Pepe Madochi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 601
- 816
Sasa janja wa 19 anathamani gani kwa taifa letu ??? 😖
Mimi pia nimeshangaa sanaa 😊 ☺️ 😁Yaani Yamal ni mrefu kuliko makonda!
Forwhat purpose?.. ndo maana pesa inazidi kua ngumuWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye, Paul Makonda, amefanya ziara ya kikazi nchini Hispania ambapo ametembelea Jiji la Barcelona na kukutana ana kwa ana na nyota kijana wa mpira wa miguu duniani na klabu ya FC Barcelona, Lamine Yamal.
Ziara hiyo ya kiserikali imefanyika wiki hii jijini Barcelona, Hispania. Katika ziara hiyo, Waziri Makonda alitembelea makao makuu ya klabu ya FC Barcelona pamoja na viwanja vyake vya mazoezi, ambapo alipata fursa ya kufanya mazungumzo na mchezaji huyo anayekipiga katika timu ya taifa ya Hispania na FC Barcelona.
Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kuimarisha diplomasia ya michezo, kuhamasisha maendeleo ya soka la vijana nchini Tanzania, pamoja na kumwalika rasmi Lamine Yamal kuitembelea Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha utalii na kutoa chachu kwa chipukizi wa michezo nchini.
Katika mazungumzo yao, Waziri Makonda alimpongeza Yamal kwa viwango vya juu anavyovionyesha uwanjani na mchango wake katika kuwavutia vijana wengi barani Afrika na duniani kote.
Kwa upande wake, Yamal alieleza furaha yake kukutana na Waziri huyo wa Michezo kutoka Tanzania na kuonyesha nia ya kuunga mkono juhudi za kukuza vipaji vya soka miongoni mwa vijana. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kubadilishana zawadi za ukumbusho na picha za pamoja.
Mimi ningemwambia yamal avae nguo vizuriIla umri wa ma teenagers bana. Sasa huo ndo uvaaji gani wa Lamine?
Amevaa kama Mzee Nambuo Ndeshau wa pale Mashati.
Umeelewa code au unafurahia kumuona tu ?
Ila hii inji dahh!!
Sasa janja wa 19 anathamani gani kwa taifa letu ??? 😖
Soma hiyooooo!Yamal ni professional footballer kwa kizazi hiki cha gen Z
Amtafute yule Rais wa Liberia (Sierra Leone?)aliyeingia madarakani akiwa na miaka 25,akakae naye ampe uzoefu wa kutanguliza ujinga mbele.Bashite kula bata mpk kuku waone wivu. Na pia hakuna w kukugusa kijana pendwa.
Kazi ni kipimo cha utu
Hasara kubwa sana. Na hawajali wala nini.Hii ni hasara kwa Taifa aiseeeee
Mtu kutoka Tanganyika anayekatisha uhai wa wenzake kisa tofauti za kimitizamo kisiasa/ideologies ndiyo katembelea Ulaya/Spaniards!
Msukuma Alisema Tanzania Yote Barabara Ni MahandakiNaona Ile bajeti iliyotengwa kwaajili ya safari za watawala kwenda nje ya Nchi kiasi Cha Trilioni 1.2 inafanya kazi
Huku miradi ya barabara na Maji ikiwa imesimama kwa kukosa fedha 🙌
Endelea kusikia hivyo hivyoLamine nasikia ni shoga