Waziri Masauni ameonya watu au vikundi vya watu ambavyo vinatumia uhuru wa kutoa maoni kutoa kauli za uchochezi

Wewe unamsikiliza Masauni kweli? Hawa wazanzibar ni wanafiki sana! Juu ujinga hatutakubali Watanganyika! Ndo maana alipoingia tu Samia akamteua Mzanzibari Mbarawa kuwa waziri lengo ni kuuza bandari!
 
Si
Sisi wananchi hatuvumilii serikali isiyo na uzalendo.
 
Asitishe watu hii nchi sio ya ukoo wake, cheo ni dhamana tu anaweza futika hata kesho akaja mwingine
 
..Wazanzibari kama Othman Masoud, Juma Duni, Ismail Jussa,.wakiukosoa muungano hatusikii wakitishiwa na Bwana Masauni.

..Watanganyika wakikosoa muungano ndipo Bwana Masauni anajitokeza kuelekeza vyombo vya dola dhidi yao.
Kwani wewe hujui ni kwa nini inakua hivo?
 
Hawezi kuwambia kitu wazanzibari hao uliowataja kwa sababu hayo wanayoyasema yote kuhusu Muungano niyakweli
 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametoa onyo kali kwa watu wanaotumia uhuru wa kutoa maoni vibaya kwa lengo la kuhatarisha usalama na kuleta mpasuko kwa taifa.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuibuka baadhi ya watu hususani wanasiasa kutumia majukwaa yao kutoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani vyenye kuleta mgawanyiko nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kindondoni Shamba iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa tawi katika kata hiyo lililopo Chuo Kikuu Huria.

"Ninalielekeza jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha havimfumbii macho mtu yeyote au kikundi chochote kitakachopelekea kwa vitendo au kwa kauli katika kuvunja sheria za nchi yetu na kuhatarisha usalama wa nchi hii"_ Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni

"Katika nchi hii kama kuna chama kinachosifika katika ujenzi na misingi ya umoja na mshikamano na amani ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ndiyo kina dhamana ya kuiongoza Serikali, na Serikali hii inayo jukumu la kuhakikisha nchi inabaki kuwa salama na kuwa moja kwa kudumisha umoja na mshikamano, vyama vingine havina jukumu hilo"_Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni

JAMBO TV
 
Kwan watoa maoni hasa LISSU hajui katiba inasemaje? Au ndo ile kauli ya... Kosoeni kwa staha 🀣🀣🀣. Politics is jus a bad playground tuishi humo kikubwa mtu asivunje sheria tu!!!
 
Kwan watoa maoni hasa LISSU hajui katiba inasemaje? Au ndo ile kauli ya... Kosoeni kwa staha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Politics is jus a bad playground tuishi humo kikubwa mtu asivunje sheria tu!!!
Nyie wazanzibar mmeuza bandari zetu then tunawaambia ukweli badala ya kurekebisha mnatutisha haikubaliki

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…