Waziri Mchengelwa aangukia pua zoezi la upandishaji madaraja watumishi wa umma, vilio vyatanda kila kona

Waziri Mchengelwa aangukia pua zoezi la upandishaji madaraja watumishi wa umma, vilio vyatanda kila kona

Utapandishe madaraja bila budget

Hivi wabongo akili zetu uwa tunaziweka wapi?

Yaani hii budget ya Magufuli ndio inaishia tarehe30 mwezi huu halafu hii hii wapachike billion 300 zitakuwa zimetoka wapi?

Tena bila bunge kuzipitisha yaani mnataka turudi kulekule kwenye kufanya kazi bila kufuata sheria?

Mama Samia kwa hili wala siwezi kumlamu mwacheni afanye kazi kwa mjibu wa sheria na katiba huwezi kupandisha watu madaraja na kuwaongeza pesa wakati pesa hazipo kwenye budget.

Tumekuwa nchi ya kulau tu kwa kila kitu bila kufanya critical thinking "
Eti critical thinking, acha usomi mzigo bwamdogo. waziri husika alisema atapandisha mwezi huu wasita!! Uwege conscious na up to date kidogo kabla ya uklitiko sinkingi wako
 
Mkuu Tuache kuichafua serikali,Mimi na mke wangu ni watu wa chini Sana huku shuleni kwetu mpigamiti-Liwale lakini tumepanda madaraja bila ya konekisheni unayoisema ,Kama Kuna watu hawjapanda madaraja Basi ni wachache Sana na ni makosa madogo madogo,

Hapa shuleni kwangu tuko walimu wanne ambao tulipaswa kupanda na wote tumepanda.
Wewe jamaa! Ubinafsi umekujaa sana, wewe watu wanalalamika halafu unajitolea mfano wewe na familiya yako! Daaa! Afrika tunayo safari ktk kifikia ukombozi wa kiuelewa
 
Waziri Mchengelwa una yapi ya kuwaambia watumishi baada ya kuwaaminisha kuwa wote wanaostahili kupanda madaraja watapandishwa na watalipwa kuanzia mwezi huu na umewaacha hewani huku idadi kubwa awaoni badiliko lolote.

Walio karibu na waziri nisaidieni kumfikishia hii
Niliwaambia wakae kwa utulivu na barua zao wakashupaza shingo ..oooh utawala mpya huu tumehakikishuwa inapanda June ... Haipungui miezi 3 mpaka kubadilika wakawa wabishi ...
 
Na hakika sn mkuu, nimefanya field utumishi mkuu, kuna wale ambao majina yao yaliingia kabla ya tarehe 10 kwenye lawson wote wamepata, mishahara huwa inapelekwa hazina kabla ya tarehe 15 ya mwezi husika mkuu, mtu jina limeingizwa kwenye lawson tarehe 20 unapataje mshahara mpya tarehe 24? tuwe na akili basi na sisi siyo kulialia, siipendi CCM lakini kwa hili hapana.
Kweli wanalia lia ndio maana jiwe aliwakomesha Sasa mama ameanza kupandisha Bado Wana lalsmika ka wachawi, ka miaka mitano hawakufa why siku 100 za mama wawe na kihoro kiasi hicho.
 
baada ya kuwaaminisha kuwa wote wanaostahili kupanda madaraja
Mbona hili darala la Manzese tunapanda bila usumbufu? Acheni kusumbua serikali. Tangu lini kupanda daraja Ikawa mpk uruhusiwe na waziri?
 
Ni wajinga sn wale, mama asiwadekeze hata kidogo
Kwa kweli hawana shukrani hawa watu, magufuli aliwafungia six year's wakaufyata mikia. Ila watanzania huwa tunajitaftia balaa kwa kulalamika na kuwa na shukrani matokeo yake tukaletewa jiwe aliyezidi mpaka wakakoma.
 
Ndo tatizo la kuweka hadharani (publicize) kila kitu ikiwemo taarifa nyeti!! Issue hii nayo ilizidi mno kusemwasemwa, yaani hakuna usiri kabisa......Luna vitu vingine inapaswa view na mipaka ya kuzunguzwa na kusikika.
 
Kudadeki zao! Hata mimi sijapandishwa eti!! Na kupambana kote kule toka enzi Rais ni Magufuli, mpaka leo bila bila!!

Ngoja na mwezi ujao waache kunipandisha ili nianze ule usumbufu wangu wa kuomba ruhusa kila siku kazini kulifuatilia hilo daraja kwenye ofisi zao.
 
Unaweza kumlaumu mchengerwa kumbe ni afisa utumishi wako hajapeleka taarifa utumishi au kachelewa kupeleka au kapeleka lakini Ina makosa mengi sasa ni vema kabla ya kumlaumu mchengerwa anza na afisa utumishi wako ili ujirishishe kama yup safi
Unaniambia mimi, au?!
 
Kipi ujaelewa mkuu kaa usome vizuri idadi kubwa ya wanaostahili kupanda wamekuta mambo tofauti sasa hapo ujaelewa kipi au we ndo mchengelwa nini unajibu thread kiaina
Wewe ndo hujaelewa! Kwani ni nani anaye-determine kwamba huyu anastahili kupanda, na yule hastahili kupanda?
 
Na hakika sn mkuu, nimefanya field utumishi mkuu, kuna wale ambao majina yao yaliingia kabla ya tarehe 10 kwenye lawson wote wamepata, mishahara huwa inapelekwa hazina kabla ya tarehe 15 ya mwezi husika mkuu, mtu jina limeingizwa kwenye lawson tarehe 20 unapataje mshahara mpya tarehe 24? tuwe na akili basi na sisi siyo kulialia, siipendi CCM lakini kwa hili hapana.
Serikali inapaswa kutoa ufafanuzi wa nini hasa kimetokea kwani si wote wanaelewa nini hasa kimetokea.
 
Mama kaanza kuwapandisha madaraja mmeanza kuchonga ngenga. Mbona wakati wa magufuli hamkuyasema .shenzi sana.
 
Kweli wanalia lia ndio maana jiwe aliwakomesha Sasa mama ameanza kupandisha Bado Wana lalsmika ka wachawi, ka miaka mitano hawakufa why siku 100 za mama wawe na kihoro kiasi hicho.
Wewe kama una chuki au una wivu,sema ila sio kutetea ujinga na ukatili wa Jiwe.
 
Back
Top Bottom