Waziri Mbarawa: Tutajenga barabara ya njia 4, Dar-Moro, ili upite lazima ulipie

Waziri Mbarawa: Tutajenga barabara ya njia 4, Dar-Moro, ili upite lazima ulipie

Acheni akili za kimaskini. mmeshakariri kila kitu kifanywe na serikali ndo mana nchi inachelewa kupata maendeleo. inawezekana sekta binafsi wakajenga miundombinu na maisha yakawa safi kabisa
CCM mna shida gani? Mkiambiwaga serikali isiingie kwenye biashara, huwa mnang'aka na kujisifu kuwa 'mmetekeleza' na mwisho wa siku hizo biashara zenu zinaendaga kupata hasara na kutoa huduma mbovu.

Leo mnazinduka ndiyo mnajua sekta binafsi inaweza kufanya miradi mikubwa na kuwaona wanaowapinga hawana akili. Kesho tena akija mwingine na maujinga yake atapiga vita sekta binafsi na mtaendelea kusifu na kuabudu.
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame M. Mbarawa ametangaza mkakati wa ujenzi wa barabara mpya kwa kushirikiana na sekta binafsi kutoka Dar es Salaam – Chalinde hadi Morogoro yenye urefu wa Kilometa 215 itakayojulikana kwa jina la Express way.

Barabara hiyo itakuwa ni ya kulipia pindi mtu anapohitaji kuitumia na wale ambao hawataweza kulipia watalazimika kutumia barabara ya kawaida

“Tanzania hatuna express way tangu tumepata uhuru, haya ndio maendeleo, mfano kutoka Kibaha hadi Morogoro utakuwa unaenda kilometa 120 kwa saa na hauwezi kuingia tu, kutakuwa na maeneo maalum ya interchange ndiyo yatatumika kuingia.

“Itakapofika Aprili au Mei 2023 naamini tutakuwa tumempata mkandarasi ambaye atajenga kwa fedha zake mwenyewe kisha atakuwa anakusanya fedha mradi ukikamilika, magari madogo na makubwa yatakuwa na bei tofauti.

“Wenzetu Kenya wanayo, Uganda, njia yetu itakuwa na njia nne, mbili za kwenda na mbili za kurudi, itapunguza ajali kwa kuwa mtakuwa hamkutani kama iliyo sasa.”

Profesa Mbarawa ameongeza kwa kusema: “Serikali tunakuja na utaratibu mpya wa mtu anakuja na pesa yake anajenga mradi kisha Serikali tunamlipa.

“Pia tunakuna na mabadiliko ya Sheria ili turuhusu watu waendeshe mabehewa yao, TAZARA wameshaanza kufanya hilo jambo, TRC nasi tunataka kufanya hilo jambo."
Barabara ni mali za umma kulipisha watumiaji ni WIZI
 
Back
Top Bottom