila ujazo wa Crude oil itakayphudumiwa nalo.

Tatizo bado litabaki kwetu na ubadhirifu wetu wa kula urefu wa kamba.

Kosa la mwinyi ni kukubali ushauri mbovu toka kwa waliokuwa na nia mbaya,bila ya yeye kujua.

Kama ilivyo sasa kwa mama na Msoga team ya makamba .

JPM aliamua the other way round!
 
Narudia tena, shida si Makamba. Tatizo ni la KISERA na mfumo mzima wa UTAWALA
Mkuu hapa umemaliza, tunakwenda mbele hatua 5 then tunarudi nyuma hatua 10- fucus & direction hakuna, haijulikani hadi leo tunataka kufika wapi - ni mwendo wa kupapasa.

Sera pamoja na mwendelezo wake kwa awamu za uongozi ndiyo tatizo kubwa. Kiongozi akiongoka anaondoka nazo, akija mwingine anaanza na mpya anazoona yeye zinafaa.
 
Hajasema, ila ni kuunga mkono hoja yako, kwenye baadhi ya mipango yetu ya maendeleo, we are not strategic, tunakimbilia kununua midege mikubwa kwa cash, bila business, midege imefika sasa ndio tunatengeneza business plan!.
Tunakimbilia kujenga SGR, huku hatuna port ya kuifeed SGR ika operate kwa faida !. Sasa tuna bomba la mafuta la Uganda, ni ajabu sana kama mafuta ya Uganda, yatapita kwetu, halafu sisi tukaendelea kufuata mafuta Arabuni!.
Hili nimelizungumza.
na asante kuchangia.
P
Je lifespan ya hayo mafuta ya Uganda yatafaa kuanzisha refinery?
 
Umeongea bonge la point. Tatizo hawa viongozi wanaotuongoza sijajua wanatoa maamuzi wapi au sijui wanafikiria tanzania ipi hawana uzalendo kabisa yaani wanawanufaisha wafanyabiashara kwa kupewa rushwa.
Wewe naye kachukue hiyo rushwa
 
Ili andiko lako liwe zuri zaidi naomba kama unaweza ukatafuta na haya:-
Cost ya kufanya refinery (na hapa usiweke hata capital cost tunaweza kujibana na kufanya investment) weka operation cost n.k.
Difference ya kununua already refined na kurefine hapa ni kiasi gani...

Hizo addictives tutakazopata je zitaoffset gharama ya refinery ?

Je kwa nchi yenye gas pia tunaonaje kupunguza matumizi ya petroleum (ambayo inabidi tuagize) na kutumia Compressed Natural Gas wherever Possible kwenye magari na viwandani kwenda full gas / electricity ?

Tunaonaje kuhusu kumalizia lile Bwawa la Nyerere as soon as possible ili umeme viwandani na majumbani katika kupikia na shughuli zingine usitegemee gesi ?

All in all Kupanga ni Kuchagua and its all about Opportunity Cost
Household nyingi hutumia gesi kupikia na heating, umeme hutumika kwenye lighting na kuendesha vifaa vya umeme
 
Household nyingi hutumia gesi kupikia na heating, umeme hutumika kwenye lighting na kuendesha vifaa vya umeme
Because its cheaper...,

Ila kama kuna Bwana la HEP (la kuzalisha watts mpaka za kumwaga) na gesi inayotumiwa sio Piped Natural bali ni LPG hapo nina uhakika Electricity itakuwa Cheaper..., Kwa wale vijana ambao sio wa leo nadhani watafahamu kwamba kuna wakati ule Bulbs za watts 100, watu walikuwa wanaziwasha nje kama nne na bado mtu ana oven na electric cooker na bado watu walikuwa wanasahau hata kuzima taa WHY because electricity was Cheaper
 
Pamoja umenitukana nadhani ni sababu ya hayo uliyoyasema dhidi yangu kumbe ni wewe ndio unajisema .

Ungeelewa nilichomaanisha wala usingeandika hayo maana I'm saying what you are saying labda sababu sikuandika kwa lugha nyepesi Kama yako.

Anyway nimekusamehe sababu ya ujuaji wako lakini mie nilikuwa part ya negotiations na hayo unayosema ndio ugumu uliopo labda utaelewa niliandika hivi.
Mkuu sikukutukana bali kwenda straight to the burning point.

Na hili ndilo tatizo kubwa la watendaji wengi serikalini.

Wana ukomalia utaratibu bila kufikiria sana the desired results.

Waswahili wa kule majuu huwa wanasema .." the end must justify the means."

Wengi wa wenzetu serikalini kuanzia hata wale wa juu kabisa wanamkomalia the messenger badala ya message yenyewe.

Utaratibu wa kuuza na ubinafsishaji wa sekta ya umma haikutilia sana mustakabali wa Taifa kimkakati.

Na ndio maana TIPER iliyoanzishwa na Tanzania na Italy chini ya baba wa Taifa ilipanguliwa utafikiri waliofanya hivyo hawakujua madhara yake.
 
Lengo na mkakati wa Tanzania kuwa kutuo kikubwa cha usambazaji mafuta, ni kuua lile bomba toka Uganda,

Fikiria mafuta ya toka uarabuni yanajazwa kwetu pwani kwa wingi ili yasambazwe Africa Mashariki na kati, Mganda anataka kusafirisha tu- mafuta twake kuja Tanga - unafikiri anaweza kushindana na mafuta ya Waarabu!

Time will tell.

Halafu mafuta hayatahifadhiwa pwani tu, yatahifadhiwa hata ndani kabisa ya bara. labda tutakuja na mkakati wa kuzuia magari ya mafuta yasipimwe kwenye mizani kwani haina maana yoyote kwani yatakuwa yanakwenda kuhifadhiwa tu.

Mafuta hayo yaliyohifadhiwa kwenye maeneo mengi yatakapouzwa ndani ya nchi nani atajua?

Tushangilie kidogo, naona kama tunaenda kupigwa
 
Mitambo ya TIPER yote imetolewa na kuuzwa scrapper...tiper ni storage tu na sasa wanaload mafuta
 
Makamba ajitafakari sana....

Ni kweli tunafahamu anakula kutokana na urefu wa kamba yake, lakini ajitahidi kupiga kazi kwa bidii..
 
Hii ni argument ya mtu aliyeshindwa kufikiri.

Hivyo inabidi asaidiwe all options.
Haya saidia jinsi ya kupata hiyo 10 billion USD (16% ya GDP) ya kujenga refinery. Tena hiyo ni low end estimation, gharama ya kweli inaweza kuzidi hapo.

Utapata wapi huo mkopo? Au utajibana wapi ili utumie kipato cha taifa kwenye huo mradi?
 
Haya saidia jinsi ya kupata hiyo 10 billion USD (16% ya GDP) ya kujenga refinery. Tena hiyo ni low end estimation, gharama ya kweli inaweza kuzidi hapo. Utapata wapi huo mkopo? Au utajibana wapi ili utumie kipato cha taifa kwenye huo mradi?
Hela za kujenga Nyerere Hydro Power Plant na SGR tumepata wapi?

Lazima kuthink forward.
 
Nimeona luninga Waziri Makamba akitamba kuwa Tanzania itafanywa kuwa kituo kikubwa cha usambazaji mafuta.

Mimi nikifikiri serikali itafufua kiwanda cha refinery cha TIPER, kumbe sivyo.

TIPER, Tanzania Italian Petroleum Refinery, ilianzishwa na Mwalimu Nyerere kama strategic plant around 1965.

Serikali ya Awamu ya pili chini ya Rais Mwinyi ilifanya KOSA KUBWA kuua kiwanda cha TIPER.

Katika kiwanda hiki nchi ililuwa ikiagiza tu crude oil, a one off operation.

Katika crude oil baada ya ku refine na kudistill hiyo crude oil, utapata mafuta aina zote hadi lami na mafuta ya vaseline.

Kilichotokea wakati wa Mwinyi kwa hakika ni cha kulaumiwa maana haieleweki kwanini tuagize finished product badala ya kuagiza malighafi ambayo itatoa mafuta aina zote na bidhaa nyingi za ziada.

Lami iliyokuwa inapatikana kama by product sasa hivi wanafaidishwa wafanyabiashara wakubwa kwa gharama za usafiri.

J Makamba, be strategic.
Huyu kipara ngoto anaongozwa na maslahi binafsi. Kenya hadi leo wana refinery yao sisi tukazugwa tukaua yakwetu.

Kwa uhakika high on the agenda ingekua kujenga refinery Tanga ambapo bomba la mafuta ya uganda ndio terminal. Kwa hivyo tungenunua crude ya uganda na kurefine kwa matunizi yetu.

Ukisema unataka kua kituo kikubwa cha usambazaji kwa nchi jirani una hakika gani wao watakubali kua soko lako.

Kuna risk kwa hivyo hiyo fulsa inaweza wala isinunulike na wafanya biashara.
 
Back
Top Bottom