Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Omary Mchengerwa, akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi, uliofanyika leo Ijumaa, Oktoba 04, 2024, katika Uwanja wa Kituo cha Mabasi cha Kilombero Jijini Arusha, amesema mkoa huo umekuwa ukijichelewesha wenyewe kutokana na siasa za majitaka.
Pia, Soma: Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024
"Ninapongeza jitihada na kazi kubwa inayofanywa katika mkoa huu wa Arusha, na si siri yamesemwa mengi hapa. Nimepita mitaani nimejionea kasi ya maendeleo, lakini lazima tukiri Arusha tulijichelewesha wenyewe kwa siasa za majitaka"