Waziri Mbarawa: Tutajenga barabara ya njia 4, Dar-Moro, ili upite lazima ulipie

Mheshimiwa waziri kuanzia ubungu hadi kimara mwisho ile njia inahitaji kupanuliwa haraka saana.Ile goleni iliyokuwepo pale ubungo imehamia kimara koregwe hadi kimara mwisho.

Hii njia ndio njia kuu ya nchi na usitegemee bamdari yetu kuwa na tija kwa uwepo wa barabara ya aina iliyopo kuanzia ubungo hadi kimara Mwisho
 
Huu Mradi utakuwa na maana kama mkandarasi atakuwa ni wa hapa hapa Tanzania.

Kama akiwa wa nje maana yake tuna export pesa
 
Wanataka kusumbua wananchi kama wanavyosumbuliwa wa kigamboni?kwa nini huo mradi usijengwe na serikali?pesa zipo nyingi tu lakini mnashindwa kuzisimamia.Banane mianya ya wizi hasa wizara ya madini pesa zinaibiwa njenje kuliko kuweka mradi utakaokuwa kero kwa wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame M. Mbarawa ametangaza mkakati wa ujenzi wa barabara mpya kwa kushirikiana...
Hii sawa!

agalia wenzetu Bangkok, hiyo ya kulia unalipia, unapita juu kwa juu mpaka Airport toka Rama (toka Rama 9 Road
 

Idiotic proposal, you build the Project with taxpayer’s money, still the Road is used segragatively,
 
Huu Mradi utakuwa na maana kama mkandarasi atakuwa ni wa hapa hapa Tanzania.

Kama akiwa wa nje maana yake tuna export pesa

Mkandarasi yoyote yule alazimishwe kufungua account za bank katika taifa ili na malipo yalipwe kwa njia ya Tanzania shilingi. Pia wafungue ofisi bongo au headquarters ndogo itakayo toa ajira professional na un professional
 
Habari ndio hiyo 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221109-142751.png
    174.8 KB · Views: 3
Kwa nini iwe hadi Morogoro tu?.... Miundombinu ya aina hii kwa umuhimu wake ilipaswa ilengwe kufika angalau Dodoma kwa kuanzia. Kiuhalisia nchi hii inahitaji "Express ways" kati ya mikoa na mikoa au kanda kwa kanda na zile zinazo unganisha nchi kwa nchi. Hii ni miundombinu ya kasi kubwa mbali na hizi barabara unganishi tulizo nazo sasa na zile zilizoko kwenye hatua ya ujenzi sasa.

Barabara ya sasa inayounganisha Morogoro na Dodoma ni nyembamba sana, Ile ya Chalinze hadi Himo ndio kabisa!!. Hatujachelewa tuanze sasa kujenga miundombinu imara, inayopendeza na yenye ubunifu kwa miaka 100. Hii mambo ya kujenga barabara zisizonyooka iwe kwa urefu au kupanda milima na kushuka tuaachane nayo, palipo na bonde lijazwe kifusi na pale penye milima "tunnels" zichorongwe tu! gharama zitarudishwa kupitia "Road Tolls"...🙏
🙏🙏🙏
 
Kodi tulipie na kupata huduma tunalipia hii nchi CCM wameshindwa kuingiza
Kodi finyu hazitufikishi kokote zitatufanya tuendeleee kuwa masikini
Hili lililotangazwa litafanya nchi hii iwe na maendeleo in five years tutakuwa mbali mno serikali itenge sera nzuri uchumi na kutengeneza hela waachiwe sekta binafsi wafanye kwa mkakati huo itakusanya kodi maradufu na pia itawezesha wananchi kuumiliki uchumi na sio serikali pigia mfano tu mitandao ya simu kama mpaka leo ingekuwa ni ttcl tu mitandao ingekuwa imefika vijijini ???
Au ingekuwa ni RTD hadi leo bongo fleva ingekuwa na kuzalisha akina diamond tunahitaji sekta binafsi ikue na ibebe uchumi na serikali kazi yake kusimamia game kama refa na kuhakikisha sheria zinafuatwa mambo ya serikali kujenga viwanda hii ni mambo ya mwaka 47 hio kazi ya wananchi wawezeshwe wafanye nchi iwe na matajiri walipa kodi wakubwa waongezeke sio wachache kama sasa .
 
Nchi ina viongozi wa ajabu sana hii. Miaka yote mnafanya ziara huko nje mnaenda kushangaashangaa tu na kujifanyia shopping, leo mnazinduka ndiyo mnajua kuna kitu kinaitwa "Express Way". Na hii najua mtaipa majina yenu kama vile mmejenga kwa pesa zenu.

Toka mwanzo, njia zote kuu za barabara za kuunganisha mikoa zilitakuwa kuwa na njia zisizopungua tatu, na kizingiti kutenganisha pande mbili. Badala yake mkaamua kujenga vibarabara vyembamba vilivyoua mamia kama siyo maelfu ya Watanzania mpaka sasa.

Eti express way ya njia mbili mbili. Hiyo bado ni local road.
 
Angekuwa yule jamaa korofi korofi marehemu ningemuelewa maana jamaa lilikuwa likisema nafanya A,b,c basi balaa linaanza hapo hapo hata kama kuna watu watalala njaa na kufa.
 
Acheni akili za kimaskini. mmeshakariri kila kitu kifanywe na serikali ndo mana nchi inachelewa kupata maendeleo. inawezekana sekta binafsi wakajenga miundombinu na maisha yakawa safi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…