Imekua ni utamaduni kwa uongozi wa halmashauri ya ILEJE mkoani Songwe kutokuheshimu kauli za viongozi hasa wanapotaka watumishi walipwe stahiki zao.
Ziara ya waziri wa afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ya tarehe 12/9/2023 aliagiza ajira mpya walipwe stahiki zao, mkurugenzi pamoja na wahusika wakakaa kimya huku watumishi wakiendelea kuteseka.
Jana Mheshimiwa Mchengerwa wa TAMISEMI ametoa tamko rasmi fedha hizo zilipwe kwa watumishi bado halmashauri ya ILEJE iko kimya na hawajali.
Mkurugenzi kukaidi maagizo haya ni kwamba Yuko juu ya Sheria?
Wao wako kimya kama vile hawaelewi. Ileje imejaa mno vitisho kutoka kwa katibu ofisi ya DMO ni shida tupu. Hamna ushirikiano kabisa hasa kwetu sisi tulioko humu vijijini ndani ndani ukimuuliza anakukejeli.