Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye, Paul Makonda, amefanya ziara ya kikazi nchini Hispania ambapo ametembelea Jiji la Barcelona na kukutana ana kwa ana na nyota kijana wa mpira wa miguu duniani na klabu ya FC Barcelona, Lamine Yamal.
Ziara hiyo ya kiserikali imefanyika wiki hii jijini Barcelona, Hispania. Katika ziara hiyo, Waziri Makonda alitembelea makao makuu ya klabu ya FC Barcelona pamoja na viwanja vyake vya mazoezi, ambapo alipata fursa ya kufanya mazungumzo na mchezaji huyo anayekipiga katika timu ya taifa ya Hispania na FC Barcelona.
Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kuimarisha diplomasia ya michezo, kuhamasisha maendeleo ya soka la vijana nchini Tanzania, pamoja na kumwalika rasmi Lamine Yamal kuitembelea Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha utalii na kutoa chachu kwa chipukizi wa michezo nchini.
Katika mazungumzo yao, Waziri Makonda alimpongeza Yamal kwa viwango vya juu anavyovionyesha uwanjani na mchango wake katika kuwavutia vijana wengi barani Afrika na duniani kote.
Kwa upande wake, Yamal alieleza furaha yake kukutana na Waziri huyo wa Michezo kutoka Tanzania na kuonyesha nia ya kuunga mkono juhudi za kukuza vipaji vya soka miongoni mwa vijana. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kubadilishana zawadi za ukumbusho na picha za pamoja.