Waziri Mchengerwa aagiza Fedha za Kujikimu za Ajira Mpya zilipwe kabla 30 Oktoba, 2023

Waziri Mchengerwa aagiza Fedha za Kujikimu za Ajira Mpya zilipwe kabla 30 Oktoba, 2023

Imekua ni utamaduni kwa uongozi wa halmashauri ya ILEJE mkoani Songwe kutokuheshimu kauli za viongozi hasa wanapotaka watumishi walipwe stahiki zao.

Ziara ya waziri wa afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ya tarehe 12/9/2023 aliagiza ajira mpya walipwe stahiki zao, mkurugenzi pamoja na wahusika wakakaa kimya huku watumishi wakiendelea kuteseka.

Jana Mheshimiwa Mchengerwa wa TAMISEMI ametoa tamko rasmi fedha hizo zilipwe kwa watumishi bado halmashauri ya ILEJE iko kimya na hawajali.

Mkurugenzi kukaidi maagizo haya ni kwamba Yuko juu ya Sheria?

Serikali litazameni hili kwa uzito wa kipekee.

IMG-20231003-WA0001.jpg

 
Vilio vya kujikimu ni vingi sana
Wao wako kimya kama vile hawaelewi. Ileje imejaa mno vitisho kutoka kwa katibu ofisi ya DMO ni shida tupu. Hamna ushirikiano kabisa hasa kwetu sisi tulioko humu vijijini ndani ndani ukimuuliza anakukejeli.
 
Ileje Kuna tatizo.....ikibidi uchunguzi ufanyike. Yapo yaliyojificha kuhusu hizi fedha za kujikimu.
 
Hebu watoe majina ya uhamisho dah, kiburudisho changu kinamaliza mwaka mbali na mimi! this is unfair sana.
 
Je, anafahamu kuwa tangu mwaka huu umeanza hakuna Vibali vya uhamisho vya Watumishi vimetolewa na Tamisemi lakini Watu wanahama kila siku?

Yaani ni rushwa rushwa rushwa hatari aliangalie hili kwa makini.
 
Back
Top Bottom